Prof. Kabudi: Watanzania tuache uoga, hakuna atakayeshitakiwa na ACACIA

Wewe uwezo wako kifikra uko chini sana!

Mada zingine angalau uwe unakuwa msomaji tu lakini kwa sababu hujui kama uwezo wako ni kiduchu ndio maana unaandika vikomenti vyako vya kitoto kitoto kwenye mada hata ambazo zinahitaji tafakuri pana la watu wenye upeo mpana.

Ujinga ni mzigo katika jamii yenye uelewa mkubwa!

Ninashangaa kuona hata mazingira yameshindwa kukuelimisha!
Upo sawa mno kuna watu wanatoa comment kwa mihemko pasipo kufikirisha angalau kiasi kidogo kwenye ubongo
 
acacia akashitaki nini wakati the new law does not apply kwa mikataba ya zamani?
 
Hahahah!

Mkuu hiyo ni sentesi mpya yenye msamiati mgumu katika siasa za Tanzania.

Kama mtanzania anayeishi Tanzania anashikwa na mkewe live akiwa na mchepuko halafu anakataa hata kuomba msamaha, unategemea wanasiasa wataweza kuomba msamaha!

CCM hawawezi kuomba msamaha kwa sababu watanzania wengi hawajui maana ya kuombwa msamaha.

Nalielewa sana hilo.

Nilikuwa tu nampa rejea huyo jamaa lakini kumbe jamaa mwenyewe hata kusoma na kuelewa alichokisoma ni mgogoro.

Ananiambia kuwa eti uzi ni wa 2006. Yaani miaka 11 ilopita.

Wakati uzi ni wa mwaka jana tu.

Na huyo jamaa ndo sampuli ya watu tunaobishana nao humu [wasio hata na attention to detail].

Ni shida.
 
PART I
PRELIMINARY PROVISIONS
Short title and
commencement
1.-(1) This Act may be cited as the Natural
Wealth and Resources Contracts (Review and Re-
negotiation of Unconscionable Terms) Act, 2017.
(2) The Act shall come into operation on such
date as the Minister may, by notice published in the Gazette, appoint.
 
Dah!

Uzi ni wa 2006?

Kumbe mtu mwenyewe hata kusoma vizuri na kuelewa ulichokisoma ni shida!

Kumbe ndo maana!

Jumapili njema:D.

Bwaaaahaaaaaa bwaaahaaaaaa, bonge la aibu imekupata. We chapa mwendo huna jipya, na kuanzia sasa hicho kuherehere kitakuisha.
 
Huyu Professor nae anatetea kaugali kake tu. Nani kamwambia tunaogopa kushtakiwa? Tunachomwambia watumie akili kwa kubadilisha sheria kwanza kabla ya kuparamia Makinikia ambayo kisheria ni mali ya mwekezaji. Hizo akili zingegundua hilo tungeshukuru.
Hivyo viswanglish vyake vya nn wakati tunasisitiza Kiswahili kitumike zaidi?
 
PART I
PRELIMINARY PROVISIONS
Short title and
commencement
1.-(1) This Act may be cited as the Natural
Wealth and Resources Contracts (Review and Re-
negotiation of Unconscionable Terms) Act, 2017.
(2) The Act shall come into operation on such
date as the Minister may, by notice published in the Gazette, appoint.
Kwa hiyo hapa unataka kusema nini?

Nisaidie mimi ambaye sijui kiingereza!
 
Wameshatunyonya sana acha mikataba yote irudiwe upya. Na siyo ya madini tu nahisi kwenye gasi ndo kumejaa uozo. Mikataba yote irudishwe bungeni.

Ila wabunge haswa wa CCM hata siwaelewi, ni kama bendera fuata upepo tu. Wao walikaa na kupitisha miswada yote ya madini kwa kura ya ndiyo. Wapinzani walipowapinga wakabakia kuzomea. Sasa hivi walichokuwa wanahoji wapinzani ndo kinawatokea puani.

Tukiacha mihemko na uchama tukaweka nchi yetu mbele nina uhakika kabisa Taifa letu litasonga mbele. Ila kama sheria zitapitishwa tu kwa sababu tunataka ushabiki wa chama chetu ushinde tutatambukia shimoni.

Nakubaliana kabisa Prof Palamagamba alichosema ni vyema tukaenda mbele kwa ujasiri mkubwa na kuangalia upya mikataba iliyowekwa ya madini na kutengeneza mikataba mipya kuliko kuweka mkia katikati ya mapaja.

Liwalo na liwe tu. Ama zao ama zetu. Hata tukiliwa basi tujuwe pia tumejaribu kurudi kwenye mstari ikashindikana na siyo kubakia kulia lia tu.
bunge la sasa sioni umuhimu wake tena hasa hasa kwa uyu job ndugai kupitia wabunge wake wa ccm!!sioni tena check&balance maana limekuwa msemaji wa serikali badala ya kuwa kuisimamia serikali!!yani juzi nimeshuhudia mbunge mmoja ambaye sio waziri wala nini anadiriki mpk kusema sisi kama serikali!!!yni kashindwa kujitambua kabisa yy ni nani!!cthani kama hata hii miswada itaenda kutendewa haki uko bungenu kwa hii trend iliyopo sasa!!nchi imekuwa na utawala wa absolute monarchy.,mtu mmoja anakuwa kama mungu mtu!!thanks to judiciary kidogo linajitambua
 
Nalielewa sana hilo.

Nilikuwa tu nampa rejea huyo jamaa lakini kumbe jamaa mwenyewe hata kusoma na kuelewa alichokisoma ni mgogoro.

Ananiambia kuwa eti uzi ni wa 2006. Yaani miaka 11 ilopita.

Wakati uzi ni wa mwaka jana tu.

Na huyo jamaa ndo sampuli ya watu tunaobishana nao humu [wasio hata na attention to detail].

Ni shida.
Nenda nao tu polepole, hii ndiyo Tanzania yenye watu wanadhani wanajua wakati hawajui.

Unakuta mjinga fulani anasema Prof, Kabudi hajui sheria wakati huyo anayesema, hata ukimuuliza nini maana ya sheria hawezi kukupa jibu sahihi.

Hii nchi ina matatizo zaidi ya tudhaniavyo!
 
Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi wakati akiwasilisha hoja na kujibu maswali mbali mbali kwenye Kamati nne za kudumu za bunge kuhusu miswada mitatu inayohusu raslimali za Taifa.

Prof. Kabudi amesema Serikali sio naive na inafahamu dunia ilivyo kuhusu economic order. Tunajua we are fighting giants but we cannot be afraid of giants. Tunatumia akili nyingi, hekima na busara katika vita hii.

Aliendelea kusema, ‘’We know there will be an attempt to sabotage, definitely na kama tuki-succumb kwamba we are fight a giant busi tukae, tutakuwa hatulitendei haki Taifa’’.

‘’This country has survived sabotage, miaka mingi tu, na sisi lazima tujaribu kuliko kukaa chini na ku-succumb’’ alisema.

Aliendelea kusema‘’Hatuwezi kuwa na wawekezaji ambao hatufaidiki nao nani bora madini tuyaache badala ya kuyachimba ili tusubiri hao kizazi kijacho watakaokuwa na busara na akili kwa sababu sisi tumeshindwa. Madini huwa hayaozi’’

‘’Sheria hii tutakayotunga haiwafukuzi bali inawakaribisha kwa mazungumzo, waje tuongee, tutaelewana na uzuri mambo tunayoyadai yamo ndani ya sheria za kimataifa, hatuyazui wenyewe. Mikataba ya sasa itaangaliwa, tutajadiliana nao. Hatufukuzi mtu na hawawezi kufunga migodi kwa sababu tunafahamu wanapata faida’’.

‘’Yes, we fighting giant, biashara ya dhahabu inafahamika nani ana control lakini huyo giant unapomfikisha anarusha ndege kuja nchini kujadiliana, hayo ni mafanikio’’

‘’Kama Botswana yenye wananchi milioni 2 inaweza ku-flex its muscles kwenye maliasili zake, sisi Watanzania ambao ni 50 millions, we are lame ducks and toothless bulldog. It's incredible’’.

‘’Tusisahau kuwa nchi hii ime survive kwa vitisho vikubwa kuliko leo. Mwaka 1964, Mwalimu angetetereka kwa Wajerumani waliokuwa wanatupa hela nyingi, akawasikiliza, Tanzania isingekuwepo kama Jamhuri ya Muungano. Kwa msimamo wa Mwalimu, tulipoteza Deutsche Mark milioni 35 lakini Mwalimu akawaambia pack and go’’.

‘’Mwaka uliofuata, 1965 kulitokea Unilateral Declaration of Independence (UDI) in Rhodesia ambapo nchi zote za Afrika zilikubaliana lazima Uingereza imuondoe Prime Minister, Ian Smith ama sivyo nchi zote zitavunja uhusiano wa kibalozi na Uingereza. Baada ya Uingereza kukataa, nchi mbili za Tanzania na Ghana ndizo zilivunja uhusiano wa kibalozi ambapo gharama yake ilisababisha Rais wa Ghana kupinduliwa huku Tanzania tukikosa msaada wa pound milioni 5’’.

‘’Malengo ya mifano yangu sio kwamba turudie hayo bali kuonyesha kuwa Taifa hili limepita vipindi vigumu kwa sababu lilikuwa na uongozi unaothubutu na kusimamia maslahi ya watu ili liweze kuvuka. Hiki ni kipindi kingine cha kuvuka’’.

‘’Tusiogope na kuanza kuulizana kuwa tutaweza au hatutaweza? Wawekezaji watatishia kuwa wataondoka lakini ninasema hawataondoka’’.

Prof. Kabudi amesema watu wa ACACIA kinachowasumbua siyo sheria bali ni integrity yao kwa sababu kampuni inayovunja integrity pledge hupelekea kushitakiwa kwa kosa la fraud. kampuni inayofanya fraud na ikadhibitika kisheria, mali zake hutaifishwa. Hiki kinafanyika hata kwenye nchi zao za Ulaya na Marekani’’.

Alisema, ‘’Ukiona ACACIA wanavyohangaika ambapo mara ya kwanza waliomba kuonana na Rais ambaye maombi yao aliyakataa. Wakaomba tena mara ya pili na kukubaliwa kupitia Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambaye ni mmiliki mkubwa wa hisa 63.9 wa Kampuni ya Acacia Mining, Profesa John Thorton’’.

‘’Kwao integrity ni muhimu sana kutokana na heshima ya kampuni ambayo wajumbe wa bodi ni viongozi wastaafu wenye heshima kubwa duniani’’.

Alimaliza kwa kusema, Watanzania tunatakiwa tujiamini kwa sababu nchi yetu ime train watu wengi katika fani mbali mbali pamoja na fani ya madini lakini tatizo lililopo ni kutowathamini, kuwadharau na kutowatambua. Hatukuwatumia na wameondoka kwenda kusaidia nchi nyingine. Kwa mfano, Nchi ya jirani tunayoisifu kuwa miji yake imepangwa vizuri, wataalam waliochora ramani ya miji hiyo wametoka Tanzania. Director of finance wa Air Tanzania ndio alikuwa Director of finance wa Air Rwanda. Ndiye ameiwezesha Air Rwanda kufika hapo ilipo. Key staff wa Air Rwanda ni Watanzania ambao baadhi yao wamekubali kurudi. Tatizo letu watanzania tunajidharau wenyewe wakati uwezo tunao’’.

Kwa maelezo zaidi angalia video.

Aliendelea kusema‘’Hatuwezi kuwa na wawekezaji ambao hatufaidiki nao nani bora madini tuyaache badala ya kuyachimba ili tusubiri hao kizazi kijacho watakaokuwa na busara na akili kwa sababu sisi tumeshindwa. Madini huwa hayaozi

=======
Hapa ni kama ametukana wale wote waliotukifisha hapa katika suala la madini.
Kimsingi Proff amewatukana Ma SISIEM wote kwa ujumla waliokuwepo chamani na Serikalini tokea tunaingia hiyo Mikataba
 
Ninakubaliana na wewe.

Matatizo haya yametokea ndani ya utawala wa CCM nani lazima wabebe lawama.

Kazi ya CCM kwa sasa ni kujirekebisha baada ya kupewa nafasi ya kuongoza tena taifa.

Kuna baadhi ya watanzania wanasema lazima CCM iombe msamaha kwa kuruhusu hali hii itokee. Nadhani madai yao ni halali lakini ikumbukwe kuwa neno SAMAHANI ni geni katika jamii ya Tanzania achilia mbali siasa za Tanzania. Sioni CCM wakiomba msamaha!
Nmesoma thread na comments zake Ila nmefika hapa ikanibidi kuandika. Hii ndiyo Tanzania tuitakayo, watanzania wasimamia ukweli bila kujali vyama. Wengi wetu tunashabikia hadi uozo kisa tu umetoka kweny chama chetu. Wewe ni Mzalendo, Hakika big up
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom