Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba akiwa Bunda: Serikali inajisifu kununua ndege wakati Wananchi wa hapa hawapati huduma Bora za Afya

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
Screenshot_20201006-104645.png

Serikali inajisifu kununua ndege wakati wananchi wa Bunda hapa hawapati huduma bora ya afya "Prof. Lipumba"

Akisalimia bunda, musoma

Wanawake nchi hii hawapati huduma bora wakati wa kujifungua nichagueni kuwa rais wa nchi hii nitatoa huduma bora ya afya na kudhibiti vifo vya wajawazito na watoto."

Bunda, Musoma

Nitahakikisha kuwa Bajeti ya Wizara ya Afya inapanda na kufikia asilimia 15 ya Bajeti ndani ya miaka 10 ijayo. Ongezeko la bajeti litawezesha katika kuandaa miundombinu ya kisasa, wataalam, vifaa tiba na vipimo vya kutosha kwa maradhi yote.

Aidha ongezeko la bajeti litawezesha kutenga fungu maalum kwa ajili ya kukabili maradhi ya milipuko kama COVID-19 kwa kadri yatakavyojitokeza.

Ili kuhakikisha kuwa kila raia ana haki na anapata huduma za msingi za afya, Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha asilimia 70 ya Watanzania wote wana Bima ya Afya ifikapo 2025 na asilimia 100 ifikapo 2028.

Hatua maalumu zitachukuliwa kuhakikisha kuwa huduma za uzazi bila malipo zinapatikana kwa kila mama mjamzito ili kupunguza vifo vingi vinavyotokea ambavyo vinadhibitika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom