Prof. Kitila Mkumbo atoa neno kwa Rais baada ya kuapishwa

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Prof. Kitila amesema katika maisha yake ametumia muda mwingi kuihoji na kuuliza maswali hasa serikali lakini kwa sasa Rais amempa kazi ya kushiriki kikamilifu na kujibu alichokuwa anakihoji serikalini.

''Ukipewa kazi na Mkuu wa Nchi unashukuru Mungu na jukumu langu ni kufanya kazi kwa bidii. Ninaahidi nitakusaidia wewe na Mweshimiwa Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuhakikisha kwamba ajenda yako ya kuwafikia Watanzania na kuwaboreshea maisha tunaifanikisha'' Prof. Kitila Alisema.

VIDEO:

1cdbncbb.jpg
 
Njaa mbaya sana
Ni kweli njaa ni mbaya kwa sababu hakuna binadamu anaweza kuishi huku akiwa na njaa.

Kwani wewe ungeteuliwa ungekataa au ndio yaleyale ya unafiki wa kusema Prof Kitila ana njaa wakati hata wewe kama ungeteuliwa ungekubali?

Inashangaza kuona kuna baadhi ya watu/wanasiasa wanamwambia Prof. Kitila asikubali uteuzi wakati wao wameandika barua ya kumuomba Rais Magufuli aonane nao. Wao kushirikiana na Rais/serikali ni sawa lakini mwingine akifanya wanadai ni mchumia tumbo.

Watanzania tumekuwa wanafiki wa kiwango cha juu!

Charity begins at home.
 
Njaa mbaya sana
Jamani tupunguze chuki dhidi ya serikali !ina maana mpaka leo hamuamini kuwa Magu ni Rais wenu?na kwamba anaweza kumteua mtanzania yeyote kushuka wadhifa wowote ule ambao hauna mashart ya kiitikadi?kwamba Kitila anapaswa kuwa mpiga kelele tu si mtendaji na kuteuliwa kwake ni ubatilifu?mimi naona Kitila kapewa nafasi ta kuyafanya aliyo yapigia kelele ikiwezekana amchague na lisu kuwa Jaji mkuu au mwanasheria mkuu!
 
Tunahitaji afanye kazi kwa vitendo na si maneno matupu ambayo hayana msaada wowote kwa Taifa letu. Sasa yupo uwanjani sijui kama atayaona makosa waliokuwa wakiyafanya watendaj wengine tofauti na unapokuw nje ya uwanja. Naimani atakuw ameusoma mchezo
 
Nakuambia Mungu huyu, angeweka vipande vitatu vya mbao tumboni, ina maana hakuna kula, acha masihala ndio ungeona mkuu. Nakuhakikishia wote tungesimamia tunayoyahubili.
 
Na ameapa kwa kuwa ataiheshimu na kuilinda katiba, daaah, njaa mbaya sana, katiba hii chakavu aliyokuwa anaiponda kila siku na kudai mpya, leo anamuapia mwenyezi Mungu kuwa atailinda? Njaa mbaya sana.
 
Back
Top Bottom