Prof. Lipumba: ACT-Wazalendo imeongeza damu yenye virusi ikidhani ni damu salama

Kwani wale walioanzisha kauli mbiu ya." ALIPO TUPO " walikuwa wafuasi wa Maalim Seif Hamad ?
Au kwasababu Maalim hastahili kuwa na wafuasi ?
Katika mimbari za kisiasa,
Kuna wananchi wanafuata Chama bila kujari sera zake.
Wengine wanafuata msimamo wa mtu (political candidate) bila kujari Sera ya Chama.
Wengine wanafuata Sera ya chama bila kujali mtu (candidate husika)
Wengine wanafuta mtazamo wa jamii inayowazunguka kwamba wanafuata nini, iwe, mtu, sera au chama, nao wanafuata mkumbo wa wenzao.
Maalim Seif anaondoka na baadhi ya wafuasi wa CUF, lakini sio wote, ingawa inawezekana wakawa wengi zaidi kuliko watakao baki.
Lipumba ilibidi afahamu hilo tokea mwanzo kuwa wanachama wengi wa CUF wanahitaji nini hasa katika chama.








Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom