Prof. Kitila Mkumbo aombwa kugombea urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo

Prof. Kitila Mkumbo aombwa kugombea urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo

Monday, August 17, 2015

Mwakilishi wa chama cha ACT WAZALENDO na Katibu mkuu wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akipewa maelekezo na Afisa tawala wandamizi wa Tume ya uchaguzi (NEC),George Baasha kuhusiana na vitu vinavyotakiwa kwenye uchaguzi mkuu pamoja na kampeni zitakazo anza hivi karibuni.

Katibu mkuu wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akimwakilisha Dkt. Kitika Mkumbo kupokea fomu ya kugombea nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT WAZALENDO amechukua fomu hizo leo katika ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam.

Katibu mkuu wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akionyesha fomu ya kugombea nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT WAZALENDO mara baada ya kupokea fomu hiyo katika ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam.

Katibu mkuu wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam. Picha na Avila Kakingo

Na Chalila Kibuda

CHAMA Cha ACT-Wazalendo wamechukua fomu kwa ajili ya mgombea urais atakayepeperusha bendera katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya kuchukua fomu ya urais,Katibu Mkuu wa Chama hicho,Samson Mwigamba amesema kamati kuu imempitisha Profesa Kitila Mkumbo kuperusha bendera katika uchaguzi utaofanyika mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.

Mwigamba amesema kuwa wamejipanga katika kushinda uchaguzi huo kutokana na watu waliokupwepo katika chama hicho ni wazalendo wa vitendo.

Amesema kuwa watu amesema chama chao ni kidogo lakini wameweza kusimamisha wagombea wa ,Udiwani,pamoja na ubunge ambapo katika vyama vyote vilivyoanizisha kwa kipindi kifupi vilishindwa kufanya hivyo.
Aidha amesema wanamuamini Profesa Mkumbo kutokana na malengo ya uanzishaji wa chama hicho kwa kutoa mchango mkubwa hivyo lengo la chama limetimia.

Amesema ambao wanahamia katika Chama hicho watapimwa uadilifu wao katika kuweza kuwatumikia wananchi wanao wachagua katika nafasi mbalimbali.

ACT-Wazalendo wamechukua fomu kwa kuwa idadi ndogo kuliko vyama vyote na utulivu ulitawala katika ofisi za tume ya Tifa ya Uchaguzi (NEC).

at 10:47 AM
 
Kitila Mkumbo ameshawachomolea mbona? yaani abebe aibu ya kuzomewa kwenyemajukwaa? hahahhhhaa halafu wenzake wapate ubunge??
 
Last edited by a moderator:
Hakuna nchi Afrika iliyowahi kutawaliwa na profesor ktk nafasi ya urais.hii ni kwa sababu profesa si mtu tamaa ya maendeleo kwa kwa kasi kama watu wanavyotaka kwa kuwa ameshafikia ngazi ya AHA stage na yeye ktk hatua hii anaamini mtu akila ,akilala na akawa na uwezo wa kusagiri baasi wakt watu wanahitaji zaidi.

Mfano.maprofesa ukiangalia magari yao pale Udsm ni Double cabin tu tena ya zamanii.

Profesors huea ni washauri tu wa serikali.Nchi mbili tu Afrika ziliwahi kutawaliwa na maprofesa.

Act jueni hilo siasa na Utawala si lazima elimu kubwa ni Busara.
 
Wewe --------- si alisema, mgombea urais wao atatikisa sana, ni mmoja wa vigogo wakubwa? Duh nimemkubali.
 
Hao nao wanataka urais,ila nashukuru kunipatia kichekesho cha jumatatu
 
Hawa ni wa kupuuzwaa, kuwajadili watapata sifa zisizo wastaili
 
Mkuu acha uwongo basi, Tanzania ipo Afrika na rais wake wa sasa ni profesa.
 
Hakuna nchi Afrika iliyowahi kutawaliwa na profesor ktk nafasi ya urais.hii ni kwa sababu profesa si mtu tamaa ya maendeleo kwa kwa kasi kama watu wanavyotaka kwa kuwa ameshafikia ngazi ya AHA stage na yeye ktk hatua hii anaamini mtu akila ,akilala na akawa na uwezo wa kusagiri baasi wakt watu wanahitaji zaidi.

Mfano.maprofesa ukiangalia magari yao pale Udsm ni Double cabin tu tena ya zamanii.

Profesors huea ni washauri tu wa serikali.Nchi mbili tu Afrika ziliwahi kutawaliwa na maprofesa.

Act jueni hilo siasa na Utawala si lazima elimu kubwa ni Busara.
Kiswahili umepatia lakini kiingereza rudi darasani
 
Mate uwe unajisomea kabla ya kufichua upompopo wako kwenye kadamnasi. Unamjua Prof Thabo Mbeki -S.A? John Atta Mills -Ghana?Prof Yusuf Lule wa Uganda?
 
Nakubaliana na Mkumbo, angalau amejitambua na kujua kwamba hakuna haja ya kuingia kwenye game ambayo unajua wazi kabisa kwamba hutaambulia chochote.
 
Back
Top Bottom