Prof.Kironde-Wakoloni waliwekeza na kujenga miundo bora Imara kuliko Utawala wa miaka 50 wa CCM

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,599
3,220
GreatThinkers,
Sikiliza TBC ingawa akiongea mazuri yao wanainterfere matangazo ila ni bora kuishi na wakoloni weupe kuliko wakoloni weusi. Acheni Mapr
Kwa kifupi anasema,
-Wakoloni walianzisha mashamba makubwa sana na mengi ya mkonge-sasa hivi hayapo
-Wakoloni walijenga mashule, mahakama,majengo ambazo zinadumu hadi leo, mfano Ilala quarters,Upanga quarters na Kurasini
-Walijenga Reli ya kati ambayo hadi leo lakini imeshindwa kutunzwa
Nitaendelea kuwapa updates
 
Umenikurupusha kumtazama Prof then nawasha tv naye anaconclude..
 
Dogo ana akili sana. heri tz warudi wakoloni kuliko chamachetu.

Kinachonishangaza hata hao wanaokata kata matangazo ni kwa faida ya nani mimi,wao na ndg zao wanapigikaga maisha magumu,shule za kata zilizojengwa miaka 10 ijayo zaidi ya 50% zitakuwa hatarishi kwa walimu na wanafunzi.
Mijitu mingine aisee
 
Mkuu hii ndio fact. Jaribu kuangalia shule zinazoitwa Ilboru, Iyunga, Ifunda, Malangalai etc uangalie quality yake halafu linganisha na shue zilizojengwa baada ya uhuru. Angalia barabara zilizojengwa na mwingereza linganisha na za sasa. Barabara ya Port Access na Maendela ya sasa haifanani hata kidogo kwa quality. Angalia madaraja ya mwingireza ulinganishe na ya sasa utaona tofauti kubwa sana.

Anachosema Profesa Kironde hata hakihitaji uprofesa kukiona. Hatujajenga uwanja wa ndege hata mmoja toka mkoloni aondoke, zaidi ya ile Runway KIA. that is why we need to be serious.
 
angalau serikali yetu inaweza kujivunia kuwa ilimsomesha Professor Kironde.........lol
 
Wenzetu na Akili zao fupi watambrad Prof Kironde mpizani! Inahitaji uwe mjinga kufurahia serikali ya CCM gambazi!!
 
Ukweli ni kuwa hutijawahi kama nchi kuwa makini katika kusimamia rasirimali zetu wakiwemo watu. Ubinafsi na kutokukubali kwa watawala kukosolewa ndiyo sala ya kila siku. Uongo na porojo kila siku.
 
Mkuu hii ndio fact. Jaribu kuangalia shule zinazoitwa Ilboru, Iyunga, Ifunda, Malangalai etc uangalie quality yake halafu linganisha na shue zilizojengwa baada ya uhuru. Angalia barabara zilizojengwa na mwingereza linganisha na za sasa. Barabara ya Port Access na Maendela ya sasa haifanani hata kidogo kwa quality. Angalia madaraja ya mwingireza ulinganishe na ya sasa utaona tofauti kubwa sana.

Anachosema Profesa Kironde hata hakihitaji uprofesa kukiona. Hatujajenga uwanja wa ndege hata mmoja toka mkoloni aondoke, zaidi ya ile Runway KIA. that is why we need to be serious.

Ingawa nakubaliana 100% na mtizamo wa profesa na kwa sehemu kubwa nakubalina nawe kwenye mtizamo wako, ninapenda pia nisikubaline nawe katika sehemu ndogo mbili kama ifutavyo.

(a) Ile barabara ya Port Access ambayo ilikujwa bdilishwa na kuitwa Nelson Mandela Expressway mwaka 1990 haikujengwa na Mkoloni. Ilijengwa na watanzania wenyewe, na contractor wake alikuwa ni MECCO; kampuni ya umma ambayo ilijenga soko la Kariakoo, NIC kitega uchumi miaka hiyo ya sabini.

(b) Uwanja wa ndege ambao leo hii unaitwa JKN ahukuach hivyo na mweingereza. Uwanja ule ulijengwa mwanzoni mwa miaka ya themanini na kampuni ya kifaransa ilikouwa inaitwa Coogees wakati huo. Vile uwanja wa KIA haukuwapo kabisa bali ulijengwa na serikali ya Tanzania mwishoni mwa miaka ya sabini.

Inasaidia sana iwapo tunakuwa tunejanga hoja zetu tukiwa na uhakika nazo. Prosa Kirone alikuwa anazungumza hali ya nchi kwa jumla, na sidhani kama anegtumia mifano yako hiyo niliyosaqhihisa hapo juu.
 
Kampuni ya kifaransa naona unzugumzia ile terminal mpya ambayo hata vyoo vayeke vinanuka, na huenda ni airport pekee ambayo maji huwekwa kwenye mapipa na ndoo, ambako escalator huwa haifanyi kazi kwa miezi sita. Kimsingi ni uwanja uleule hakuna kipya pale. Inafact kampuni ya Ufaransa haikujenga uwanja mpya, nakumbuka tulijadili sana bunge ufisad wa kununua madeni na kujenga ule uwanja.

So, inawezekana kuwa sina kumbukumbu vizuri kuhusu MECCO, kama kweli MECCO ilikuwa na uwezo wa kujenga barabara ile basi naona leo Tanzania tungekuwa na barabara nzuri sana. Na MECCO na fahamu ni kampuni iliyokuwa na engineers wengi kutoka Soviet union na wakatulazimisha kununua magari yao mengi ambayo sasa yanaoza tu. Mkuu sijui kama unakumbuka kampuni moja inaitwa MOWLEM, kajaribu kuikumbuka kidogo na uangalie kazi zao.
 
MECCO walijenga hii bara bara ya kigogo magomeni, na hata kabla ya kwaisha ilikuwa na mahandaki. Mimi nashangaa hawa JF wanaozungumzia mambo bila kuwa na uhakika. Lakini nafikiri umenjibu vizuri.
 
mecco ilikuwepo na ilifanya kazi nzuri kabisa kabla ya watanzania kufahamu lugha ya ufisadi na uhujumu uchumi hata huku kwetu tuna mtaa unaitwa Mecco ulipimwa na kuwekewa infrastructre zote na Mecco kabla ya mladi kuhamishiwa kwa wajanja.
 
Kampuni ya kifaransa naona unzugumzia ile terminal mpya ambayo hata vyoo vayeke vinanuka, na huenda ni airport pekee ambayo maji huwekwa kwenye mapipa na ndoo, ambako escalator huwa haifanyi kazi kwa miezi sita. Kimsingi ni uwanja uleule hakuna kipya pale. Inafact kampuni ya Ufaransa haikujenga uwanja mpya, nakumbuka tulijadili sana bunge ufisad wa kununua madeni na kujenga ule uwanja.

So, inawezekana kuwa sina kumbukumbu vizuri kuhusu MECCO, kama kweli MECCO ilikuwa na uwezo wa kujenga barabara ile basi naona leo Tanzania tungekuwa na barabara nzuri sana. Na MECCO na fahamu ni kampuni iliyokuwa na engineers wengi kutoka Soviet union na wakatulazimisha kununua magari yao mengi ambayo sasa yanaoza tu. Mkuu sijui kama unakumbuka kampuni moja inaitwa MOWLEM, kajaribu kuikumbuka kidogo na uangalie kazi zao.
Hawa ndio walijenga Port Access Avenue, bila shaka na Pugu road. Back to the topic, yapo yaliyofanywa na mkoloni, lakini pia awamu ya kwanza ya utawala baada ya uhuru ilifanya mengi. Kama waliopokea kijiti wangeendeleza spirit ile, leo hii tungekuwa mbali kidogo ukizingitia kuwa sasa tunazo resources nyingi tofauti na miaka ile.
 
Kampuni ya kifaransa naona unzugumzia ile terminal mpya ambayo hata vyoo vayeke vinanuka, na huenda ni airport pekee ambayo maji huwekwa kwenye mapipa na ndoo, ambako escalator huwa haifanyi kazi kwa miezi sita. Kimsingi ni uwanja uleule hakuna kipya pale. Inafact kampuni ya Ufaransa haikujenga uwanja mpya, nakumbuka tulijadili sana bunge ufisad wa kununua madeni na kujenga ule uwanja.

So, inawezekana kuwa sina kumbukumbu vizuri kuhusu MECCO, kama kweli MECCO ilikuwa na uwezo wa kujenga barabara ile basi naona leo Tanzania tungekuwa na barabara nzuri sana. Na MECCO na fahamu ni kampuni iliyokuwa na engineers wengi kutoka Soviet union na wakatulazimisha kununua magari yao mengi ambayo sasa yanaoza tu. Mkuu sijui kama unakumbuka kampuni moja inaitwa MOWLEM, kajaribu kuikumbuka kidogo na uangalie kazi zao.

Ni kweli ni kampuni ya MOWLEM iliyojenga, samahani kwa kupoteza kumbukumbu - ni zamani sana; hata hivyo MECOO nayo ilifanya kazi nzuri pia katika ujenzi mbalimbali hapo Dar wakati wake. Baada ya hayo, ni dhahiri basi kuwa unakubaliana nami kwamba vitu hivyo havikuachwa na mkoloni. Tatizo ni kuwa ingawa miaka ya sabini tulijifanyia mambo yetu kulingana na hali ya wakati huo, kuanzia miaka ya themanini tukadumaa na kushindwa hata kuendeleza yale tuliyojitengezea wenyewe. Habari ya vyoo kuwa vichafu hapo leo na magari kuharibika sidhani kama inatosha kudiscredit juhudi tulizofanya wenyewe miaka ya sabini.
 
Heri Tz ya zama za ukoloni kuliko Tz ya zama hizi za sasa chini ya CCM
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom