Uchaguzi 2020 Prof. Kitila Mkumbo kuzindua kampeni zake za Ubunge Jimbo la Ubungo Ijumaa Septemba 4

Minaely mimi

New Member
Aug 29, 2020
2
2
Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Prof. Kitila Mkumbo, ambaye ni mwanazuoni mbobevu na mkazi wa Ubungo kwa zaidi ya miaka 20, kesho atazindua rasmi kampeni zake kwa jimbo hilo.

Prof. Kitila ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa mshindi wa jimbo hili, atazindua kampeni hizo katika viwanja vya EPZA vilivyo external karibu na hostel za abibo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Profesa Kitila kugombea jimbo hili ila tayari ana uzoefu mkubwa katika siasa za tanzania na utumishi Serikalini, kwani amekua mshauri mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo kabla hajateuliwa kuwa Katibu Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Prof. Kitila Mkumbo anagombea jimbo hili ambalo kwa miaka kumi lilikuwa chini ya umiliki wa CHADEMA.

Ni zamu sasa ya wana ubungo kupata sera na uongozi utakaowasogeza mbele hivyo wanahimizwa kesho kujitokeza kwa wingi kumsikiliza.

IMG-20200903-WA0010.jpg
 
Yupo Vizuri Sana
Namfahamu akiwa Rais & Spika nami nikiwa Mbunge pale Mlimani.

Anamisimamo ya nguvu sana na aliwahi kugoma kutulipa posho za KIKAO cha Bunge kilichoendelea zaidi ya saa 6 usiku. Tulidai posho kwa hoja kuwa tumefanya kikao kwa zaidi ya siku moja bila kupumzika. Pamoja na vitisho vyote ALIGOMA KULIPA ila alitoa soda!

Akiomba kura za Urais pale Nkuruma alitoa Hotuba fupi sana na yenye maneno ya Hekima ya juu na Wanafunzi wote walimshangilia na alipita kwa kura nyingi sana.

Makamu wake alikuwa Dr Francis Michael na Katibu alikuwa Shilinde Masalu C.K.
Kitaaluma yupo Vizuri na Kiutendaji yupi Vizuri.

Kitu pekee alichoniudhi Ni kutuacha Kwenye mataa pale Ubungo darajani siku tuliyoandamana kudai posho zetu.
Hatukujua alitorokea wapi zaidi ya kutuacha tukichezea kichapo cha FFU. Kwa hilo sijamsamehe hadi leo!
 
Back
Top Bottom