Prof. Kabudi tusaidie kumng'amua aliyeuza eneo la Kanisa Anglican kule Buza na kumfanya DC Gondwe kuchachamaa sana!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,736
2,000
Najua nafasi katika Kanisa Anglican jimbo la Tanzania na hususani Dayosisi ya Dar es Salaam ndio maana nakuomba sana mh Prof Kabudi utusaidie kumng'amua aliyeuza kiwanja cha Kanisa kule Buza ili kijengwe kituo cha daladala.

DC Gondwe ambaye pia ni mwana St Alban japo yeye ni Mlutheri wa Mbezi Beach amefichua uozo huu na kutufumbua macho sasa ni jukumu lenu wazee wa dayosisi tena mlio wakongwe Prof Kabudi na kapteni Mkuchika mkatutatulia kitendawili hiki cha serikali kununua kiwanja cha Kanisa kinyemela.

Mungu wa mbinguni awatie moyo muweze kusimamia kweli.

Maendeleo hayana vyama!
 
residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
3,661
2,000
Kabudi kiboko yake ni tha late prof D. Mwaga. Alikuwa analeta za kuleta CPT/KJT/KAT enzi hizo za kuanzishwa St. John's University,akataka prof Meshack asiwe DVC.

Huyo ana mikono yake,miguu,na kiwiliwili chote katika kuchangia migogoro ya DCT - Dr. M. Mhogolo, Dayosisi ya DSM - V. Mokiwa. Hana uhalali wala kushughulikia jambo lolote la Anglican Church of Tanzania.
 
Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
27,431
2,000
Mleta Mada Nadhani Wewe Ni Mgeni Sana

DC Hajafichua Lolote Kuhusu Hilo Eneo

Hapo Buza, Buguruni Shell, Buguruni Malapa Hayo Ni Maeneo Ya Kanisa Anglican

Huko Buza Eneo Limeuzwa Kwa Hira, Thread Imo Humu Iliyojadili Kwa Kina, Unajua Kilichomtoa Archbishop Mokiwa Ni Hayo Maeneo

Ulitokea Mpasuko Mkubwa
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
14,797

Mmmmh haya makanisa sasa bora mwenye nayo arudi ayachukue maana yamejaa wahuni na magenge ya wezi kwa kivuli cha biblia
 
Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
27,431
2,000
Mmmmh haya makanisa sasa bora mwenye nayo arudi ayachukue maana yamejaa wahuni na magenge ya wezi kwa kivuli cha biblia
Nani Ya Kanisa Shida
Thread Za Hii Issue Zipo Humu Ila Zimefungwa Huwezi Kuchangia Tena!!
 
Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
27,431
2,000
Mnakumbuka Kauli Ya
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Kwa Kanisa Catholic, Alipokufa Yule Sister
Kwa Kujinyonga, Alisema Endeleeni Kuniombea Nina Siri Zenu Nyingi Sana
Ili Niziseme Maana Yake Ni Bhalaa
 
wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
19,496
2,000
Najua nafasi katika Kanisa Anglican jimbo la Tanzania na hususani Dayosisi ya Dar es Salaam ndio maana nakuomba sana mh Prof Kabudi utusaidie kumng'amua aliyeuza kiwanja cha Kanisa kule Buza ili kijengwe kituo cha daladala.

DC Gondwe ambaye pia ni mwana St Alban japo yeye ni Mlutheri wa Mbezi Beach amefichua uozo huu na kutufumbua macho sasa ni jukumu lenu wazee wa dayosisi tena mlio wakongwe Prof Kabudi na kapteni Mkuchika mkatutatulia kitendawili hiki cha serikali kununua kiwanja cha Kanisa kinyemela.

Mungu wa mbinguni awatie moyo muweze kusimamia kweli.

Maendeleo hayana vyama!
Vumilieni apone kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,703
2,000
Mleta Mada Nadhani Wewe Ni Mgeni Sana

DC Hajafichua Lolote Kuhusu Hilo Eneo

Hapo Buza, Buguruni Shell, Buguruni Malapa Hayo Ni Maeneo Ya Kanisa Anglican

Huko Buza Eneo Limeuzwa Kwa Hira, Thread Imo Humu Iliyojadili Kwa Kina, Unajua Kilichomtoa Archbishop Mokiwa Ni Hayo Maeneo

Ulitokea Mpasuko Mkubwa

Buza eneo halijauzwa.. bali wameingia mkataba na tajiri kishimba mbunge wa kahama... amejenga appartments nyingiiiii... ambazo kodi anazolipwa kuna asilimia inaenda kanisani Anglican
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,736
2,000
Buza eneo halijauzwa.. bali wameingia mkataba na tajiri kishimba mbunge wa kahama... amejenga appartments nyingiiiii... ambazo kodi anazolipwa kuna asilimia inaenda kanisani Anglican
Kuna eneo Gondwe amesema panataka kujengwa stendi ya daladala, unapajua hapo bwashee?!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom