Prof. Lipumba akiwa Dodoma Mjini: Mkinichagua kuwa Rais wa nchi hii nitatoa huduma bora ya afya na kudhibiti vifo vya wajawazito na watoto

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
PhotoGrid_1_20200914184403.jpg
IMG_20200914_181421_535.jpg
MKINICHAGUA KUWA RAIS WA NCHI HII NITATOA HUDUMA BORA YA AFYA NA KUDHIBITI VIFO VYA WAJAWAZITO NA WATOTO."PROF.LIPUMBA" DODOMA MJINI

Nitahakikisha kuwa Bajeti ya Wizara ya Afya inapanda na kufikia asilimia 15 ya
Bajeti ndani ya miaka 10 ijayo.

Ongezeko la bajeti litawezesha katika kuandaa miundombinu ya kisasa, wataalam, vifaa tiba na vipimo vya kutosha kwa maradhi yote.

Aidha ongezeko la bajeti litawezesha kutenga fungu maalum kwa ajili ya kukabili maradhi ya milipuko kama COVID-19 kwa kadriyatakavyojitokeza.

Ili kuhakikisha kuwa kila raia ana haki na anapata huduma za msingi za afya, Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha asilimia 70 ya Watanzania wote wana Bima ya Afya ifikapo 2025 na asilimia 100 ifikapo 2028.

Hatua maalumu zitachukuliwa kuhakikishakuwa huduma za uzazi bila malipo zinapatikana kwa kila mama mjamzito ili kupunguza vifo vingi vinavyotokea ambavyo vinadhibitika.
 
CUF uchaguzi huu wa 2020/25 huenda msipate hata mwakilishi mmoja kwenye bunge la JMT.

Mmeshuka sana kiushawishi
 
Back
Top Bottom