Prof Kamuzora: Falsafa ya Elimu yetu ni kuwa watu wanasomea taifa na si kusomea maisha yao.

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,053
4,595
Prof Kamuzora RAS Kagera: Tatizo lile lile nililolisema awali. Falsafa ya Elimu yetu ni kuwa watu wanasomea taifa na si kusomea maisha yao. Hivyo, wote mnaingizwa kwenye behewa kuelekea kwenye combinations ambazo Taifa limechagua yaani PCM, PCB, PGM, CBG, CBN, ECA, EGM, HGL, HGE, HGK. Ukikosa nafasi kwenye behewa sasa ndio ukatafute hizo fursa zingine za NACTE na VETA.
Falsafa hii na mfumo huu una athari za kisaikolojia. Kwanza unafanywa watu wakikosa nafasi kwenye behewa la form five wajione kuwa ni watu waliofeli na waliopoteza ndoto za maisha. Pili, inafanya elimu ya NACTE na VETA kuonekana kama ni sitara na hifadhi kwa waliokosa nafasi behewani. Matokeo yake, tunapeleka huko kwenye NACTE na VETA waliopoteza matumaini. Yaani tumegeuza NACTE na VETA kuwa ni elimu mbadala na si chaguo tu kama kwenda form 5.
Katika hili nitapenda kutoa mfano wa jamii ya watanzania wenye asili ya asia. Hivi hawa wanaishiaga wapi? Mbona wengi hawaendi form 5 na hata wanaoenda hawasomi HGL, HGK na HGE bali utawakuta aidha kwenye PCB, PCM na ECA na EGM? Na je mbona huko chuo hawaonekani kwenye vitivo vya Sheria, Sayansi ya Siasa, Sociolojia na Historia na Archaeology? Mbona ni kama hawapo kabisa kwenye Masters degree zinazotolewa na Chuo Kikuu kipendwa cha UDSM na pia hawapatikani kule kwenye Masters za jioni za Mzumbe wala zile za Open University? Lakini mbona pamoja na kutowaona huko kote hatuwaoni mtaani wakipita na bahasha za khaki zenye photocopy za vyeti na barua za kuomba ajira?
Wenzetu hawa walishajinasua siku nyingi katika mtego wa fikra tuliouingia wa kusomeshea watoto kwenda kujaza nafasi za wanaostaafu na kufa katika sekta ya umma. Wenzetu wanajifunza stadi zaidi. Anayetaka uhasibu, akifika form four anajisajili kwenye mitihani ya Bodi za Uhasibu (NBAA na ACCA) anaendelea huko. Wengine watakwenda kujifunza masuala ya kukatisha tiketi za ndege IATA system, wengine watakwenda kujifunza stadi za Hardware na Software Engineering na stadi nyingine nyingine. Wengine watasomea u-pilot, wengine insurances nk. Leo nenda kwenye nursery schools walimu wengi ni watanzania waasia kwa kuwa wanakwenda kusomea fani hiyo. Kwao behewa la form 5 ni moja tu kati ya mabehewa mengine na si behewa takatifu au la wateule.
Wenzangu na sisi tunakwenda na behewa, tunaingia chuo tunapigwa sumu ya DS 101 tunakuwa wanamapinduzi na wachukia mabeberu huku tukisoma archaeology, Sociology, Political Science na Kiswahili mwisho wa siku tunasubiri Sekretariati ya Ajira itangaze kazi tunajikuta inaajiri asilimia 10 tu ya waliomaliza chuo. Mwishowe hao hao wasomi wanarudi kuajriwa na mabepari waliokuwa wanawachukia wakiwa chuo🤣🤣🤣🤣🤣.
Kuna kitu tunakosea mahala😎.
*COPY & PASTE *
 
Prof Kamuzora RAS Kagera: Tatizo lile lile nililolisema awali. Falsafa ya Elimu yetu ni kuwa watu wanasomea taifa na si kusomea maisha yao. Hivyo, wote mnaingizwa kwenye behewa kuelekea kwenye combinations ambazo Taifa limechagua yaani PCM, PCB, PGM, CBG, CBN, ECA, EGM, HGL, HGE, HGK. Ukikosa nafasi kwenye behewa sasa ndio ukatafute hizo fursa zingine za NACTE na VETA.
Falsafa hii na mfumo huu una athari za kisaikolojia. Kwanza unafanywa watu wakikosa nafasi kwenye behewa la form five wajione kuwa ni watu waliofeli na waliopoteza ndoto za maisha. Pili, inafanya elimu ya NACTE na VETA kuonekana kama ni sitara na hifadhi kwa waliokosa nafasi behewani. Matokeo yake, tunapeleka huko kwenye NACTE na VETA waliopoteza matumaini. Yaani tumegeuza NACTE na VETA kuwa ni elimu mbadala na si chaguo tu kama kwenda form 5.
Katika hili nitapenda kutoa mfano wa jamii ya watanzania wenye asili ya asia. Hivi hawa wanaishiaga wapi? Mbona wengi hawaendi form 5 na hata wanaoenda hawasomi HGL, HGK na HGE bali utawakuta aidha kwenye PCB, PCM na ECA na EGM? Na je mbona huko chuo hawaonekani kwenye vitivo vya Sheria, Sayansi ya Siasa, Sociolojia na Historia na Archaeology? Mbona ni kama hawapo kabisa kwenye Masters degree zinazotolewa na Chuo Kikuu kipendwa cha UDSM na pia hawapatikani kule kwenye Masters za jioni za Mzumbe wala zile za Open University? Lakini mbona pamoja na kutowaona huko kote hatuwaoni mtaani wakipita na bahasha za khaki zenye photocopy za vyeti na barua za kuomba ajira?
Wenzetu hawa walishajinasua siku nyingi katika mtego wa fikra tuliouingia wa kusomeshea watoto kwenda kujaza nafasi za wanaostaafu na kufa katika sekta ya umma. Wenzetu wanajifunza stadi zaidi. Anayetaka uhasibu, akifika form four anajisajili kwenye mitihani ya Bodi za Uhasibu (NBAA na ACCA) anaendelea huko. Wengine watakwenda kujifunza masuala ya kukatisha tiketi za ndege IATA system, wengine watakwenda kujifunza stadi za Hardware na Software Engineering na stadi nyingine nyingine. Wengine watasomea u-pilot, wengine insurances nk. Leo nenda kwenye nursery schools walimu wengi ni watanzania waasia kwa kuwa wanakwenda kusomea fani hiyo. Kwao behewa la form 5 ni moja tu kati ya mabehewa mengine na si behewa takatifu au la wateule.
Wenzangu na sisi tunakwenda na behewa, tunaingia chuo tunapigwa sumu ya DS 101 tunakuwa wanamapinduzi na wachukia mabeberu huku tukisoma archaeology, Sociology, Political Science na Kiswahili mwisho wa siku tunasubiri Sekretariati ya Ajira itangaze kazi tunajikuta inaajiri asilimia 10 tu ya waliomaliza chuo. Mwishowe hao hao wasomi wanarudi kuajriwa na mabepari waliokuwa wanawachukia wakiwa chuo.
Kuna kitu tunakosea mahala.
*COPY & PASTE *
Tufanye nini sasa na umechukuwa quote ya profesa amesaidiaje kurekebisha mazoea hayo?
 
We get education in the class, we get knowledge in the field work.
Watanzania bado tumepumbaa kwa kuamini kuwa ukipata elimu kubwa basi umemaliza kazi na baada ya hapo ni kutumbua maisha na kutamba mbele ya watu na kusema " Mimi nimesoma bwana".
Mambo mengi yanaharibika maofisini kwa sababu tunaongozwa na watu ambao wana elimu kubwa lakini hawana ujuzi (knowledge) wa mambo waliyosomea na wengine wanajiingiza kwenye mambo ambayo hakusomea kabisa kwa sababu tu kuwa sehemu hizo kuna pesa.
Hii inasababisha hata wanataalumu wa fani zingine kukimbilia kwenye taaluma ya Siasa au Uongozi ambayo hawakuisomea kabisa na huenda shuleni walikuwa wanaidharau kuwa ni elimu ya vilaza.
Wanafanya hivyo kwa sababu, wao ndiyo walikuwa na akili nyingi Shuleni, lakini katika kuajiriwa wamekuta wanatawaliwa na wale ambao walikuwa vilaza shuleni na pengine vilaza hawa wanakuwa na maslahi mazuri kuliko wao.
Wasomi wengi wa Inchi hii hawasomi kwa maslahi ya Taifa kwanza bali wanasoma kwa maslahi binafsi bila kujali Taifa litapata hasara kiasi gani kwa wao kunufaika.
Muda wa kusoma Form five na Six ni matumizi mabaya ya raslimali. " poor resource management" kwa sababu katika miaka miwili ambayo mwanafunzi anakaa shuleni kama mwanafunzi wa Sekondari angekuwa chuoni kwa kusomea ujuzi Fulani katika ngazi ya Diploma na miaka miwili mingine angekuwa anasomea digrii.
Huyu anayemaliza Diploma tayari anaweza kuajiriwa au kujiajiri na kuanza kuzalisha mali.
Kenya wanafanya hivi na ndiyo maana wanasonga mbele haraka kuliko sisi.
 
Yeye mbona amesoma hakutaka kwenda kwenye behewa la pili au wanae anaweza waruhusu kwenda behewa la pili?
 
Mhh kweli bhuaana . TufanyeJe sasa, wakati tumetanguliza siasa ktk kila jambo ?!
 
Yeye mbona amesoma hakutaka kwenda kwenye behewa la pili au wanae anaweza waruhusu kwenda behewa la pili?
yeye kakuonyesha wewe njia,ni juu yako sasa,kuifuata ama kukalia kuhoji njia aliyoutumia yeye kufika mahali alipo!!!. Kwanza ujue miaka yao ukiwa unaelekea kumaliza kidato cha sits tayari taasisi mbalimbali zinakuja mashuleni kutafuta watu wa kuajiri unaanza kuchagua ajira bado hata hujahitimu form6!!!. Ukikalia kumhoji process hivyo utajikuta unaridhika na division 0 kwa sababu mwalimu wako alipata div4
 
Back
Top Bottom