Prof. Kabudi, kwani ni nani kakutuma ujibu hoja za EU? Mbona kama umeliamsha

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
4,564
2,000
Mhe. Prof. Kabudi, samahani I wish to know yale majibu umewapa EU umetoa kwa niaba ya kikao cha Baraza la Mawaziri mlichokaa na Rais akiwa mwenyekiti au umetoa kama Wizara au ni maneno yako binafsi.

It seems maneno yako yataibuwa mtifuwano wakidiplomasia nakuleta shinikizo uondolewe na usipo guswa itadhihirika Baba ndio alie kutuma jambo litazuwa jambo sio zuri ndani ya Serikali.

End
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,612
2,000
Mbona kama mmechanganyikiwa mnapokezana kuanzisha mada maudhui ni yale yale tu, aliyeambiwa ni Muzungu kuumia na povu mnatoka ni ninyi, kulikoni?
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,447
2,000
Kweli amewakosea wakubwa wa Dunia adabu
Hatari na nusu. Amechanganyikiwa huyu waziri tokea alivyoambiwa hatopewa nafasi ya kugombea urais.

Kisa kwanini wamemhoji mwenyekiti wao wa bunge kwa "KIGEZO KIPI KILITUMIKA TANZANIA KUPEWA MSAADA WA € MILLIONI 27 ZA KUPAMBANA NA COVID-19" wakati Tanzania imesema haina Covid.

Na hizo hela zimetumika vipi.
 

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
1,527
2,000
Ukawa ilishaisha ilikuwa programu ya muda tu

Jibu hoja mkuu USSR, mbona hoja iko wazi unakwama wapi!?

Ndiyo maana nasema mataga hoja ikiwazidi uwezo mnakuja na matusi.
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,447
2,000
Wanatafuta la jambo baya kwa gharama sijuwi ni kwa nini !
Katumia lugha ambazo sio za kistaarabu na za kugandamiza demokrasia
"Nasema hizo hela watazitapika, zitawatokea kupitia tundu lolote" kauli pendwa na mheshimiwa.

Sasa itatumika dhidi ya serikali ya tanzania.
 

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
1,982
2,000
Umeandika ujinga mtupu ila kwakuwa mods ni wanaukawa wataliacha hili
Ujinga ni nini hapo? Kwani kamati za bunge la ndungai zikikaa huwa kuna waziri anazijibu nje ya bunge na kwa majibu ya kikolofi kama alivyofanya Kabudi, kwanini kabudi anataka kuwaaminisha watu kuwa nchi yetu imetwezwa jambo ambalo sio kweli, EU imewataka kujibu? Jibu ni hapana ni kiherehere chao.

Sisi kwenye EU ni third part country sisi sio wanachama wa EU,hatuna hicho kibesi cha kuikoromea EU kwa staili hiyo, hajaulizwa anajibu je akiulizwa?
 

inchaji

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
1,552
2,000
Kibao kikigeuka watamruka watasema yale maneno ya kwake katoka nayo jalalani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom