Prof. Kabudi kama huwezi kujibu hoja, kaa kimya

EU wametoa hoja zao ambazo ni kukosekana demokrasia kwenye uchaguzi mkuu, polisi kuhujumu uchaguzi, na kupokea pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona. Hizi ndio hoja za EU ambazo kaka Msando amekwepa kuzijibu badala yake amemshambulia mtoa hoja (McAllister) na chama chake.

Lakini tujiulize je madai ya EU ni ya uongo? Je vyombo vya dola havikutumika kuvuruga uchaguzi? Je, watu hawakukamatwa? Je hakuna walioripotiwa kuuawa? Je hatukuchukua pesa za corona? Kwanza kuchukua pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona ni utapeli. Serikali imejipatia pesa kwa njia za udanganyifu. Hii ni jinai, na ni uhujumu uchumi.

Kwanini tunaacha kujadili hoja za EU tunawashambulia watoa hoja? Urafiki wa McAllister na Lissu haundoi ukweli kwamba tumetapeli hela za Corona. Wala urafiki wa Chadema na CDU hauondoi ukweli kwamba uchaguzi ulivurugwa na vyombo vya dola.

Hata kama McAllister angekuwa rafiki wa CCM bado hoja za kamati yake haziwezi kupuuzwa. Kaka Msando ni rafiki mkubwa wa kaka yangu mwingine Ally Bananga japo wanatofautiana vyama. Je, ikitokea Msando akafanya kosa huko CCM, halafu CCM wakamhukumu kwa sababu ya urafiki wake na Bananga ataridhika?

Tujadili hoja za EU na kuzitolea majibu bila kuwashambulia viongozi wake. Hoja za EU hata zingetolewa na mwanafunzi wa darasa la 3B kule Manda Ludewa, bado zingehitaji majibu. Tuhadili hoja, tusiwajadili watoa hoja.!

Msando Alberto aliandika kuhusu mjadala unaoendelea bunge la Ulaya kuhusu Tanzania kupokea pesa za Corona, pamoja na mapendekezo ya kamati ya mambo ya nje kutunyima msaada kwa sababu ya udanganyifu kwenye uchaguzi, wizi wa kura, watu kuuawa na wengine kutupwa jela. Wanahoji kama kuna haja ya kuendelea kuipa msaada nchi isiyoheshimu demokrasia.

Msando amedai tishio la EU kutunyima msaada ni kutokana na ushirika uliopo kati ya Chadema, CDU, Konrad Adenauer Stiftung na David McAllister.

Anadai kwa kuwa CHADEMA na chama cha CDU cha Ujerumani (anachotoka McAllister) ni wajumbe wa shirikisho la vyama vya kidemokrasia duniani (IDU), basi Chadema itakua imetumia nafasi hiyo "kuiharibia" Tanzania, hasa kwa kuwa McAllister ndiye Makamu Mwenyekiti wa IDU.

Ukivuliwa nguo chutama

Credit: G. Malisa

Kila mahali nchale! Wamebakia kukudoa macho mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango.
 
Tupo na fascist wa kwanza Tanzania tumpinge.
Duhhhh.....
Haya sasa, tulisema ulikua wa uwazi na haki na haya ndio matokeo yake tunavuna tulicho kipanda.

Haifai
Hii Ni Hatari
Vitendo Vya Hovyo Sana Hivi
Uchaguzi Umekwisha X 3

Waanze na wewe unaeshabikia shenzi kabisa.

Safi Sana, no, samahani

Acheni ujinga kusema mali ya wananchi imechomwa. Nimekagua mali zangu hakuna iliyochomwa. CCM wasijivike ngozi ya wananchi kuhalalisha ushenzi wao.

Waliiba uchaguzi ambao watu walichagua watu wao wanaowapenda, acha walipie upuuzi walioufanya.

Juhudi Zifanyike Haraka Sana Vinginevyo Mambo Haya Yataenea. Haikubaliki Hii

Ila huyo mbunge kanyooshwa kweli kweli hahahahahahah

Kwa kauli zake nadhani anamtafutia janga Rais na Watanzania wote kwa ujumla.

Kama kauli hiyo haijatokana na msimamo wa pamoja wa Serikali, ambao nilitarajia utoke baada ya kikao cha baraza la mawaziri, basi inahitaji kuchunguzwa kama kweli ina lengo zuri.

Tunahitani waziri anayeweza kumpunguzia Rais pressure kwa kujikita katika kauli za kidiplomasia.

Kuonesha wazi wazi tena kwa njia ya matusi kuwa hukufurahishwa na maoni ya wabunge wa bunge la EU, ni udhaifu.

Hata hivyo nina wasi wasi huenda hii ikawa hujuma iliyofanywa kisomi sana.

Hatujawahi kushindwa Vita yoyote, so kama wanajiandaa iwe kwa vita ya Vikwazo, vita ya kugaidi itakayopelekea majeshi yetu yawe sungusungu kwenye mpaka wetu na za Msumbiji poa tu, sisi tupo tayari. Hata hao Magaidi wa Msumbiji wakitaka kuvuka mpaka kuja kuteka Westgates zetu wajue tupo tayari.

Hatujawahi kushindwa

Ameambiwa asahau kuwa raisi, hata Kama ni maagizo soon atakanwa na kuchezea utumbuzi

Aloo naungana na wewe mtoa mada Kabudi alichofanya ni kwenda kuchokoza mambwa alafu yeye kawahi kupanda juu ya mti then yale mambwa yataanza kumkimbiza Jpm kwa sababu hajajiandaa.Alafu Kabudi kule juu ya mti anabaki anacheka the way jpm anavyosumbuka na yale mambwa chini.

Kiburi si uungwana! Kabudi anapaswa kujifunza kutokana na msemo huu.

Hii inaitwa "kupatwa kwa Tanzania"

nawe unashangaa wanavyomshangaa Kabudi.Swali la msingi Kabudi kajibu hoja?

Mshenzi mwenyewe!

Kabudi anahujumu utawala uliopo baada ya kuambiwa 'HATAIONA CANAAN'!
😅

👊 ✌️✌️✌️
 
Mwambie huyo Bwana yako Malisa uwezo wake wa kujua mambo ni mdogo sana! Sawa na kulinganisha Kichuguu (Malisa) na Mlima Kilimanjaro (Prof. Kabudi)
Sasa hapo umejibu hoja? Ushabiki unawafanya muonekane wapumbavu
 
EU wametoa hoja zao ambazo ni kukosekana demokrasia kwenye uchaguzi mkuu, polisi kuhujumu uchaguzi, na kupokea pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona. Hizi ndio hoja za EU ambazo kaka Msando amekwepa kuzijibu badala yake amemshambulia mtoa hoja (McAllister) na chama chake.

Lakini tujiulize je madai ya EU ni ya uongo? Je vyombo vya dola havikutumika kuvuruga uchaguzi? Je, watu hawakukamatwa? Je hakuna walioripotiwa kuuawa? Je hatukuchukua pesa za corona? Kwanza kuchukua pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona ni utapeli. Serikali imejipatia pesa kwa njia za udanganyifu. Hii ni jinai, na ni uhujumu uchumi.

Kwanini tunaacha kujadili hoja za EU tunawashambulia watoa hoja? Urafiki wa McAllister na Lissu haundoi ukweli kwamba tumetapeli hela za Corona. Wala urafiki wa Chadema na CDU hauondoi ukweli kwamba uchaguzi ulivurugwa na vyombo vya dola.

Hata kama McAllister angekuwa rafiki wa CCM bado hoja za kamati yake haziwezi kupuuzwa. Kaka Msando ni rafiki mkubwa wa kaka yangu mwingine Ally Bananga japo wanatofautiana vyama. Je, ikitokea Msando akafanya kosa huko CCM, halafu CCM wakamhukumu kwa sababu ya urafiki wake na Bananga ataridhika?

Tujadili hoja za EU na kuzitolea majibu bila kuwashambulia viongozi wake. Hoja za EU hata zingetolewa na mwanafunzi wa darasa la 3B kule Manda Ludewa, bado zingehitaji majibu. Tuhadili hoja, tusiwajadili watoa hoja.!

Msando Alberto aliandika kuhusu mjadala unaoendelea bunge la Ulaya kuhusu Tanzania kupokea pesa za Corona, pamoja na mapendekezo ya kamati ya mambo ya nje kutunyima msaada kwa sababu ya udanganyifu kwenye uchaguzi, wizi wa kura, watu kuuawa na wengine kutupwa jela. Wanahoji kama kuna haja ya kuendelea kuipa msaada nchi isiyoheshimu demokrasia.

Msando amedai tishio la EU kutunyima msaada ni kutokana na ushirika uliopo kati ya Chadema, CDU, Konrad Adenauer Stiftung na David McAllister.

Anadai kwa kuwa CHADEMA na chama cha CDU cha Ujerumani (anachotoka McAllister) ni wajumbe wa shirikisho la vyama vya kidemokrasia duniani (IDU), basi Chadema itakua imetumia nafasi hiyo "kuiharibia" Tanzania, hasa kwa kuwa McAllister ndiye Makamu Mwenyekiti wa IDU.

Ukivuliwa nguo chutama

Credit: G. Malisa
Prof anaamin utu KWANZA pesa badae ,akatoa na mfano wa mwalim
Ushauri ,ili mfano wake uwe sawasawa na kipindi Cha mwalim
WAZIRUDISHE HIZO PESA ZA CORONA
 
Hahaha mgogoro wa CCM sio mgogoro wa Tanzania kachanganya huyu.

Anataka watanzania tushiriki vita ya ccm, kwanini?!
 
EU wametoa hoja zao ambazo ni kukosekana demokrasia kwenye uchaguzi mkuu, polisi kuhujumu uchaguzi, na kupokea pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona. Hizi ndio hoja za EU ambazo kaka Msando amekwepa kuzijibu badala yake amemshambulia mtoa hoja (McAllister) na chama chake.

Lakini tujiulize je madai ya EU ni ya uongo? Je vyombo vya dola havikutumika kuvuruga uchaguzi? Je, watu hawakukamatwa? Je hakuna walioripotiwa kuuawa? Je hatukuchukua pesa za corona? Kwanza kuchukua pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona ni utapeli. Serikali imejipatia pesa kwa njia za udanganyifu. Hii ni jinai, na ni uhujumu uchumi.

Kwanini tunaacha kujadili hoja za EU tunawashambulia watoa hoja? Urafiki wa McAllister na Lissu haundoi ukweli kwamba tumetapeli hela za Corona. Wala urafiki wa Chadema na CDU hauondoi ukweli kwamba uchaguzi ulivurugwa na vyombo vya dola.

Hata kama McAllister angekuwa rafiki wa CCM bado hoja za kamati yake haziwezi kupuuzwa. Kaka Msando ni rafiki mkubwa wa kaka yangu mwingine Ally Bananga japo wanatofautiana vyama. Je, ikitokea Msando akafanya kosa huko CCM, halafu CCM wakamhukumu kwa sababu ya urafiki wake na Bananga ataridhika?

Tujadili hoja za EU na kuzitolea majibu bila kuwashambulia viongozi wake. Hoja za EU hata zingetolewa na mwanafunzi wa darasa la 3B kule Manda Ludewa, bado zingehitaji majibu. Tuhadili hoja, tusiwajadili watoa hoja.!

Msando Alberto aliandika kuhusu mjadala unaoendelea bunge la Ulaya kuhusu Tanzania kupokea pesa za Corona, pamoja na mapendekezo ya kamati ya mambo ya nje kutunyima msaada kwa sababu ya udanganyifu kwenye uchaguzi, wizi wa kura, watu kuuawa na wengine kutupwa jela. Wanahoji kama kuna haja ya kuendelea kuipa msaada nchi isiyoheshimu demokrasia.

Msando amedai tishio la EU kutunyima msaada ni kutokana na ushirika uliopo kati ya Chadema, CDU, Konrad Adenauer Stiftung na David McAllister.

Anadai kwa kuwa CHADEMA na chama cha CDU cha Ujerumani (anachotoka McAllister) ni wajumbe wa shirikisho la vyama vya kidemokrasia duniani (IDU), basi Chadema itakua imetumia nafasi hiyo "kuiharibia" Tanzania, hasa kwa kuwa McAllister ndiye Makamu Mwenyekiti wa IDU.

Ukivuliwa nguo chutama

Credit: G. Malisa
MAKOFI TAFADHARI............
Nina wasiwasi mkubwa sana kwa watu wa nchi yangu kugeuza kila kitu kuwa siasa hata kwa mambo yenye maslahi kwa taifa langu yangeuzwa siasa chafu ili yapuuzwe. Amini amini nawaambia sasa hivi hata mtu mtu akiiba 5 litageuzwa siasa na baadae litatupwa, kwani hapo ndipo wametufikisha na ndipo walipopataka tusiwe kama taifa tena.
 
Kwa kweli Wakoloni wafanye mpango wa kurudi Africa. Hatuwezi kujiongoza, hatuwezi kujitawala, hatuwezi kuchaguana, tunauana, tunatafuna mali za umma na misaada, hatuwezi lolote. Hatuwezi.
 
Katika maisha ata kama unacho kidogo jitahid kukisimamia hicho hicho, lakin pale unapo acha mwanya afu mtu mwingine anataka akutawale kifikra apo unaweza jikuta unapoteza kila kitu

Sasa pro. Kabudi yeye alichokifanya ni kusimama katika kile anachokiamini kama kiongonzi mwenye maono ya mbali katika nchii hi ya Mh JPM
Mlipoharibu ni hapo kusema Kabudi ana maono ya mbali!! Unamaanisha Kabudi gani? Ni huyu Kabudi ambaye Rais Magufuli alisema amekula pumbavu nyingi, na yeye Kabudi alipoambiwa hivyo akawa anakenua meno na kyzungusha macho?

Nadhani Kabudi na huo uprofesa wake wa family ni hasara kubwa kwa Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom