Prof. Kitilya acha janja yako ya kutaka kufukia visima kwa kisingizio cha kipindupindu

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Umoofia kwenu,

Huyu Prof. Mkumbo ameanza kujisahau kuwa ametoka kwenye imaya ya wanyonge kwa kujitoa ufahamu na kuaamka na hoja dhaifu kuwa visima ndio vinaleta kipindupindu.

Kwanza idadi ya wanaopata maji safi ni wangapi? Mtu huyu alitakiwa kuishauri Serikali itengeneze mitaro na njia za maji yaliyotuama majumbani, na Wizara ya Afya kuhakikisha vyoo kila nyumba viko salama.

Kitendo Cha Prof. Kusimama na kutangazia umma kuwa maji ya visima ndio chanzo cha kipindupindu ni wivu tu na kutaka kulazimisha watu wawekewe mita ili serikali ipate kuuza maji.

Miaka 60 hatujawahi kupata maji salama. Kwanza atuambie maji sehemu nyingi yanatoka mara ngapi? Je, yanatosha?

Pili haya anayoyasifia kweli ni salama kiasi hicho? Sehemu ngapi zinavuja na watu wanafunga na mipira michafu?

Prof. unatakiwa ukamate Bashite asafishe mji, zile fedha anazotoa ovyo angeweza kukodi magari apunguze uchafu unaonuka jiji zima.
 
Kwanza asilimia kubwa ya Jiji la Dar linamwonekano wa kipindupindu, ndio maana hata Raisi anataka kuhamia Dodoma lile shombo la feri limemchosha bila shaka.

Mvua ikinyesha kila mmoja anafungulia choo, mitaa yote inanuka kinyesi...Dar wanaovuta hewa safi ni wachache sana.
 
Prof. Unatakiwa ukamate Bashite asafishe mji, zile fedha anazotoa ovyo angeweza kukodi magari apunguze uchafu unaonuka jiji zima.
Kwa hiyo unakataa kwamba visima vidogo vinaleta magonjwa?
Pinga pinga mna kazi
 
Kwa hiyo unakataa kwamba visima vidogo vinaleta magonjwa?
Pinga pinga mna kazi
Siku zote wako wapi wasisambaze maji salama. Kipindupindu pindu kinatokana na kinyesi. Murundikano wa uchafu na yule inzi wa kijani sio visima ova.
 
Tatizo kubwa la kipindupindu ni maji yakiyotuwama kipindi cha mvua wiki chache zilizopita. Watafute long term solution si political publicity.
 
Siku zote wako wapi wasisambaze maji salama. Kipindupindu pindu kinatokana na kinyesi. Murundikano wa uchafu na yule inzi wa kijani sio visima ova.
Sio kila kitu cha kupinga
Kisima kikiwa kifupi huo mlundikano wa uchafu na kinyesi ni rahisi kusombwa na kuingia kisimani kamanda
 
Tatizo kubwa la kipindupindu ni maji yakiyotuwama kipindi cha mvua wiki chache zilizopita. Watafute long term solution si political publicity.
Maji yaliotuama ndio.hivyo visima.vifupi
Kisima gani kinafika magotini,watu wanafua,wanaoga wanyama nao wanatumia
Tubadilikeni jamani,kitila hajakurupuka
 
Maji yaliotuama ndio.hivyo visima.vifupi
Kisima gani kinafika magotini,watu wanafua,wanaoga wanyama nao wanatumia
Tubadilikeni jamani,kitila hajakurupuka
Kwanini watu wanategemea maji ya visima na si running tap water?
 
Maji yaliotuama ndio.hivyo visima.vifupi
Kisima gani kinafika magotini,watu wanafua,wanaoga wanyama nao wanatumia
Tubadilikeni jamani,kitila hajakurupuka
Tunapenda mabadiliko lakini tunakwamishwa na ziongozi hawana maono. Kitendo Cha dar kushambuliwa na magonjwa wakati kulitakiwa kuwa jiji la mfano. Taka zinakusanywa, wiki hakuna gari unategemea wale inzi wa xxm watakuacha
 
Karibia miaka 60 ya uhuru bado tuna tatizo kubwa la maji!
Maji kama huduma ya msingi sana kwa binadamu lakini hayapewi kipaombele ktk kutolewa kwa wananchi.

Pamoja na kuwa na vyanzo vya maji vya asili ambavyo Mungu ametupatia bure !

Sijui ni ujinga wa wananchi kupenda kupigapiga makofi na vigelegele vya kinafiki au tatizo ni nini?
 
Kwanini watu wanategemea maji ya visima na si running tap water?
Awamu hii imeshatumia zaidi trilioni moja kwa miradi ya maji na kufufua ya zamani
Nia ni kufanya kila chanzo cha maji kitumike kusambaza maji kupitia mabomba
Dar hali kidogo imeimarika,mpaka December visima vya huko.kimbiji vitaanza kazi
Mikoani kila siku tunaona kina Mbarawa na Aweso wanatimu wakandarasi na wahandisi nia ni kuboresha sekta ya maji
Tuliibiwa sana kwenye miradi ya maji mkuu
 
Tuliibiwa na kina nani mkuu!?
Maana kuna msemu usemwao serikali hailali hata siku moja.
 
Awamu hii imeshatumia zaidi trilioni moja kwa miradi ya maji na kufufua ya zamani
Nia ni kufanya kila chanzo cha maji kitumike kusambaza maji kupitia mabomba
Dar hali kidogo imeimarika,mpaka December visima vya huko.kimbiji vitaanza kazi
Mikoani kila siku tunaona kina Mbarawa na Aweso wanatimu wakandarasi na wahandisi nia ni kuboresha sekta ya maji
Tuliibiwa sana kwenye miradi ya maji mkuu

Dar bado maeneo mengi hayana maji kabisa,
Maeneo mengine wamejaribu kupeleka maji baada ya siku mbili tatu yamekata,
Maji hayatoki wala nini!
 
Andika hapa ni maeneo gani upate majibu stahiki

Taarifa za mrejesho watakuwa nazo maofisini za kile walichokifanya!

Na hali hiyo imepelekea hata watoe ujumbe kupitia simu za wananchi kuhusu kusimamishwa kwa kuunganishwa kwa huduma ya maji kwa muda usojulikana!

Kwa maelezo zaidi kumuulize Menes wa DAWASA Kituo cha Kawe.

Yani wananchi wamekuwa very dispointed,
Kwa miaka mingi tangu Uhuru hawajawahi pats huduma ya maji,
Haya juzi wakasema wale walipotiwa karibu na mabomba ya mchina wakae mkao wa kupata huduma ya maji,
Yakafunguliwa siku mbili sijui tatu,

Mama mmoja kasema kaishia kukinga ndoo 7 tu baada ya hapo imebaki hadithi.
 
Back
Top Bottom