Prof Kitila: Nimewaomba TANROADS wawape muda zaidi wakazi wa Kimara kabla ya kuwabomolea nyumba zao!

Mbunge wa Ubungo Prof Kitila Mkumbo amesema wakazi wa Kimara wasiwe na hofu kwani hatua zote za kisheria zitafuatwa kabla hawajahamishwa kupisha ujenzi wa barabara.

Mkumbo amesema kwa kuanzia amewaomba Tanroads kuwaongezea muda wakazi hao ili kupisha majadiliano ya msingi yafanyike.

Prof Kitila amesema anashirikiana kwa karibu sana na DC Herry James kuhakikisha wananchi wake wanapata haki yao ya kikatiba.

Source: ITV

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Kuna tofauti kati ya ombi na agizo. Ombi linaweza kukataliwa.
Alitakiwa kusema haya baada ya kukubaliwa na Tanroads na kupewa muda wa ziada.

Amandla...
 
Ombi la waziri?!!!
Yeye sio waziri wao. Anaomba kama mbunge. Angekuwa amesema Waitara labda lakini huyu! Yeye kama waziri alitakiwa aongee na waziri mwenzake ambae ndio angewaagiza Tanroads kupitia Katibu Mkuu wake. Hivi zilivyo ni poroja tu.

Amandla...
 
Kuna watu hawana ubinadamu wako TANROADS, ni watu 'rigid' na 'impervious' wenye roho za kishetani za awamu ya tano. Wanapaswa kustaafishwa kwa manufaa ya umma
 
Kitila anamaanisha nini au nae ana nyumba yake Kimara anataka kujipanga? inamaana hao Tanroads walikurupuka kutaka kuwavunjia hao wakazi nyumba zao kabla hawajatoa taarifa ya maandishi kwa wahusika? huu ni usanii anaofanya.
Ni mbunge wao hapo anajitafutia kura za 2025
 
Back
Top Bottom