Prof. Kitila Mkumbo: Serikali ifanye 'National Audit' kujua mahitaji halisi ya Watumishi wa Umma

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo amezungumzia upungufu wa Watumishi wa Umma katika Sekta mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya, Kilimo, Maji na Kilimo akisema Serikali haina budi kuja na Mikakati mipya kutatua tatizo hilo

Amependekeza kufanyika Ukaguzi wa Taifa (National Audit) ili kupata mahitaji halisi ya Watumishi wa Umma. Vilevile ameishauri Serikali kuweka mazingira mazuri kwa Sekta Binafsi, akikemea kile alichokiita ni matamko ya kuisumbua Sekta hiyo
 
Hii nchi Kuna shida sehemu yaani Profesa anaongea kama mgeni nchi hii ,ukija kule bungeni kale KASPIKA nako kila kakimtaja mbunge wa kuchangia au kuuliza swali kananikera kanaongea utadhani kitoto kilichokula UBAGA mdomoni(UBAGA ni uji wa maziwa),kinachekacheka tu .
 
Kwa pumba hizi kichwani Huyu enzi za jiwe alikuwa waziri viwanda na biashara,hapo sasa ndio maana jiwe aliamua mashine kiwanda Cha sukari ikanunuliwe na tanroad
 
Nafikiri alichosema profesa hamjamuelewa.

Yeye alitaka ifanyike HR Audit ambayo kimsingi huwa inafanywa ili kujua majukumu yaliyopo na idadi ya watumishi inayotakiwa.

Bila kufanya hili Serikali inaweza kuajiri na kujikuta inawatumishi wengi kuliko kazi zilizopo.

Kwa mfano, Chuo Kikuu Huria Tanzania kina maafisa Rasilimali watu na Utawala zaidi ya kumi lkn utakuta wamewekwa kwenye vitivo ila kazi zote za kiHr zinafanywa centrally na wa kwenye vitivo kubaki bila cha maana cha kufanya na kufanya kazi ambazo Sektratari angepaswa kufanya.

Audit ingetuonyesha wapi kuna watumishi wengi ambao hawatumiki ipasavyo na hivyo kusaidia kufanya uamuzi hata wa kuwarelocate wengine.

Si vema km hufahamu jambo usimshambulie mtu tulia wenye ujuzi waje wakuelimishe.
 
Tangu akubali kununuliwa kwa Bei Chee sijui amekuwaje. Wenzake kina Sugu walipelekewa blank check waweke figure wenyewe lkn walikataa kuhama chama, huyu kirahisi tu Kama kumtongoza mwanamke wa Corner bar Sinza.
 
Nafikiri alichosema profesa hamjamuelewa.

Yeye alitaka ifanyike HR Audit ambayo kimsingi huwa inafanywa ili kujua majukumu yaliyopo na idadi ya watumishi inayotakiwa.

Bila kufanya hili Serikali inaweza kuajiri na kujikuta inawatumishi wengi kuliko kazi zilizopo.

Kwa mfano, Chuo Kikuu Huria Tanzania kina maafisa Rasilimali watu na Utawala zaidi ya kumi lkn utakuta wamewekwa kwenye vitivo ila kazi zote za kiHr zinafanywa centrally na wa kwenye vitivo kubaki bila cha maana cha kufanya na kufanya kazi ambazo Sektratari angepaswa kufanya.

Audit ingetuonyesha wapi kuna watumishi wengi ambao hawatumiki ipasavyo na hivyo kusaidia kufanya uamuzi hata wa kuwarelocate wengine.

Si vema km hufahamu jambo usimshambulie mtu tulia wenye ujuzi waje wakuelimishe.
Nchi yetu kuna wakati inashangaza sana, wakati wanasitisha kuajiri walifanya audit au hawakufanya?
Unakumbuka kwamba kuna wakati walifanya hamisha hamisha ya walimu kutoka sekondari na kuwapeleka shule za msingi kwa madai kwamba wapo wengi?

Walifanya pasipo kuzingatia uhalisia wa mambo kwenye ground, mwendelezo wa MIKURUPUKO, kitu ambacho ni hatari kwa ujenzi wa taifa!

Maeneo mengi kwa sasa yana uhitaji mkubwa wa watumishi, kwani kuna wanaostaafu na wanaofariki bila kuwa replaced, na taarifa hizo zote zinapatikana kwenye Lowson hivyo kufanya "National audit" ni ufujaji tu wa pesa za umma, kwani kila kitu kinaweza kufanyika kwa kuizingatia hiyo lowson na mambo yakaenda sawa!

Kitila anapaswa kutulia tu, kwani uprofesa wake kwa miaka mitano iliyopita ulikuwa "useless" kwa taifa!
 
Back
Top Bottom