Prof. Lipumba akana kumtetea Pinda, akiri kupigiwa simu kuhusu uwaziri

Chadema wasikubali serikali mseto. itawapaka matope
....Usiogope mkuu hakuna matope wala nini humo ndio kunafaa kabisa Magamba wakileta za kuleta yanatembezwa makonde tu kama Somalia vile adabu itakuja tu!!
 
Mmmh hapo kwenye heading mie ulintingisha; nkawa najiuliza huyu "LUPUMBA" ndo nan tena
Sasa kwenye Wizara hapa bwana Lipumba nadhani aende TAMISEMI ili aanze kuushape uchumi wetu tangu kwenye mzizi"
 
duuu hizi hbr sijui mnazipata wapi, HILO HALIWEZEKANI KWA KATIBA YA SASA. Isije ikawa mnakoncludi baada ya kuwaona CUF walivyompokea JK Tanga
 
mmmh.wakuu

mm nitafurahi sana kama akiwapa wapinzani majembe tena zile wizara tukutu,(FEDHA,Viwanda, nje,ndani,mawasiliano)inshaalah mambo yetu waTZ yatakua POA. kwani wale woote ambao kwasasa morale chini zitaamka na mafisadi watarajiwa Wataogopa.
though HAIWEZEKANI
 
Wana jf nimesikia leo katika vyombo mbali mbali vya habari kuwa,Mkuu wa Kaya yetu anatarajiwa kusuka baraza lake la kuongoza kaya yetu upya.
Safari hii ni kwa staili mpya kabisa, inasemekana ule upepo wa Zenji utafika na bara "ndoa ya cuf &ccm"
Mvumilivu hula mbivu, Mh. Lipumba aweza kuingia tena Mjengoni safari hii akiwa na TITLE kubwa, Waziri sio 'kivuli' wa ukweli kabisa.
Swali ni kama itakuwa kweli atakwenda kuwa Prof. wa mawaziri wote "mkuu wa mawaziri" au kuwa mchumi?.
Na je ni inaonyesha kuwa ni kweli wasafi ni adimu ndani ya ccm?.

Iwe kweli au si kweli, itakuwa ni matusi kwa mtu mwenye caliber ya Prof Lipumba kuwa kwenye baraza la JK, kama ni kweli JK atamuomba awe waziri i believe atakataa, itakuwa ni shame kwake, hata ma-prof na ma-Dr walioko sasa wanaona aibu kukimbia, lakini wangeweza wangekimbia.
 
WAKUU HAKUNA KIFUNGU KWENYE KATIBA KINACHO MZUIA RAIS KUTEUA MAWAZIRI KUTOKA VYAMA VINGINE, MNACHOKIONA NI MAAMUZI TU YA RAIS NA CHAMA KUFANYA HIVYO ILA HAKUNA KINACHOMZUIA, RAIS KATIKA NAFASI ALIZO NAZO KIKATIBA ZA KUTEUA WABUNGE WA VITI MAALUMU BUNGENI ANAZO NAFASI 10, KATIKA NAFASI HIZO RAIS ALITEUA WATU 3 TU KATI YA 10 MWAKA 2010, KWAHIYO AMEBAKIWA NA NAFASI 7, KATIKA NAFASI HIZO RAIS ALIMTEUA WAZIRI WA SASA WA MAMBO YA NDANI SHAMSI VUAI NAHODHA, Prof.MAKAME MBARAWA NA MAMA ZAKIA MEGHJI, KWA MAANA HIYO RAIS ANA MAAMUZI YA KUMTEUA MTU YEYOTE ANAYEONA ATAWEZA KUWA MTENDAJI MZURI KATIKA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI BILA KUANGALIA UCHAMA, LAKINI AKIAMUA KUCHAGUA KICHAMA PIA NI MAAMUZI YAKE.
 

• Rais Kikwete ashangilia wabunge kuwasulubu mawaziri

na Bertha Mwambela, Tanga


amka2.gif
WAKATI macho na masikio ya Watanzania yakielekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete aliyeahidi kufanya mabadiliko makubwa kwenye baraza lake la mawaziri, jina la Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ni miongoni mwa majina yanayotajwa kuwapo kwenye baraza hilo, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Profesa Lipumba ambaye si miongoni mwa wabunge, anatajwa kuwa mmoja wa mawaziri watakaoteuliwa kutoka nje ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Rais Kikwete ambaye tayari ameshapata baraka za Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kufanya mabadiliko, anatarajia kutangaza mawaziri wapya wakati wowote kutoka sasa baada ya mawaziri wake wanane kukumbwa na kashfa ya ufisadi iliyoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Duru za kisiasa kutoka ndani ya CCM na CUF, zinaeleza kuwa Rais Kikwete anatarajia kumwingiza Profesa Lipumba kwenye baraza lake na kwamba anaweza kumpa wizara ya Fedha na Uchumi.
“Kuna taarifa kwamba Profesa Lipumba anaweza kuwa miongoni mwa sura mpya za mawaziri. Anachoweza kufanya Rais ni kumteua kuwa mbunge, kisha kumpa uwaziri.
“Na kwa vile Bunge linatarajiwa kukutana Juni 12 mjini Dodoma, kama kuna watu kutoka nje ya Bunge ambao Rais anataka wawemo kwenye baraza lake, anaweza kuwateua kuwa wabunge na mawaziri wateule hadi hapo watakapoapishwa bungeni, ndipo ataweza sasa kuwaapisha kuwa mawaziri,” kilisema chanzo chetu cha habari.
Alipoulizwa na gazeti hili kwa njia ya simu, Profesa Lipumba alisema kuwa hawezi kuzungumzia uvumi huo kwani hata yeye ameusikia kutoka kwa watu mbalimbali.
“Siwezi kuzungumzia nafasi yangu kuhusu taarifa hiyo, lakini ukweli ni kwamba hadi sasa sijaitwa na Rais kwa ajili ya mashauriano yoyote kuhusu jambo hilo na kimsingi najua kama ana mpango huo, angeniita, lakini sijaitwa na sina taarifa,” alisema Profesa Lipumba.
Mwenyekiti huyo wa CUF ambaye ni mchumi, alisema kuwa amepigiwa simu na vyombo vya habari kadhaa pamoja na watu wengine kumuulizia jambo hilo ambalo alisisitiza ni uvumi usio na ukweli wowote.
Kwa wiki mbili sasa kumekuwa na shinikizo la kutaka mawaziri wanane wajiuzulu nyadhifa zao kutokana na wizara zao kutajwa na CAG kwamba zimehusika na ufisadi huku wengine wakitajwa moja kwa moja kufanya uamuzi wenye maslahi binafsi.
Mawaziri hao ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye amekuwa akitajwa kutaka kuvunja Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC) kwa madai ya kuficha kile kilichoitwa baadhi ya tuhuma za ufisadi katika uuzaji mali za umma ikiwemo Kiwanja Namba 10 kilichoko Barabara ya Nyerere, kwa Kampuni ya Mohamed Enterpises (MeTL).
Mawaziri wengine walio kikaangoni ni pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami. Chami ameingia katika malumbano na Naibu wake, Lazaro Nyarandu, wakitupiana mpira kuhusu kashfa ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), inayomkabili Mkurugenzi wake Mkuu, Charles Ekelege, baada ya kudaiwa kuiingizia serikali hasara ya karibu sh 30 bilioni kutokana na ukaguzi hewa wa magari nje ya nchi.
Mwingine ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, na Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu.
Waziri Nundu anatuhumiwa kuipigia kifua kampuni ya Chinese Merchants kwa ajili ya ujenzi wa gati Na 13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam huku akienda mbali na kumtuhumu Naibu wake, Athuman Mfutakamba, kwamba amekuwa akishinikiza kampuni ya China Communication Construction Company (CCCC), ipewe kazi ya kujenga magati hayo.
Wengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, ambaye wizara yake imekumbwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo uuzaji wa mazao ya misitu, ujangili na kusafirishwa wanyamapori nje ya nchi na Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika.
Waziri Mkuchika anatakiwa kujiuzulu kutokana na tuhuma za ubadhirifu katika wizara yake kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo, ambazo ni pamoja na mtandao mpana wa wizi katika wizara hiyo huku Halmashauri ya Wilaya Kishapu pekee ikiwa imepoteza sh 6 bilioni.
Katika sekeseke hilo, yumo pia Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika, Jumanne Maghembe, na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.
Shikizo la mawaziri hao kujiuzuli lilianzia bungeni baada ya wabunge wengi kutaka wawajibishwe kwa kuondolewa katika nyadhifa zao.
Katika kuongezea nguvu shinikizo lao, wabunge hao waliamua kuanzisha mchakato wa kumpiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mchakato huo ambao ulikuwa ukisimamiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, hadi Bunge linaahirishwa, wabunge 76 wakiwamo wa CCM walikuwa wameshasaini katika orodha hiyo.
Uamuzi huo wa wabunge pia uliridhiwa na kikao cha faragha cha wabunge wa CCM kilichofanyika Dodoma wakati Bunge likiendelea.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amewapongeza wabunge na kwa mapendekezo yao waliyoyatoa katika kikao cha Bunge kilichopita kutaka awawajibishe baadhi ya mawaziri walioonekana na kasoro za kiutendaji ikiwemo ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi, zilizofanyika kitaifa mkoani Tanga na kuongeza kuwa maamuzi hayo yanaonyesha uwajibikaji na ukomavu walionao wabunge katika kuisimamia serikali.
“Sijafadhaishwa wala kukasirishwa na mjadala wa wabunge; hiyo inaonyesha uwajibikaji na ukomavu wa Bunge letu katika kujadili mambo kwa uwazi na uzito mkubwa, haya ndiyo niliyoyataka na sasa mapendekezo yao yanatekelezwa,” alisema Rais kikwete.
Alisema kwa sasa anayafanyia kazi mapendekezo ya wabunge waliotaka mawaziri watimuliwe na majibu ya hatua hiyo yatatekelezwa haraka iwezekanavyo kwani aliwahi kuwaambia mawaziri watakaobainika kufanya vibaya katika wizara zao, watawajibishwa.
Alisema amefurahishwa na mjadala huo bungeni kwani awali taarifa za serikali zilikuwa hazizungumzwi wala kusikika kutokana na usiri uliopo lakini katika kipindi chake, amevunja usiri huo ili kila jambo liwe wazi na kujadiliwa kwa upana na mapendekezo yatolewe kwa uwazi bila kificho.
Aliongeza kuwa kuwajibika kwa uwazi kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), kumesaidia kuchochea kasi ya uwajibikaji na uwazi katika utendaji wa serikali kuu na za mitaa kwani sasa mapungufu yanatolewa kwa uwazi na bila upendeleo.
“Hapo awali nidhamu ya fedha katika halmashauri zetu haikuwa nzuri kwani fedha zilikuwa zinafujwa bila taarifa sahihi na ukihoji hupati majibu sahihi hili nalo lilikuwa linasababisha matumizi mabaya ya fedha za umma,” alisema.

 
itakuwa busara sana kama Lipumba akafanywa Waziri wa Mkwanja

Kama JK anataka mabadiliko lazima aanze kubadilika yeye kwani kwa staili hii hata Mrema Kiraracha AKIWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI BADO HATOWEZA KUFANYA KAZI KWA KASI
 
Wala sintoshangaa kwani hata kule Zanzibar Maalim Seif ni nani? Nawapongeza sana Chandema kwakutokubali kuungana na Cuf katika kuimarisha kambi ya upinzani! Muheshimiwa Mbowe aliliona hili mapema sana! Below is the Answer:
attachment.php
 
abdulahsaf inawezekana Mh Raisi kuteua mawaziri nje ya wabunge wa chama chake bila ya idhini ya vyama vinavyohusika na sheria (marekebisho ya katiba) ya kuratibu uanzishaji wa serikali ya mseto?
 
Last edited by a moderator:
At this moment it is going to be political suicide kama akichagua nje ya chama tawala, kwa sababu chama chake kinaamini kuwa kuna watu ndani ya CCM ambao wanaweza wizara hizo nyeti.

But again, ukifikiria kwa undani zaidi political suicide kwa nani kwani JK ndio anamalizia ngwe yake!
 
naunga mguu lakini kwa mfumo huu lipumba ataenda kuivua ch*pi phd yake
 
Hivi Prof. Lipumba ni Mbunge wa Jimbo gani vile ? anaweza kuwa Waziri bila kuwa Mbunge ? Au hata akiteuliwa katika nafasi za Ubunge alizonazo Rais, ataapishwa lini ili aweze kuwa Mbunge na kuteuliwa Uwaziri ?
 
Wala sintoshangaa kwani hata kule Zanzibar Maalim Seif ni nani? Nawapongeza sana Chandema kwakutokubali kuungana na Cuf katika kuimarisha kambi ya upinzani! Muhesimiwa Mbowe aliliona hili mapema sana! Below is the Answer:
attachment.php
Hao wanaomusalimia ni Waislamu wenzake hapo kuna udini
 
Back
Top Bottom