lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,147
- 33,297
Wapendwa JF members salaam,
Napenda niwashirikishe hofu yangu juu ya uongo wa Zitto,Kitila,Mwigamba and na washirika wao hasa waliohamia ACT-Wazalendo wakitokea CHADEMA.
Mtanzania yeyote aliyeishia darasa la saba wa umri wa Zitto na wenzake anaweza kusoma,kuelewa na kuelezea vizuri sana juu ya UJAMAA na UBEPARI kwani tumejifunza vizuri juu ya ujamaa hapa Tanzania kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu.
Sasa Zitto alijiunga na CHADEMA tangia akiwa chuo kikuu,Kitila alijiunga na CHADEMA tangia akiwa Mwalimu wa wanafunzi wa chuo kikuu na Mwigamba alijiunga na CHADEMA vilevile pengine akiwa na elimu ya juu, na hata kwa wafuasi wao.
Zitto amekua mbunge kupitia CHADEMA kwa miaka kumi,Kitila pia amekua mwanachama wa CHADEMA kwa miaka mingi tu, na akaweza hata kuandika ILANI ya uchaguzi ya CHADEMA.
Sasa najiuliza Zitto na wenzako wakati mnajiunga na CHADEMA hamkusoma katiba ya CHADEMA?
Haukujua kuwa CHADEMA sio chama cha kijamaa?
Haukujua sera ya CHADEMA?
Je, UJAMAA wako na wenzako umekuja baada ya kufukuzwa CHADEMA?
Kama nyie ni wajamaa kwanini hamkujiunga na chama cha kijamaa CCM ingawa kwa CCM ujamaa ni jina tu na umebaki vitabuni.
Hata kama CCM waliacha kuufuata Ujamaa kwanini hamkujiunga ili mtumie ushawishi wenu kuirudisha CCM?
Mtaniambia kuwa ingekua ngumu kuwarudisha wana CCM ndani ya Ujamaa,sawa.
Sasa kama ninyi ni Wajamaa kwa nini mliingia chama CHADEMA kisichofuata imani mnayoiamini?
Mlitegemea nini kwa miaka yote mliyokua mnadai mmeijenga CHADEMA isiyofuata Ujamaa huku mkijua chama mnachokijenga kwa miaka zaidi ya kumi hakina sera ya Ujamaa mnayoiamini?
Au mlitegemea kufanya mapinduzi ya sera. Je mlijaribu kushawishi wenzenu?
Zitto Ujamaa umeanza baada tu ya kufukuzwa CHADEMA.Zitto unataka kutumia utamu wa sera za UJAMAA ili kugawa kura za wapinzani ili CCM ipite kirahisi.
Ujamaa na Azimio la Arusha ni vitu vizuri sana lakini hata founder wake hapa nchini JK Nyerere alikili kuwa kuvihubiri hapa Tanzania inabidi uwe na akili ya mwendawazimu.
Zitto, ACT-Wazalendo ni mkakati maalum wa kuirahisishia ushindi CCM.Mkuu unafurahi CCM iendelee kutawala?
Mkuu kuna maisha zaidi ya siasa na kesho kwa MUNGU tuna maswali ya kujibu.UJAMAA wako umeibuka ghafla sana siku zote ulikua wapi usianzishe chama cha Kijamaa kwa amani tena kwa kuondoka CHADEMA kwa amani?