Prof Kabudi: Kiswahili kinapotoshwa, neno Fisadi maana yake ni mtu anayetongoza wake za watu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,747
139,529
Waziri wa mambo ya nje amesema kuna wakati kiswahili kimekuwa kikitumika ndivyo sivyo lakini wasomi na waandishi wa habari wamekaa kimya.

Kwa mfano maneno Kuchakachua na Fisadi yamekuwa yakitumika isivyo stahili. Kuchakachua maana yake ni kuchanganya kimiminika kisicho na ubora na kile chenye ubora ili kuongeza thamani.

Na fisadi ni mwanamme anayetongoza wake za watu, amemalizia Prof Kabudi.

Source Ayo tv!
 
Oyaaaaaaa
Kumbe ndio maana yake pia duh!!!!

Naona ni kumaanisha kwamba fisadi ni anayefuja mali ya mwanaume mwingine.. ambaye ni mkewe eeeeh

Fisadi pia ni anayefuja mali za serikali, mtu kwa sababu ni vyao sio vyake fisadi.. vinamilikiwa.. patamu hapo eeeh
 
Sasa anayetumia sana neno fisadi hadi akawaanzishia mahakama ni nani?

Sisi wengine tunaelewa vizuri tu maana ya Fisadi na tuliwahi kulijadili kipindi kile cha Yusuf Makamba alipokuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Tunaelewa pia kuwa hata neno Afande maana yake ni basha au m.fira.ji
 
Lakini profesa Kabudi sio mtaalamu wa kiswahili! Ifike mahali kila mmoja amheshimu mwenzake kwenye suala zima la professional..
Halafu hii nchi mbona ina matatizo mengi sana ya kuzungumzia mbali na hilo?
 
mwandishi wa habari yeye, nguli wa sheria yeye, mtaalamu wa kiswahili yeye.
kabudi wewe ni kiongozi mwandamizi serikalini na sio mhadhiri wa chuo, acha tabia ya ku 'behave' kama uko darani na watu wote ni wanafunzi wako, huku duniani kuna watu vichwa zaidi yako na wanakuchora tu unavyotema matango pori . Focus kwenye kazi yako mzee.
 
Mgogo na Kiswahili wapi na wapi?

Asili ya neno Fisadi ni neno la kiarabu yenye maana ya Haribifu

Hata kwny Qur an neno fisadi linatamkwa kama neno lenye kuashiria uharibifu katika Ardhi

Tatizo la huyu mipovu ni kuamini anajua kila kitu
Zamani nilikuwa naamini mtu akiwa Prof. alikuwa anajua kila kitu.
 
Mgogo na Kiswahili wapi na wapi?

Asili ya neno Fisadi ni neno la kiarabu yenye maana ya Haribifu

Hata kwny Qur an neno fisadi linatamkwa kama neno lenye kuashiria uharibifu katika Ardhi

Tatizo la huyu mipovu ni kuamini anajua kila kitu
Hahahaa....... Kwani kutongoza wake za watu siyo uharibifu?!
 
mwandishi wa habari yeye, nguli wa sheria yeye, mtaalamu wa kiswahili yeye.
kabudi wewe ni kiongozi mwandamizi serikalini na sio mhadhiri wa chuo, acha tabia ya ku 'behave' kama uko darani na watu wote ni wanafunzi wako, huku duniani kuna watu vichwa zaidi yako na wanakuchora tu unavyotema matango pori . Focus kwenye kazi yako mzee.
We muache tu ajishauwe
 
mbona kama anamsema yul aliyewaita wao ni wapumbuvu,maana anapenda sana kulitumia hili neno fiasdi
 
Upumbavu tuliombiwa anatukanwa kila siku ndio huu!!! Sasa kumtongoza mke wa mtu mwingne ina tofauti gani na kutumia au kumiliki mali za wizi au kufujaa mali za umma??.
 
Ufisadi/Fasada/المفسد ni uharibifu bila kujali wa aina gani,mzinifu ni fisadi maana anaeneza uharibifu katika jamii, mwizi ni fisadi maana anawadhuluma na anakula mali za watu kwa batili, kusengenya ni ufisadi maana maafa yaweza kutokea kwa sababu ya kusengenya, hivyo ufisadi ni kila aina ya uharibifu hukumu yake ni Ufisadi.

My take. Kabudi asitake kutupotosha wanataaluma wa lugha hii , nadhani anajishughulishe na sheria na siasa zake tu.
Fonolojia, fonetikia, semantikia, pragmatiki, foni, fonimu, alofoni, mofu, atuachie wenye navyo .
 
Prof Kabudi ni mtaalamu wa lugha ya kiswahili pia!
 
Sasa anayetumia sana neno fisadi hadi akawaanzishia mahakama ni nani?
Sisi wengune tunaelewa vizuri tu maana ya Fisadi na tuliwahi kulijadili kipindi kile cha Yusuf Makamba alipokuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
Tunaelewa pia kuwa hata neno Afande maana yake ni basha au m.fira.ji
Eeeh hili la Afande maana yake ni mfiraji sijawahi kujua duh
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom