Prof. Lipumba: ACT-Wazalendo imeongeza damu yenye virusi ikidhani ni damu salama

UMEN
Wanabodi,

Pamoja na tuhuma za baadhi ya wanabodi kutotazama TBC kwa hoja kuwa eti ina boa, hadi wengine kuuita TBCCM, lakini hii ndio TV yetu pekee inayoendeshwa kwa kodi zetu, hivyo kutazama TBC sio issue ya choice bali ni wajibu, hivyo tutimize wajibu wetu kwa kuangalia TBC. Mimi naangalia TBC japo nina kaugomvi kidogo na wife hapa kuhusu hili, yeye anataka kuangalia Clouds 360, hivyo sometimes lazima ubaba utumike kinguvu, TV ya kuangaliwa na baba ni TBC!, hivyo mtu kuwa mzalendo wa kweli wa taifa lako, ni pamoja na kuiangalia TV ya Taifa lako, hata kama ni kweli sometimes inaboa, uzalendo ni kuweka utaifa mbele, hivyo TV ya Taifa ndio TV yetu sisi wazalendo wa kweli wa taifa letu, hivyo tunaangalia TBC.

Leo Mwenyekiti wa CUF Taifa kwa mujibu wa Msajili wa Vyama Siasa, na kwa mujibu wa Mahakama, Prof. Ibrahim Lipumba, yuko live TBC kwenye kipindi cha Jambo.

Natoa wito, karibuni tumsikilize.

Paskali
Update 1
Prof. Lipumba amesema kazi kubwa ya kwanza ya chama chake ni kuwaleta pamoja wanachama wake, kuwa kitu kimoja kujenga chama.

Lipumba amemshutumu Maalim Seif kwa kusema analeta usultani, anachotaka yeye tuu ndicho, hivyo kitendo cha kuhamia ATC chama chenye sera tofauti kabisa na malengo ya CUF, huko sasa kutakuwa ni kumfuata mtu kama usultani na sio kufuata sera au itikadi.

Sasa wameweka kipande cha Maalim Seif Akitangaza kuhamia ACT, kwa msisitizo kuwa "umma haujawahi kushindwa hata mara moja", hivyo Maalim Seif anaamini umma utashinda ndani ya ACT Wazalendo.

Prof. Lipumba anasisitiza ofisi za CUF nchini kote ni mali ya chama cha CUF na sio mali ya mtu, hivyo amelaani kitendo cha watu kupora ofisi za CUF na kuzigeuza ni za ACT, amesema atazipigania ofisi hizo ambalo ni mali halali ya CUF, lazima zibaki CUF.

Prof. Lipumba amesema CUF bado ni chama imara, na kutolea mfano Mrema alipohama na wafuasi na wanachama wake kutoka NCCR Mageuzi kwenda TLP, sasa wako wapi?, NCCR bado ipo imara, Mrema na TLP yake wana hali gani?.

Prof. Lipumba amekiponda ACT, ukimondoa Zitto na mwana mikakati wake Prof. Kitila Mkumbo, amesema ACT ni chama hoi bin taaban kama mgonjwa mahututi aliyepo ICU akihitaji kuongezewa damu, bahati damu yenyewe aliyoongezewa ni damu yenye virusi, badala ya kuponya mgonjwa, itamuangamiza.
Prof. Lipumba amemalizia kwa kusisitiza CUF itashirikiana na vyama vyenye kutaka ushirikiano wa kweli.

My Take ya Lipumba, ningekuwa mimi, ningejiepusha na kusema jambo lolote negative kumhusu Maalim Seif, Lipumba anajua fika kuna watu wanamuabudu Maalim Seif, hivyo akisema anything kumhusu muabudu huyu, watamuona kama amekufuru.

Kipindi kimemalizika, na hapo hapo, wife akanipokonya remote, haikupita hata dakika, akabadilisha!.
Asanteni kwa kufuatilia.
Paskali
UMENIPIGA CHENGA YA MWILI MIMI NAANZA KUANGALIA SINEMA ZETU NA HUU NI UZALENDO PIA. HAHAAHAAAA MAYALA(NZALA) BAGHESHI ULIHE NIZE NAKUGISHE
 
HIVI ILE HOTUBA YA MZEE MCHONGA MAANA WENGINE UKIITA BABA WA TAIFA WANCHUKIA YA MALAYA WA KISIASA ALISEMAGA NINI VILE? UCHOCHEZI NAKO SHIDA SIKU HIZI KUNA TETESI YA KWAMBA YUKO KAKAMATWA WA KUTOA HABARI MBAYA ZA JIMBO ANAKOTOKA FARU NANI VILE
Nashukuru Paskali kwa kutufumbua macho hata wale ambao huwa hatumsikilizi Lipumba popote. Sasa umetudhihirishia kuwa; Mwizi siku zote hujihami kwa kujitetea hata kama sio yeye.
Najiuliza swali; Kati ya Maalim na Lipumba ni nani aliyejaawa na tabia hizo alizotaja? Kama ni usultani, Tangu Lipumba awe m/kiti alimpisha nani?? Tangu 1995 kila uchaguzi mkuu ni nani amesimama kwa tiketi ya CUF kwenye urais?? Mbona anajisahau kuwa hata baada ya kuutema uenyekiti akaenda kula mema mwaka mzima, si ni yeye alirudi na kuung'ang'ania uenyekiti alioutupa hadi akaupata kwa mbinde?? Ni nani anadhihirisha kuwa; Anachokitaka ndicho atakichukua hata kwa mbinde??
Kwetu kuna kamsemo; Nyani haoni kundule. Mwambie akatafute vioo viwili ajiangalie. Huenda kamzidi Maalim
 
Heri aliyeongezewa damu yenye virusi maana ataendelea kuishi kwa matumaini kuliko yule ambaye ametokwa na damu yote na amebaki bila damu. Huyo atakufa muda si mrefu, hana maisha.
 
Mkuu kama wife hapendi kuangalia TBC inawezekana hata hizi nondo unazotemaga humu JF, wife huwa anakupasia.
 
..nakumbuka wakati wa bunge maalum la katiba.

..Prof.Lipumba alikuwa karibu sana na Zitto Kabwe.

..na ukiwaangalia hao wawili, ulikuwa unaona heshima aliyokuwa nayo Zitto kwa Prof.Lipumba.

..Prof amepoteza muda wake, elimu yake, na heshima yake, kwa kujiunga na upinzani na kuishia kufanya mauza-uza ya kiwango hiki.

..aliwahi kuwa mshauri wa uchumi wa Raisi Ali Hassan Mwinyi. Ni afadhali angebaki kufanya kazi serekalini kuliko alivyoingia kwenye siasa na kujivunjia heshima namna hii.
 
Lipumba ni pumba inayopumua lakini kichwani hana taaluma tena kabakia na kamasi Debe mbili
 
Hivi DR. Rioba na wafanyakazi wa TBC wanasoma maoni haya ya wadau? Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni na wakurugenzi wake wanasoma haya? Haiwezekani kubadili mfumo wa utangazaji wa TBC ili walau uwe wa kitaifa zaidi kuliko hivi ulivyo wa ki-CCM? Kilangila.

Remote control... controller yupo sehemu anatazama tu
 
Wapinzani wa kweli huwa hawaalikwi TBCCM!!

Nakumbuka Jiwe alivyoingia Magogoni Lipumba ndio alikuwa mgeni wa kwanza kumtembelea kitaifa na wakaongea na akakili kuwa bwana mkubwa kasema atamsaidia kwenye kesi yake ambayo allifunguliwaga enzi za JK kwa kufanya mkutano usiohalali na alipigwa virungu,ndani ya wiki kesi ile ilifutwa!!!
 
Mayala hayo ni maajabu ya mwaka mpinzani wa kwanza kutumia TBC msimu huu maajabu
kwinyara-20190320-0001.jpeg
 
Wanabodi,

Pamoja na tuhuma za baadhi ya wanabodi kutotazama TBC kwa hoja kuwa eti ina boa, hadi wengine kuuita TBCCM, lakini hii ndio TV yetu pekee inayoendeshwa kwa kodi zetu, hivyo kutazama TBC sio issue ya choice bali ni wajibu, hivyo tutimize wajibu wetu kwa kuangalia TBC. Mimi naangalia TBC japo nina kaugomvi kidogo na wife hapa kuhusu hili, yeye anataka kuangalia Clouds 360, hivyo sometimes lazima ubaba utumike kinguvu, TV ya kuangaliwa na baba ni TBC!, hivyo mtu kuwa mzalendo wa kweli wa taifa lako, ni pamoja na kuiangalia TV ya Taifa lako, hata kama ni kweli sometimes inaboa, uzalendo ni kuweka utaifa mbele, hivyo TV ya Taifa ndio TV yetu sisi wazalendo wa kweli wa taifa letu, hivyo tunaangalia TBC.

Leo Mwenyekiti wa CUF Taifa kwa mujibu wa Msajili wa Vyama Siasa, na kwa mujibu wa Mahakama, Prof. Ibrahim Lipumba, yuko live TBC kwenye kipindi cha Jambo.

Natoa wito, karibuni tumsikilize.

Paskali
Update 1
Prof. Lipumba amesema kazi kubwa ya kwanza ya chama chake ni kuwaleta pamoja wanachama wake, kuwa kitu kimoja kujenga chama.

Lipumba amemshutumu Maalim Seif kwa kusema analeta usultani, anachotaka yeye tuu ndicho, hivyo kitendo cha kuhamia ATC chama chenye sera tofauti kabisa na malengo ya CUF, huko sasa kutakuwa ni kumfuata mtu kama usultani na sio kufuata sera au itikadi.

Sasa wameweka kipande cha Maalim Seif Akitangaza kuhamia ACT, kwa msisitizo kuwa "umma haujawahi kushindwa hata mara moja", hivyo Maalim Seif anaamini umma utashinda ndani ya ACT Wazalendo.

Prof. Lipumba anasisitiza ofisi za CUF nchini kote ni mali ya chama cha CUF na sio mali ya mtu, hivyo amelaani kitendo cha watu kupora ofisi za CUF na kuzigeuza ni za ACT, amesema atazipigania ofisi hizo ambalo ni mali halali ya CUF, lazima zibaki CUF.

Prof. Lipumba amesema CUF bado ni chama imara, na kutolea mfano Mrema alipohama na wafuasi na wanachama wake kutoka NCCR Mageuzi kwenda TLP, sasa wako wapi?, NCCR bado ipo imara, Mrema na TLP yake wana hali gani?.

Prof. Lipumba amekiponda ACT, ukimondoa Zitto na mwana mikakati wake Prof. Kitila Mkumbo, amesema ACT ni chama hoi bin taaban kama mgonjwa mahututi aliyepo ICU akihitaji kuongezewa damu, bahati damu yenyewe aliyoongezewa ni damu yenye virusi, badala ya kuponya mgonjwa, itamuangamiza.
Prof. Lipumba amemalizia kwa kusisitiza CUF itashirikiana na vyama vyenye kutaka ushirikiano wa kweli.

My Take ya Lipumba, ningekuwa mimi, ningejiepusha na kusema jambo lolote negative kumhusu Maalim Seif, Lipumba anajua fika kuna watu wanamuabudu Maalim Seif, hivyo akisema anything kumhusu muabudu huyu, watamuona kama amekufuru.

Kipindi kimemalizika, na hapo hapo, wife akanipokonya remote, haikupita hata dakika, akabadilisha!.
Asanteni kwa kufuatilia.
Paskali
As a journalist, Mayalla nilitegemea utakua makini katika uchaguzi wa maneno ya kuunda sentensi zako kufikisha ujumbe/fikra zako. In simple terms, nilitegemea utachagua maneno ambayo hayatazua sintofahamu na upotoshaji kwa wanaofuatilia maandiko yako. Neno kuabudu ni neno zito hasa kwa kuzingatia ni neno linalohusishwa na imani za kiroho/kidini.

Anaepaswa kuabudiwa ni Muumba wa mbingu, dunia na vilivyomo ndani yake. Kwa maana nyepesi ni Mwenyezi Mungu mmoja ambae katika ufalme wake hana mshirika wala msaidizi. Kwa maana kuabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu mmoja, huo ni ushirikina na kumkosea Mwenyezi Mungu kwa kiwango cha juu kabisa kuliko kiwango kingine chochote kile.

Kwa mantiki hiyo, kwa mwandishi wa kiwango chako ambaye unaheshimika miongoni mwa wanaofuatilia maandikio yako, kutamka kwamba Maalim Seif "anaabudiwa" si tu kwamba unajidhihirisha true yako kwa kutumia kalamu yako, lakini pia unajishushia hadhi yako kama senior journalist!!

Jitafakari na ukiwa na busara I believe utabadili fikra zako juu ya kutaka kuwaaminisha wanaofuatilia maandiko yako kwamba Maalim Seif anaabudiwa sambamba na kuabudiwa kwa Mwenyezi Mungu! Ushauri wangu wa bure kwako ndugu mayalla, tunapojadili siasa, tujenge hoja na kuzi support kwa facts za kisiasa otherwise utajipotosha na kupotosha wengine, lakini pia kuwavunjia heshima watu na imani zao.
 
Back
Top Bottom