Prof. Kitila Mkumbo: Serikali imepeleka watoto wengi shule lakini imeshindwa kuwafanya wajifunze

Oct 9, 2016
96
250
Akitoa ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali kuhusu Tanzania kupitia kipindi cha Clouds 360 leo 28/12/2016 ameonesha wasiwasi wake kuhusu hatua ya Serikali kwa miaka 10 kuwajaza wanafunzi madarasani na kushindwa kuwafanya wajifunze.

Vilevile ameelezea jinsi gani Serikali ya Magufuli ilivyojaribu kuimarisha uchumi wa nchi kwa kubana matumizi yasiyo lazima hali inayofanya watumishi wakose pesa za ziada hivyo kuathiri wajasiriamali na wananchi wengine.

Pia ameelezea jinsi gani mwaka 2016 ulivyokuwa mbaya kwa vyama vya siasa kwa kubanwa na vyombo vya dola kuendesha shughuli zao.

Amegusia jinsi demokrasia na maendeleo jinsi vinavyoshahabiana, ameshangazwa jinsi Serikali inavyominya demokrasia nchini.
 

GeeM

JF-Expert Member
Apr 11, 2014
1,899
2,000
Elimu bure ilikuwa ni kete tu ya kisiasa kwenye uchaguzi uliopita, hakukuwa na maandalizi yoyote kuimarisha miundombinu ili kupokea idadi kubwa ya wanafunzi
 

goodluck5

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
4,016
2,000
Elimu bure imekuja na changamoto kadhaa baada ya muda nazo zitatatuliwa.
Waongeze bidii katika reli ya std gauge ili kukuza uchumi kwa kasi na pia kuokoa barabara zetu.
 

stigajemwa

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
449
500
Huyu prof, ndiye aliyemuunga mkono Jpm kuwatimua wanafunzi waliokuwa wanasoma ualimu wa sayansi diploma ya miaka3 pale udom.Walimu hawa ilikuwa waje kuondoa uhaba wa walimu wa sayansi ambapo uhaba huu ndio unasababisha wanafunzi wajae shuleni bila kujifunza.Tuseme ukweli kuwa serikali hii safari bado ni ndefu kuelekea kwenyr mafanikio
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom