Tetesi: Prof. Kitila Mkumbo kuchuana vikali na Nyalandu jimboni

Kitila atashinda kirahisi sana ....strategically yatakuwa yale yale ya 2015 ....Chadema watatumia muda mwingi kujibu tuhuma za mgombea wao ....hili hawataweza kulikwepa ....Kama kweli Kitila atasimama then ndio mbunge mtarajiwa ....
Wakati Kitila akimwaga sera wao chadema watakuwa bize na madodoki.
 
Lumumba mmeishiwa.
Dr Nyalandu, khaaa
TEC imetangaza uchaguzi lini?

If wishes were horses
 
IMG_4052.jpg

Huyu ndiye mtu aliye ijenga chadema jimbo la singida kaskazini kwa zaidi ya miaka kumi Huyu ndiye aliye kuwa mpinzani wa nyarandu jimboni
 
Mnyiramba kudharaulika kwa mnyaturu sikubaliani na wewe maana haya makabila ni watani wa jadi afu mnyaturu ndiye anayedharaulika maana mnyaturu shule hana wakati mnyilamba kasoma
Wasomi wengi toka singida ni wa kutoka ilamba maana kule wamisionari ndiko walijichimbia wakaanzisha shule watu walielimika mapema kwa hiyo mnyiramba ni msomi,maprof na ma DR ni wengi na ndio maana wanamdharau mnyaturu
Ila mnyaturu kumdharau mnyilamba sikweli mkuu,mnyaturu kichwani hana shule mwaarabu alimbania kumpa elimu alimwachia dini tu ndo maana utakuta ata mnyaturu aliyesoma ni mkristo
we hujui hata usemacho
Dungunyi seminary iko wapi? kwa wanyiramba?
Diaghwa seminaei iko wapi? lwa wanyiramba?
Nitajie walau wasomi kumi wanyiramba
alafu nitajie umuhimu wao katika nchi
wanyiramba ni watu wenye roho mbaya tu...ndio wanyaturu wanawajua hivo
so take it from me ,,,mnyiramba hata iweje wanyaturu wa Ilongero hawawezi kumchagua
 
Hayawi hayawi, sasa yamekuwa. Kile kitendawili kigumu kilichokuwa kimekosa majibu sasa majawabu yake yako bayana! Kuna kila aina ya dalili CCM wanamuandaa Prof Kitila Mkumbo kuchauana vikali na Dr Lazaro Nyalandu katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika kumchagua mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini baada ya Dr Nyalandu kujiondoa CCM na kujiunga CHADEMA hivi karibuni.

Wataalamu wa masuala ya siasa wanabainisha kuwa CCM wamejithathmini na kuona wamteue Prof Kitila kuwa mgombea wao ili achuane na mgombea wa upinzani, Dr Nyalandu. Sababu zinazopelekea CCM walenge kumteua Prof Kitila ni kutokana na hali ya siasa za Kanda ya Kati ambazo hazitabiriki hata kidogo. Inadhaniwa Prof Kitila ana uwezekano wa kumuangusha Dr Nyalandu katika uchaguzi huo kwa kuwa bado ana chembechembe za upinzani, hivyo kuweza kujizolea mashabiki kutoka upande wa upinzani pamwe na upande wa CCM.

Aidha,upande wa CHADEMA nao wanatamba kuibuka washindi katika jimbo hilo kutokana na kuwa na hazina nzuri ya wafuasi, huku wakitarajia kupata "kura za chuki" za kutosha kutoka kwa wanaCCM, hasa wale wanaokerwa jinsi nchi inavyotawaliwa kwa sasa.

MAONI YANGU
Mimi kete yangu naitupia kwa Dr Nyalandu kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo mdogo kwa kuwa bado ana wafuasi wa kutosha kutoka upande wa CCM, hasa wale wasioridhishwa jinsi CCM inavyomwandama Dr Nyalandu na kashfa za kutunga huku wakijua fika utumishi wa Dr Nyalandu haujawahi kuwa na doa lolote.

Je, wewe dau lako unalitupia kwa nani na kwa sababu gani? Toa maoni yako sasa!
WOTE wajipange vyema , "NITASIMAMA NAO "
 
Hii habari ya wafia chama ndiyo nini, unaona mambo anayo fanya Mugabe zimbabwe kisa eti aliipigania nchi kwa hiyo anaona ni bora amkabidhi nchi mkewe.? Aibu. Haya majuzi Museveni naye amewaambia wananchi wake kuwa kama kuna mtu aliwadanganya kuwa mpiganaji huwa anastaafu wasahau habari hiyo . Aibu kubwa.
 
Hayawi hayawi, sasa yamekuwa. Kile kitendawili kigumu kilichokuwa kimekosa majibu sasa majawabu yake yako bayana! Kuna kila aina ya dalili CCM wanamuandaa Prof Kitila Mkumbo kuchauana vikali na Dr Lazaro Nyalandu katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika kumchagua mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini baada ya Dr Nyalandu kujiondoa CCM na kujiunga CHADEMA hivi karibuni.

Wataalamu wa masuala ya siasa wanabainisha kuwa CCM wamejithathmini na kuona wamteue Prof Kitila kuwa mgombea wao ili achuane na mgombea wa upinzani, Dr Nyalandu. Sababu zinazopelekea CCM walenge kumteua Prof Kitila ni kutokana na hali ya siasa za Kanda ya Kati ambazo hazitabiriki hata kidogo. Inadhaniwa Prof Kitila ana uwezekano wa kumuangusha Dr Nyalandu katika uchaguzi huo kwa kuwa bado ana chembechembe za upinzani, hivyo kuweza kujizolea mashabiki kutoka upande wa upinzani pamwe na upande wa CCM.

Aidha,upande wa CHADEMA nao wanatamba kuibuka washindi katika jimbo hilo kutokana na kuwa na hazina nzuri ya wafuasi, huku wakitarajia kupata "kura za chuki" za kutosha kutoka kwa wanaCCM, hasa wale wanaokerwa jinsi nchi inavyotawaliwa kwa sasa.

MAONI YANGU
Mimi kete yangu naitupia kwa Dr Nyalandu kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo mdogo kwa kuwa bado ana wafuasi wa kutosha kutoka upande wa CCM, hasa wale wasioridhishwa jinsi CCM inavyomwandama Dr Nyalandu na kashfa za kutunga huku wakijua fika utumishi wa Dr Nyalandu haujawahi kuwa na doa lolote.

Je, wewe dau lako unalitupia kwa nani na kwa sababu gani? Toa maoni yako sasa!
Bado hawa wafuasi wana akili za panzi
 
Vyama vya siasa siku hizi wanajali sana idadi ya wabunge kuliko viwango vya mbunge husika, mtu kama Kitilya atawachanganya tu wananchi wa jimbo lake akipata ubunge badala ya kuwa msaada. Soma mawazo ya kitilya alivyokuwa CHADEMA halafu fuatilia alichokuwa anaamini alipojiunga na ACT wazalendo na umsikilize anachozungumza baada ya kurudi CCM. Mtu kama huyo unaona kabisa focus yake ya maendeleo ina​
 
Hapo ndio naamin vyama vyetu vya siasa viongozi wao wanafikiria kwa makalio badala ya vichwa.... hv mtu kang'atuka hata mwez hujafika then mnampa nafas ya kugombea ubunge ... unazani watajisikiaje wale wafia chama
vipi kuhusu ccm wanafikiria nn Maana hata Kitila alikuwa ACT
 
Hapo ndio naamin vyama vyetu vya siasa viongozi wao wanafikiria kwa makalio badala ya vichwa.... hv mtu kang'atuka hata mwez hujafika then mnampa nafas ya kugombea ubunge ... unazani watajisikiaje wale wafia chama
Mkuu unapaswa kusoma vizuri katiba za vyama ili uelewe sifa za mgombea. Kila mwanachama ana haki ya kugombea pasipo kujali alijiunga lini na chama. Katiba haziko kibaguzi kama unavodhani.
 
Back
Top Bottom