Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba akiwa Handeni Vijijini: Hali ya maisha ya watanzania ni ngumu sana vyuma vimekaza nichagueni nifute umasikini katika nyanja zote

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
HALI YA MAISHA YA WATANZANIA NI NGUMU SANA VYUMA VIMEKAZA NICHAGUENI OKTOBA 28, NIFUTE UMASIKINI KATIKA NYANJA ZOTE "PROF.LIPUMBA"

HANDENI VIJIJINI

Ukuaji wa uchumi wa Tanzania haujaambatana na kasi kubwa ya kupungua kwa watu masikini. Idadi ya watu masikini kwa kutumia kipimo cha taifa cha umasikini (mtu mzima kutumia shilingi 50,000/ au zaidi kwa mwezi) imeongezeka toka watu milioni 12.3 mwaka 2011 na kufikia watu milioni 14 mwaka 2018. Kwa kutumia kipimo cha kimataifa cha umaskini, Watanzania zaidi ya milioni 27 ni masikini.

Utafiti uliofanywa na serikali mwaka 2016 kuhusu umaskini wa watoto (Child Poverty in Tanzania) ulibaini kuwa asilimia 74 ya watoto wa Tanzania wanaishi katika mazingira ya umaskini kwa tafsiri pana inayojumuisha lishe, afya, hifadhi iliyo salama, elimu, mazingira, maji na makazi.

Lipumba.jpg
 
Back
Top Bottom