Prof Kabudi: Kati ya pesa na heshima ya nchi yetu, tutasimamia heshima. Tuko tayari kuwasikiliza na kujadiliana kwa heshima

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,823
2,000
Prof Kabudi ambaye ni waziri wa mambo ya nje amesema Tanzania haiwezi kuyumbishwa na vitisho vya kunyimwa misaada.

Kabudi amesisitiza kuwa Tanzania ni nchi huru inayoheshimu utu wa mtu na kamwe haitayumbishwa na nchi yoyote kwa vitisho vya kukatiwa misaada.

Kuhusu uchaguzi Prof Kabudi amesema ulikuwa huru na wa haki na dunia nzima imeshangaa maana hatukutumia posta kama wale wengine lakini uchaguzi wetu umefanyika kwa amani kabisa.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
=========

Prof. Kabudi: Nayasema haya kwa sababu kizazi cha sasa wanadhani hii nchi ndogo, sisi ndio nchi pekee hatujawahi kushindwa vita, hakuna mahali majeshi yetu yalipokwenda yakashindwa vita. Si Zimbabwe, Msumbiji, Comoro, Seychelles, si Uganda na hivi karibuni sio DRC Congo.

Nawahamasisha pia na vyombo vyetu vya habari tujue nini cha kuiambia dunia na watanzania, uchaguzi huu katika bara la Afrika umekuwa tulivu, wa amani.

There is nobody in the world has ever conducted a perfect election, give me one country! There is no country in the world which has conducted a perfect election. Perfect election is only conducted in heaven.

Mataifa yote yanafanya uchaguzi ambao ni huru, haki na wawazi na sisi wa utulivu na amani. Lazima tuiambie dunia hivyo na Taifa hili, nimesema na narudia, halijawahi kupigishwa magoti.

Na si jambo la kukumbusha kila wakati, sipendi, haina maana tunataka kufanya hivyo. Tulivunja uhusiano wa kibalozi na Uingereza mwaka 65 mpaka 72 na Mwalimu hakuvunja tu balozi na Uingereza, aliwarudishia msaada wao wote wa paundi milioni 5 na wakati ule zilikuwa nyingi, aliwarudishia.

Sisi leo watu wakisema vikwazo tu, tunaanza tetemeka nini? Hivi mngekuwa wakati wa Mwalimu! Hivi Tanzania ya 65 ni Tanzania ya leo? Lakini aliona kati ya heshima ya Tanzania na kudhalilishwa, aliwaambia waingireza, tumeshindwa kuelewana katika haya, basi. Ingawa tulibaki kuwa wanachama wa commonwealth.

Wajerumani mwaka 64 walipoanza kumpa masharti mwalimu baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ujerumani mashariki iko Zanzibar, Ujerumani Maghiribi iko Tanzania bara, tukawaambia hapana, hamuwezi kuanza kunipa masharti. Suala la kufunga ubalozi wa Ujerumani Mashariki Zanzibar, si la kuamua mimi, tupeni muda.

Walipomletea kejeli alilihutubia Taifa, aliwafukuza wataalam wote wa kijerumani na aliwarudishia hela yao dochmark milioni 35, sisi leo watu wachache tu wakikaa kuzungumza, ooh tutafanya hivi! tayari watu kwenye mitandao.

Kati ya pesa na heshima ya nchi yetu, tutasimamia heshima ya nchi yetu. Kati ya misaada na utu wetu, tutasimamia utu wetu. Hatutakubali kutoheshimiwa na utu wetu kudharauliwa kwa sababu ya misaada na pesa lakini tutashirikiana na mataifa yote duniani ambayo, moja yatatuheshimu sisi ni Taifa huru na yanatuheshimu sisi ni binadamu tulio sawa na wanadamu wengine wote na tuko tayari kuwasikiliza na kujadiliana kwa heshima yale ambayo wanadhani yamepungua kwetu na yale ambayo tunadhani yamepungua kwao, tuko tayari. We are ready for constructive engagement with those that respect we are sovereign state but who also respect that we are equal and as humans we have our dignity on those matters of principal, we will not compromise.

However we are ready to work with all nations in the world who share our values, sovereignity, equality of nation, human dignity and respect of all human kind and we will never, never allow anyone to use aid or assistance to undermine our sovereignity, NEVER.

That did not happen during the time of Mwalimu, it will never happen now and this is why I distributed this booklet to all staff from mwalimu Nyerere.
 

time2ball

JF-Expert Member
Feb 4, 2014
299
500
Prof Kabudi ambaye ni waziri mteule wa mambo ya nje amesema Tanzania haiwezi kuyumbishwa na vitisho vya kunyimwa misaada.

Kabudi amesisitiza kuwa Tanzania ni nchi huru inayoheshimu utu wa mtu na kamwe haitayumbishwa na nchi yoyote kwa vitisho vya kukatiwa misaada.

Kuhusu uchaguzi Prof Kabudi amesema ulikuwa huru na wa haki na dunia nzima imeshangaa maana hatukutumia posta kama wale wengine lakini uchaguzi wetu umefanyika kwa amani kabisa.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Hata Zimbabwe walisema hivyo hivyo😊
 

Zenjiboe

Member
Aug 26, 2020
27
45
Prof Kabudi ambaye ni waziri mteule wa mambo ya nje amesema Tanzania haiwezi kuyumbishwa na vitisho vya kunyimwa misaada.

Kabudi amesisitiza kuwa Tanzania ni nchi huru inayoheshimu utu wa mtu na kamwe haitayumbishwa na nchi yoyote kwa vitisho vya kukatiwa misaada.

Kuhusu uchaguzi Prof Kabudi amesema ulikuwa huru na wa haki na dunia nzima imeshangaa maana hatukutumia posta kama wale wengine lakini uchaguzi wetu umefanyika kwa amani kabisa.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Sasa yatubidi tuwajengee wananchi political will ya kuvumilia tukiyakosa yale matunda yatokanayo na misaada badala ya kuandamana! Yaani kufunga mkanda
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom