Prof.Lipumba adai CCM ni chama cha Wauza Unga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof.Lipumba adai CCM ni chama cha Wauza Unga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Dec 8, 2009.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Dec 8, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,749
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..jamani hii imekaaje?

  ..madai ya Prof yana ukweli kiasi gani?

  LIPUMBA: UFISADI BADO HAUJASHUGHULIKIWA

  Na Muhibu Saidi

  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema nchi inakabiliwa na hali mbaya kimaendeleo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo tatizo la ufisadi kushindwa kushughulikiwa, huku kukiwapo tuhuma dhidi ya baadhi ya ‘vigogo’ kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

  Profesa Lipumba alitoa madai hayo alipokuwa akifungua kikao cha Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa, jijini Dar es Salaam jana.

  Alisema hadi sasa ufisadi haujashughulikiwa, ukiwamo ule uliothibitishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya nchini Uingereza, unaohusisha ununuzi wa rada ya Serikali ya Tanzania kwa bei kubwa kuliko ilivyotakiwa.

  “Hali ni mbaya nchini. Ufisadi haujashughulikiwa, hata ule wa rada uliothibitishwa na SFO,” alisema Profesa Lipumba.

  Gazeti la The Guardian la Uingereza mwanzoni mwa mwaka jana, liliandika kuwa katika uchunguzi wa SFO, iligundulika akaunti moja inayohusishwa na Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge ikiwa na zaidi ya dola za Marekani milioni 1 (sh. bilioni 1.2), iliyopo katika Kisiwa cha Jersey, Uingereza.

  Kutokana na hali hiyo, gazeti hilo liliandika kwamba, SFO ingefanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zina uhusiano na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi milioni 28 (bilioni 70), mwaka 2002. Uchunguzi wa SFO ulishakamilika.

  Gazeti hilo lilimkariri Chenge akikiri kwamba fedha hizo ni zake na akatumia fursa hiyo kukanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa nzima ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).


  Profesa Lipumba alisema wakati ufisadi ukishindwa kushughulikiwa, kuna tuhuma zilizoibuliwa hivi karibuni kutoka kwa wanaopata habari nyeti, zinazowahusisha baadhi ya vigogo kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini.

  “
  Hivyo, CCM si chama cha mafisadi tu, bali kimekuwa chama cha wauza unga,” alisema Profesa Lipumba.

  Alisema kikao cha Baraza Kuu kinatarajia kujadili ajenda 13, ikiwamo ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) inayoituhumu Tanzania na baadhi ya nchi kuhusika katika usambazaji wa silaha haramu kwa kikundi cha waasi cha FDLR cha Kongo kinachopigana dhidi ya raia wa Rwanda, mashariki mwa nchi hiyo ya Maziwa Makuu.

  Profesa Lipumba alisema ameisoma ripoti hiyo, lakini hakuona serikali ya Tanzania ikihusishwa moja kwa moja na kashfa hiyo, badala yake kuna watu wakubwa wenye vyeo, ambao wana mawasiliano na wafanyabiashara wa dhahabu wa Kongo.

  Kutokana na hali hiyo, alisema katika kikao cha Baraza Kuu wanatarajia kupitisha azimio la kuliomba Bunge kuunda kamati maalum ya kuchunguza suala hilo na kutoa ushauri kwa serikali.
   
 2. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2009
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ukifuatilia sana mwenendo wa nchi yetu, utapata ulcers. Utadundua tunaibiwa mchana kweupe na watawala wetu. Mwisho wa utawala huu na chama hiki ni lini?
   
 3. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hawa wapinzani waongee mambo mengine ya maana ufisadi siyo sera pekee itakayokupeleka ikulu..

  Chadema na CUF hakuna agenda nyingine zaidi ya hizo...issues kama education, health, ajira etc..je mkiingia ikulu mafisadi wakawekwa jela shida za wabongo zimeisha?
   
 4. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  afadhali kwa kuliona hilo,kuna hoja nyingi sana upinzani wanatakiwa kuzishughulikia.
  tunatakiwa tujue sera zao katika afya, elimu na mengineyo
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tatizo kubwa la upinzani Tanzania ni kwamba they are reactive instead of proactive. Hausikii wakisema chochote mpaka kitokee kitu CCM. CCM kukiwa na skendo za ufisadi upinzani wataanza kuongelea ufisadi, CCM kukiwa na skendo ya mikataba nk ndipo upinzani uta sikia wakinena. Inabidi watake initiative na siyo kufuata upepo wa ni wapi CCM inaelekea.
   
 6. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2009
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Utaongelea vipi mambo ya afya na mshule wakati tunapoteza karibu 100% ya budget through ufisadi?? Ukizuia ufisadi si automatically utasolve hayo matatizo ya wananchi kwa ailimia kubwa??

  JK kwa kweli ni lazima aamue kunyoa au kusuka.
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  I beg to differ,

  Huwezi kuacha kuongelea sera mbadala kuhusu afya,elimu, uchumi na ajira ukawa for 4 years tunaongelea eneo moja tu la "uwajibikaji" corruption. Hizo media coverage wanazitumia vibay na wananchi wameshawachoka!

  Nafikiri wanatakiwa watueleze tofauti yao na CCM kwenye nyanja mbalimbali na secka mbalimbali...tena watumie media sana kwa hizo issues kuliko kila wakiita waandishi wa habari ni kuongelea ufisadi ..ccm si na wao wamesema wanawashughulikia so what is difference?

  MwanaFA umepoint out kitu cha maana upinzani wanatakiwa waanze ku-create habari siyo kila siku wao ni kujibu hoja za kijinga jinga (za kina Slaa) zinazotokana na malumbano ya wana-CCM ala!
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2014
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  riz moko?
   
Loading...