Prof. Kitila tembelea Rwanda ukatuletee teknolojia ya kutengeneza magari badala ya kuzindua matela

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
5,434
2,000
Rwanda, kama Rwanda, hawana technologia ya kutengeneza magari, achilia mbali piki piki. Walichofanya ni kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji, ndipo wenye technologia na mitaji yao wakaenda kuwekeza pale.

Serikali yetu inapaswa kujifunza jinsi ya kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia technologia za kisasa na mitaji.
Tukumbuke hii nukuu ya Charles Kitwanga kutoka katika Hansard ya Bunge
Screenshot_2021-08-03-20-30-52-1.png
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
9,507
2,000
dunia ya sasa inahitaji "exposure" sana kuliko tunavyofikiri.....wenye exposure nao wamezungukwa na vilaza na kumezwa matokeo yake ni fikra duni kila siku, wengine wenye exposure wanawaza na kuamini kijamaa kulingana na malezi yao na nyuma matokeo yake wanaishia kuwaza kizamani..

Tujitahidi sana kukuza na kulea watoto kibepari karne hii vinginevyo tutapigwa kila siku..
 

kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,327
2,000
Profesa Kitila Mkumbo, Prof Kabudi, mwigulu Nchemba, doto biteko,Prof Ndalichako Joyce, Dorothy Gwajima na Godwin mollel ni afadhali Joseph Musukuma
Msukuma na kibajaji ni wapiga domo kama manara,Kishimba ndo msomi ana phd ya exposure sababu katembea nchi nyingi kibiashara
 

wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
8,035
2,000
sera zetu za kishamba.. hata aende akakae miaka mia moja.. kama hatujabadilisha sera zetu pilocy na hasa hasa katiba.. fikiria muwekezaji akutane na jitu kama sabaya.. unadhani hawahadithiani?

wana forum zao wanaambiana kuwa pale sio ..
Dangote alilalamika kwny mkutano wa Davos mbele ya matajiri wenzake Kwamba serikali ya Tz ilikua unataka hisa kwny Co.yake ya Dangote ndio maana ikawa inamuwekea mazingira magumu ya kibiashara.
 

Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
16,470
2,000
Ni ushauri tu kwa Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo kwamba afanye ziara hapo Rwanda yeye na wasaidizi wake watajifunza mambo mengi ya uchumi halisi na siyo wa kwenye karatasi.

Mungu ni mwema wakati wote!
Kumbe Rwanda wanatengeneza magari? ''Akili ni mali kila mtu ana zake.''
 

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,335
2,000
Rwanda, kama Rwanda, hawana technologia ya kutengeneza magari, achilia mbali piki piki. Walichofanya ni kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji, ndipo wenye technologia na mitaji yao wakaenda kuwekeza pale.

Serikali yetu inapaswa kujifunza jinsi ya kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia technologia za kisasa na mitaji.
Ndiho tunachotakiwa kukifanya sisi pia, kuvutia wawekezaji. Tuna sera mbovu sana. Ujamaa bado unatutesa sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom