Prof. Kitila Mkumbo: Ni hatari kwa Kanisa kutoa kauli inayosababisha maumivu na mifarakano badala ya kuponya

Waraka wa Maaskofu ni wa kichungaji, licha ya kuonya pia huponya. Kuponya kunaendana na maumivu.
 
Andiko la Padri Titus Amigu, soma hadi mwisho acha uvivu.

VIONGOZI WA DINI KUINGIA WOGA HATA KUSEMA UONGO.

Dini hazijaanza jana, wala siasa hazijaanza jana. Kwa Wakristo Wakatoliki, kwa woga, watu wanafuja vipaimara vyao na sakramenti ya Daraja inayowafanya wawe makuhani, manabii na wafalme hapa ulimwenguni. Hao wanapatwa na woga kiasi hiki wanasema uongo wa kwamba dini haipaswi kuhusiana na siasa.
Ni uongo kabisa kwani hata Pasaka yenyewe, tunayoisherehekea kila mwaka, ni matunda ya mwingiliano wa dini na siasa. Wayahudi wanaokolewa kutoka katika mikono ya Farao (mwanasiasa). Musa alikuwa mtu wa dini lakini alipambana na Farao, mwanasiasa. Kumbe, kudai dini isihusiane na dini siyo tu woga unaowashika viongozi wa dini isipokuwa ni pia ishara ya kutoyajua Maandiko. Tangu mwanzo wa Biblia hata mwisho wake, watu wa dini walihusiana na wanasiasa. Abrahamu alihusiana na Melkizedeki, mfalme. Tena alihusiana na Farao kule Misri hata akalazimika kusema uongo wa kwamba Sara si mkewe akiogopa kuuawa. Yusufu alihusiana kisiasa na Farao sawia na Putifa na mkewe.
Musa ndiyo tusiseme alihusiana na Farao. Mapigo kumi dhidi ya Wamisri shauri lenyewe lilikuwa siasa, utumwa. Na tunajua pigo la kumi na mbili, kuuawa kwa wazaliwa wa kwanza wa wanyama na wanadamu wa Wamisri ndilo lililo asili ya sikukuu ya Pasaka. Tupo pamoja?
Naomba niendelee na mifano. Samweli alihusiana na wanasiasa Sauli na Daudi. Elisha alihusiana na akina Ahabu na Jezebeli. Isaya alihusiana na akina Sairusi. Yeremia alihusiana na siasa za wafalme wengi hata akatupwa katika shimo la simba. Danieli na wenzake walihusiana na akina Nebukadreza na Belshaza. Manabii wote walihusiana na wafalme ama wakiwaunga mkono na kuwashauri au kuwaonya na kuwasahihisha. Yohane Mbatizaji alimkanya mwanasiasa Herodi Antipasi akalipia kwa shingo lake. Yesu mwenyewe alihusiana na wanasiasa kama akina Herode na Pilato. Mbona tunakumbuka kwamba Yesu alihukumiwa na Pilato,
Hatimaye, mitume nao walihusiana na wanasiasa, wengine wakali sana wakawatoa roho zao. Hata kitabu cha mwisho cha Biblia (ndiyo Ufunuo) ni mahusiano kati ya Dola ya Rumi na Wakristo. Makaisari walikuwa wanasiasa. Kaisari Konstantino aliyelisaidia Kanisa kupata nafuu ya madhulumu alikuwa mwanasiasa. Je, hatumsifu kwa kuwa mtu mwema?
Baada ya mitume, watakatifu mbalimbali walihusiana pia na wanasiasa kwa kuwaunga mkono au kuwakanya. Akina Thomas More na John Fisher walipotezaje maisha yao? Maximilian Kolbe alikufa katika muktadha gani? Kwa nini Baba watakatifu walioishi wakati wa biashara ya utumwa na hata wakati wa mauaji ya kimbari yaliyoendeshwa na Adolf Hilter dhidi ya Wayahudi wanalaumiwa kwa kutokuwa na misimamo ya kuwatetea wanyonge?
Si hivyo tu, historia ya Kanisa imejaa hati zinazohusika na mambo ya siasa. Rerum Novarum ina muktadha upi? Gadium et Spes ina muktadha gani, kwa nini tuseme Kanisa Ulimwenguni? Ulimwengu wa wapi wanaoishi wanadini peke yao pasipo dola, nchi na mataifa? Sasa inakuwaje ajabu au haramu kwetu sisi tunaoishi katika karne hii kujihusisha kwa namna yake na siasa?
Tusijipinge wenyewe. Kwa nini kila tunaposali sala za waumini tunaiombea serikali na viongozi wao? Tunawaombeaje ikiwa mambo yao hayatuhusu? Lakini ukweli ni huu. Tunaishi katika ulimwengu mmoja na wanasiasa. Ni katika ulimwengu huo huo tunamoaswa kufanya utume. Yesu Kristo hajawapa Wakristo ulimwengu wao peke yao (Yn 16:33).
Kama ndivyo, tutawezaje kuzungumzia mambo ya haki, amani na upatanisho pasipo kuwagusa wanasiasa na watawala ambao ndio wenye vyombo vinavyohusika na hayo? Anawezaje mwanadini kuzungumzia haki bila kuigusa nchi na watawala wake? Anawezaje mwanadini kuzungumzia haki na amani pasipo kuwagusa polisi na mahakimu?
Nadhani kama Wakristo wasingelikuwa raia wa nchi za ulimwengu huu na wanasiasa wasingelikuwa waamini wa dini za ulimwengu huu, dini na siasa vingeliweza kutenganishwa vizuri kabisa. Lakini kama waamini tusingelikuwa raia tusingelilipa kodi na wala tusingelishiriki chaguzi zozote na wanasiasa nao wasingelikuwa waamini tusingeliwatazamia waje kusali wala kushika amri yoyote ya Mungu. Kumbe basi, woga wetu usitufanye tuseme uongo wa kutaka dini na siasa visigusane, tunamuumiza sana Yesu aliyekuwa jasiri namba moja.
Ukweli ni kwamba wanadini siasa inatuhusu na wanasiasa dini inawahusu. Nani aliyesema mwanadini hawezi kuwa mwanasiasa na mwanasiasa hawezi kuwa mwanadini? Tusipotoshe mambo kwa woga wetu. Kumbe, kinachohitajika ni busara na kujali uwiano wa kusifiana, kuhimizana, kujadiliana na kuonyana ili wote tusiukose uzima wa milele. La sivyo, waamini na viongozi wao wasiseme wanashiriki ofisi za unabii na ufalme za Yesu Kristo!
Aidha, kukutana dini na siasa si ajabu. Kama tumetumwa ulimwenguni tukawafanye watu wote wanafunzi wa Yesu tusistaajabu kukutana na wafanyabiashara, wanasiasa, wema na wabaya. Acha nikumbuke wimbo wa zamani. Ni hivi kila mwamini, kwa sababu ya utume wake wa kimisionari ambao kwao anatakiwa kukutana na watu wote, anapaswa kujiimbisha wimbo wa zamani wa “Wote ni abiria wangu”, maana yake wanasiasa na siasa zao wamo kati ya abiria wake.

Ndimi mzee wenu Pd. Titus Amigu.
 
Exactly Mkuu! Waraka ule ni mzito haustahili kabisa kujibiwa na mtu mdogo kama huyo bali ujibiwe na mhusika Mkuu ambaye yeye ndiye chanzo cha udhalimu wa kutisha, chuki, visasi ikiwemo utekaji, utesaji na uuaji wa Watanzania wasio na hatia yoyote ile.
Anataka kuwafundisha juu ya water treatment maana maji sehemu nyingi si salama.
 
Na kuonesha kuwa kaupuuza,wanajibu Vijana kama akina mwakibinga.Saiz Mkumbo ataujibu.Waraka hauna hadhi ya kujibiwa na Rais.Na nafikiri wameona mbali sana,kujibu wa kkkt,ilitakiwa wajibu na TEC na ukitoka mwingine hivyohivyo.So serikal iendelee kuupuza hata chama naona kimeupuuza.Wajibu Vijana na watu wengine.
Tunza haya maneno yako!!
 
Jamaa Ukatibu Mkuu tu ameshaanza Kujibu Ma-Askofu akipata Uwaziri nadhani atamjibu Papa..
Hao Viongozi wanaotetewa ndiyo kwenye Kauli Tata za Utengano..Wengine wanazitolea Huko Makanisani..Lukuvi yeye na Kauli yake mbaya Kabisa Kuhusu Zanzibar..Hakuwahi hata Kuonywa na Video Zipo..Na Bado Kateuliwa Uwaziri Awamu hii...Waacheni Viongozi Wa Dini ..Msiwaingilie..
 
Habari wanaJF,

Habari nilizozipata hivi punde ni kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Kitila Mkumbo amemuandikia barua Askofu Mkuu wa KKKT, Frederick Shoo akiujibu waraka wa maaskofu hao uliotolewa Machi 24 mwaka huu..

Waraka wa Maaskofu wa KKKT ambao Prof. Mkumbo ameujibu: Maaskofu KKKT: Tunasikitishwa na matukio ya kupotezwa watu, kubanwa kwa Uhuru wa Mahakama, Bunge na Tume ya Uchaguzi...
-------

Kutoka JF:

Ni kweli. Profesa Kitila Mkumbo ameithibitishia JamiiForums kuhusu waraka aliouandika kwa Maaskofu wa KKKT. JamiiForums itawasilisha waraka huo muda wowote kutoka sasa..

Kutoka tovuti ya Mwananchi;

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Dk Kitila Mkumbo amemwandikia barua Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Askofu Frederick Shoo akitoa maoni yake binafsi kwa kanisa hilo kuhusu maudhui ya waraka wa maaskofu wa kanisa hilo uliotolewa hivi karibuni.

Waraka wa maaskofu 27 wa KKKT ulitoka hivi karibuni na ulitarajiwa kusomwa katika makanisa yote ya kilutheri Machi 25, 2018.

Katika waraka huo maaskofu walizungumzia Katiba mpya, uchumi, siasa na jamii.

“Katika kutoa maoni yangu kuhusu Waraka huo, ninalenga mambo makubwa mawili ambayo ni pongezi kwenu, na pili ni mtazamo wangu juu ya baadhi ya masuala yaliyomo katika Waraka huo,” amesema Kitila katika barua yake aliyoisaini Machi 29 mwaka huu.

Pamoja na kuwapongeza maaskofu hao, Kitila ameandika katika barua yake kuwa maudhui yaliyowekwa katika waraka wa maaskofu hao, hayaakisi hadhi na wajibu wa msingi wa kanisa.

“Kama ambavyo mmekuwa mkitufundisha siku zote, na vile tusomavyo katika Biblia Takatifu, ninafahamu kuwa kazi za msingi za kanisa ni zile ambazo Bwana wetu Yesu Kristo alizifanya alipokuwa duniani,”amesema.

Kitila ambaye ameandika barua hiyo kama muumini wa KKKT, amesema anakubaliana na mengi maaskofu waliyogusia katika Waraka huo akiamini yamefundisha na kuponya roho za waumini kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo, alichambua hoja katika maeneo matano zilizoibuliwa na maaskofu hao na kusema ni sahihi lakini akatahadharisha kuwa ni muhimu kwa kanisa kujiepusha na kuonekana lipo upande fulani katika mijadala ya kitaifa inayogusia jamii.

“Kwa kufanya hivyo, mtaepusha migawanyiko isiyo ya lazima kwa waumini ndani ya kanisa na wananchi kwa ujumla.” Amesema.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa kanisa kupima kwa umakini mkubwa uzito wa kila neno kabla ya kutoa kauli katika umma.

“Ni hatari kwa Kanisa kutoa kauli inayosababisha maumivu na mifarakano badala ya kuponya.”

Prof Mkumbo this is not your duty and functions you are required to exercise in your office nor outside it....huna hata kwa maoni tu huna hiyo nafasi. Kwanza omba msamaha sasa......kwa kanisa narudia tena you can't advice the Church of Christ on how to preach.....the gospel to the people....Watu hamuelewi kitu kimoja there's no any social organization that is the strongest but faith based one. That's why there will be no jurisdictions of where and how the Church missions itself.

Watanzania kinachoonekana sasa eti kwamba kanisa linaingilia siasa ni kwasababu ya kikundi hiki kilichopo nchini kinachojiona kina haki ya kuitiisha nchi ya Tanzania...soma Hegemony in politics ...
 
Habari wanaJF,

Habari nilizozipata hivi punde ni kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Kitila Mkumbo amemuandikia barua Askofu Mkuu wa KKKT, Frederick Shoo akiujibu waraka wa maaskofu hao uliotolewa Machi 24 mwaka huu..

Waraka wa Maaskofu wa KKKT ambao Prof. Mkumbo ameujibu: Maaskofu KKKT: Tunasikitishwa na matukio ya kupotezwa watu, kubanwa kwa Uhuru wa Mahakama, Bunge na Tume ya Uchaguzi...
-------

Kutoka JF:

Ni kweli. Profesa Kitila Mkumbo ameithibitishia JamiiForums kuhusu waraka aliouandika kwa Maaskofu wa KKKT. JamiiForums itawasilisha waraka huo muda wowote kutoka sasa..

Kutoka tovuti ya Mwananchi;

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Dk Kitila Mkumbo amemwandikia barua Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Askofu Frederick Shoo akitoa maoni yake binafsi kwa kanisa hilo kuhusu maudhui ya waraka wa maaskofu wa kanisa hilo uliotolewa hivi karibuni.

Waraka wa maaskofu 27 wa KKKT ulitoka hivi karibuni na ulitarajiwa kusomwa katika makanisa yote ya kilutheri Machi 25, 2018.

Katika waraka huo maaskofu walizungumzia Katiba mpya, uchumi, siasa na jamii.

“Katika kutoa maoni yangu kuhusu Waraka huo, ninalenga mambo makubwa mawili ambayo ni pongezi kwenu, na pili ni mtazamo wangu juu ya baadhi ya masuala yaliyomo katika Waraka huo,” amesema Kitila katika barua yake aliyoisaini Machi 29 mwaka huu.

Pamoja na kuwapongeza maaskofu hao, Kitila ameandika katika barua yake kuwa maudhui yaliyowekwa katika waraka wa maaskofu hao, hayaakisi hadhi na wajibu wa msingi wa kanisa.

“Kama ambavyo mmekuwa mkitufundisha siku zote, na vile tusomavyo katika Biblia Takatifu, ninafahamu kuwa kazi za msingi za kanisa ni zile ambazo Bwana wetu Yesu Kristo alizifanya alipokuwa duniani,”amesema.

Kitila ambaye ameandika barua hiyo kama muumini wa KKKT, amesema anakubaliana na mengi maaskofu waliyogusia katika Waraka huo akiamini yamefundisha na kuponya roho za waumini kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo, alichambua hoja katika maeneo matano zilizoibuliwa na maaskofu hao na kusema ni sahihi lakini akatahadharisha kuwa ni muhimu kwa kanisa kujiepusha na kuonekana lipo upande fulani katika mijadala ya kitaifa inayogusia jamii.

“Kwa kufanya hivyo, mtaepusha migawanyiko isiyo ya lazima kwa waumini ndani ya kanisa na wananchi kwa ujumla.” Amesema.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa kanisa kupima kwa umakini mkubwa uzito wa kila neno kabla ya kutoa kauli katika umma.

“Ni hatari kwa Kanisa kutoa kauli inayosababisha maumivu na mifarakano badala ya kuponya.”

HUYU HANA CREDIBILITY YOYOTE YA KUONGELEA MASUALA MTAMBUKA YANAYOHUSU TAIFA, AMEKUWA NA BRAINS TOFAUTI KWENYE KICHWA CHAKE ZINAZOPINGANA, MTU MNAFIKI KAMWE USIAMINI MANENO YAKE. UKIWA UNAKULA SI RUHUSA KUONGEA, AKILI YAKE IMEFUNGWA NA MLANGO WA NJAA. MSAMEHE TU.
 
Kama wajibu wao ni wa kiraia waraka ungesema hivyo; ila kwa matumizi ya titles zao inamaana kwamba wanatoa waraka huo Katika capacities zao; hivyo moja moja kuchukuliwa kama kauli ya kanisa
Ni kauli ya kanisa kwasababu kanisa limefanya sana kazi ya kuwaombea wanasiasa bila kukosolewa na wakosowaji.
 
Maprofesa wa Tanzania wengi wao hua wana walakini !!...sielew huko shuleni wanasomea nini
 
Chuki dhidi ya mtu mmoja zisije zikawaponza mnaoshabikia hizi waraka.

Je waislamu, siku wa KKKT wakitaka kugawana kila mlichonacho mtakubali?

Mnashabikia mambo yanayofanywa na KKKT, je mnahuakika gani kuwa sio kampeni za kumuaandaa mtu wao, ambaye alishasema ni zamu ya WaKKKT hatakama Muislam ana sifa zote??
 
Halafu ni hatari kwa nani dhidi ya nani???? CCM dhidi ya CHADEMA??? Au ni hatari kwa Upinzani dhidi ya CCM??? Au Islam dhidi Ukristo????

Yaani yote haya nyie wahuni mnaogopa kukosolewa....waroho wa kilakitu nyie mnakera sana kwa kweli...
 
Habari wanaJF,

Habari nilizozipata hivi punde ni kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Kitila Mkumbo amemuandikia barua Askofu Mkuu wa KKKT, Frederick Shoo akiujibu waraka wa maaskofu hao uliotolewa Machi 24 mwaka huu..

Waraka wa Maaskofu wa KKKT ambao Prof. Mkumbo ameujibu: Maaskofu KKKT: Tunasikitishwa na matukio ya kupotezwa watu, kubanwa kwa Uhuru wa Mahakama, Bunge na Tume ya Uchaguzi...
-------

Kutoka JF:

Ni kweli. Profesa Kitila Mkumbo ameithibitishia JamiiForums kuhusu waraka aliouandika kwa Maaskofu wa KKKT. JamiiForums itawasilisha waraka huo muda wowote kutoka sasa..

Kutoka tovuti ya Mwananchi;

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Dk Kitila Mkumbo amemwandikia barua Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Askofu Frederick Shoo akitoa maoni yake binafsi kwa kanisa hilo kuhusu maudhui ya waraka wa maaskofu wa kanisa hilo uliotolewa hivi karibuni.

Waraka wa maaskofu 27 wa KKKT ulitoka hivi karibuni na ulitarajiwa kusomwa katika makanisa yote ya kilutheri Machi 25, 2018.

Katika waraka huo maaskofu walizungumzia Katiba mpya, uchumi, siasa na jamii.

“Katika kutoa maoni yangu kuhusu Waraka huo, ninalenga mambo makubwa mawili ambayo ni pongezi kwenu, na pili ni mtazamo wangu juu ya baadhi ya masuala yaliyomo katika Waraka huo,” amesema Kitila katika barua yake aliyoisaini Machi 29 mwaka huu.

Pamoja na kuwapongeza maaskofu hao, Kitila ameandika katika barua yake kuwa maudhui yaliyowekwa katika waraka wa maaskofu hao, hayaakisi hadhi na wajibu wa msingi wa kanisa.

“Kama ambavyo mmekuwa mkitufundisha siku zote, na vile tusomavyo katika Biblia Takatifu, ninafahamu kuwa kazi za msingi za kanisa ni zile ambazo Bwana wetu Yesu Kristo alizifanya alipokuwa duniani,”amesema.

Kitila ambaye ameandika barua hiyo kama muumini wa KKKT, amesema anakubaliana na mengi maaskofu waliyogusia katika Waraka huo akiamini yamefundisha na kuponya roho za waumini kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo, alichambua hoja katika maeneo matano zilizoibuliwa na maaskofu hao na kusema ni sahihi lakini akatahadharisha kuwa ni muhimu kwa kanisa kujiepusha na kuonekana lipo upande fulani katika mijadala ya kitaifa inayogusia jamii.

“Kwa kufanya hivyo, mtaepusha migawanyiko isiyo ya lazima kwa waumini ndani ya kanisa na wananchi kwa ujumla.” Amesema.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa kanisa kupima kwa umakini mkubwa uzito wa kila neno kabla ya kutoa kauli katika umma.

“Ni hatari kwa Kanisa kutoa kauli inayosababisha maumivu na mifarakano badala ya kuponya.”
Unatoa vitisho ili usionekane ka unatoa vitisho ila ni ushauri. Kazi kweli kweli
 
Sio mchaga mkuu,huyu ni kabila moja na Mwigulu. Mimi wala sishangai coz huwa ni watu wasio na msimamo
Aisee kakosa msimamo yeye, mimi siwezi kushiriki madhaifuyake kisa naye ni mnyiramba mwenzangu.
Hata mimi mnyiramba mwenzake nimefedheheka na huu waraka wake, nasema ni udhaifu wake sio kabila letu tukufu.
 
Huko kwao Mgela mpaka leo hawaamini kama ndugu yao kasanda. Gyule mmoja akanambia kipindi kile anachambua mambo kwenye TV wanakijiji wanakaa kumsikiliza sha mkumbo. Leo hii hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom