Prof Kabudi: Mikataba yote ya zamani ya Maliasili itapitiwa upya

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Kabudi Palamagamba amesema kwa mujibu wa sheria mpya, mikataba yote ya zamani ya maliasili itapitiwa upya.

Ameyasema hayo leo akiwa mkoani Dodoma.
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Kabudi Palamagamba amesema kwa mujibu wa sheria mpya, mikataba yote ya zamani ya maliasili itapitiwa upya.

Ameyasema hayo leo akiwa mkoani Dodoma.
Nani ataipitia? Si mlisema mtaipeleka bungeni ijadiliwe mbona mnageuka?
 
Wapitie tu mpaka miaka 99 iishe loliondo sijui kama tutakuwepo.
 
mdogo mdogo tutafika tu..
wale wanaoleta fake news wataumbuka tu...ikiwezekana mods tuwapige na ban.
 
Kupitiwa upya haina maana kuwa sheria itaanzia nyuma. Ni kwamba mikataba itapitiwa yote ila sheria mpya zitaanza kutumika kwa makampuni mapya na si ya zamani yanayoendelea kutuibia.
 
Nani ataipitia? Si mlisema mtaipeleka bungeni ijadiliwe mbona mnageuka?
wewe vipi, Bunge ni mamlaka ya udhibiti, hakuna technical expertise ya kuandika mikataba huko. Sheria inatoa mamlaka kwa Bunge kufanya review kwa namna ambavyo litaona inafaa siyo kuandika. Parties kwenye mikataba inayotarajiwa kupitiwa upya (reviewed) ni serikali (executive) na makampuni ya madini au mengineyo. Achaneni kuwa na wicked thinking.
 
mdogo mdogo tutafika tu..
wale wanaoleta fake news wataumbuka tu...ikiwezekana mods tuwapige na ban.

Ruksa kupiga kelele. ------------ Ndiyooooo.
Marufuku kupiga kelele ------------Ndiyooooo.
 
Kuipitia ndiyo nini? Sheria hii haiwezi kuapply dhidi ya hiyo mikataba it is a principle in law to maintain predictability mtaniambia
 
Back
Top Bottom