Prof. Lipumba akana kumtetea Pinda, akiri kupigiwa simu kuhusu uwaziri

Mlingwa

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
381
58
Wajamii, Leo Mkufunzi na mtaalamu wa uchumi Prof. Lipumba katika mahojiano ya moja kwa moja "LIVE" channel ten usiku huu kipindi cha Hamza Kasongo Hour, amekanusha kumtetea Pinda badala yake amemshangaa kwanza kutojifunza na kutenda kama Mhe. Kawawa (Waziri mkuu mstaaafu, Marehemu), pili kumwogopa Jairo na kumsimamisha Blandina.

Lakini alipoulizwa kuhusu CC ya wana CCM kuuingilia mchakato na uwezo wa Rais katika kuteua na kuwawajibisha mawaziri wake, Kwanza alikiri huu ni Uzaifu kwani Rais ni taasisi inayojitegemea na haihitaji maoni wala baraka za chama. Na alipoulizwa kuhusu tetesi kwa baraza hili Kuingiza watu wa CDM na CUF; Prof. Amekiri wazi kuwa Kasongo ni mtu wa pili kumuuliza swali hilo; amekwisha pigiwa simu na mtu furani (hakumtaja jina) kuhusiana na hilo lakini alikananusha kuwepo na mazungumzo yoyote na Ikulu ya Dar Es salaaam.

Source: Channel Ten - Hamza Kasongo Hour leo.

My take: Huenda uuongozi wa magogoni kwa mbano wa wahisani, maana naambiwa kila aendako hakuna mafanikio ya msaada, na serikali ipo hoi kifedha. Pili kujenga heshima katika miaka miwili na nusu hii iliyobaki ni kuomba rihaa ya CC ya wana CCM wenzake ili asije onekana msaliti, aweze unda baraza mseto la mawaziri.

The Truth shall be Revealed Soon, Yetu Macho.
 
nashangaa nchi zilizoendelea kama US mmeona wenyewe Obama alimteuwa mpinzani wake mama clinton,tumeona kenya,UK nk na kote huko kuna maendeleo makubwa sana.sisi walalahi wadanganyika tunangangania serikali moja kuongoza wakijifaidisha wao na hakuna uwajibikaji,katiba itenguliwe mara moja tuunde mseto kila idara wizara zitanyooka
kama tunataka maendeleo bila kuwa na mseto hatutafika popote.
 
lipumba na yeye astaafu toka enzi za mrema, marando, cheyo na yeye alikua pia anagombania urais wenzake wameshaachia ngazi na kuwaachia vijana yeye bado yupo cuf saivi ni kama ccm tu hawana sera wale...
 
nashangaa nchi zilizoendelea kama US mmeona wenyewe Obama alimteuwa mpinzani wake mama clinton,tumeona kenya,UK nk na kote huko kuna maendeleo makubwa sana.sisi walalahi wadanganyika tunangangania serikali moja kuongoza wakijifaidisha wao na hakuna uwajibikaji,katiba itenguliwe mara moja tuunde mseto kila idara wizara zitanyooka
kama tunataka maendeleo bila kuwa na mseto hatutafika popote.

Mbona Kikwete alimteua Mwandosya kuwa waziri wake? hapo hakuna tofauti mkuu, kama hujui ni bora uulize..
Kenya ni mseto baada ya vurugu hasa zilizotawaliwa na udini..,
UK vyama vya upinzani viliungana kuangusha chama kilichokuwa madarakani.
N.K I guess sababu zilikuwa kama za juu hapo..
Usiogope kuuliza next time
 
Hiyo ndoto tu ya wapinzani, hakuna cha serikali ya mseto.

Nani kakuambia kuwa hao wapinzani wanataka kushiriki kwenye serikali hii hata kama katiba ingeruhusu? Hakuna faida kwa wapinzani kudandia jahazi ambalo limeshajaa maji na liko karibu kuzama lenyewe. Wapinzani ni makini na wanafahamu kuwa wakiwa na subira, hata kama wakiamua kukaa kimya kuanzia sasa hadi 2015 magamba watajizamisha wenyewe bila mtu yeyote kuwasukuma.
 
huko ni kutapatapa kwa ccm ndio maana wanataka kuwaachia mzingo vyama vingine mimi sikubaliani na hoja ya mseto bali kama wameshindwa waachie ngazi viingie vyama vingine
 
nashangaa nchi zilizoendelea kama US mmeona wenyewe Obama alimteuwa mpinzani wake mama clinton,tumeona kenya,UK nk na kote huko kuna maendeleo makubwa sana.sisi walalahi wadanganyika tunangangania serikali moja kuongoza wakijifaidisha wao na hakuna uwajibikaji,katiba itenguliwe mara moja tuunde mseto kila idara wizara zitanyooka
kama tunataka maendeleo bila kuwa na mseto hatutafika popote.

Hivi obama na hilary wanatoka vyama tofauti eeh!!!!!!

ulifikiri unajijenga kumbe umejibomoa kabisaaaa!
 
Wajamii, Leo Mkufunzi na mtaalamu wa uchumi Prof. Lipumba katika mahojiano ya moja kwa moja "LIVE" channel ten usiku huu kipindi cha Hamza Kasongo Hour, amekanusha kumtetea Pinda badala yake amemshangaa kwanza kutojifunza na kutenda kama Mhe. Kawawa (Waziri mkuu mstaaafu, Marehemu), pili kumwogopa Jairo na kumsimamisha Blandina.

Lakini alipoulizwa kuhusu CC ya wana CCM kuuingilia mchakato na uwezo wa Rais katika kuteua na kuwawajibisha mawaziri wake, Kwanza alikiri huu ni Uzaifu kwani Rais ni taasisi inayojitegemea na haihitaji maoni wala baraka za chama. Na alipoulizwa kuhusu tetesi kwa baraza hili Kuingiza watu wa CDM na CUF; Prof. Amekiri wazi kuwa Kasongo ni mtu wa pili kumuuliza swali hilo; amekwisha pigiwa simu na mtu furani (hakumtaja jina) kuhusiana na hilo lakini alikananusha kuwepo na mazungumzo yoyote na Ikulu ya Dar Es salaaam.

Source: Channel Ten - Hamza Kasongo Hour leo.

My take: Huenda uuongozi wa magogoni kwa mbano wa wahisani, maana naambiwa kila aendako hakuna mafanikio ya msaada, na serikali ipo hoi kifedha. Pili kujenga heshima katika miaka miwili na nusu hii iliyobaki ni kuomba rihaa ya CC ya wana CCM wenzake ili asije onekana msaliti, aweze unda baraza mseto la mawaziri.

The Truth shall be Revealed Soon, Yetu Macho.

Tatizo ni nini?

Jinsi ulivyoweka kichwa cha habari na utumbo wa habari ni vitu viwili tofauti, wewe ni mhariri wa magazeti ya udaku?
 
Back
Top Bottom