Prof. Kabudi haeleweki, asema mikataba ya zamani haitavunjwa, ila wapya watapewa leseni sio mikataba

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,873
Screenshot_2017-07-06-16-26-49.png

MIKATABA MADINI KUTOVUNJWA

WAZIRI wa katiba na sheria, Prof. Palamagamba Kabudi amesema mikataba iliyopo ya madini haitavunjwa licha ya mabadiliko ya kisheria yaliyopitishwa na Bunge .
Badala yake alisema mikataba hiyo iliyopo ni ya mwisho kwani kuazia sasa wawekezaji watakaokuja katika sekta hiyo watatumia leseni.

Akihitimisha hoja ya mjadara wa Mswada wa sheria ya mabadiliko ya sheria mbalimbali ya mwaka 2017 bungeni , Waziri Kabudi alisema sheria hiyo mpya ikisaidiwa na Rais itabadilisha mfumo uliopo kutoka mikataba kwenda leseni.

Aidha, alisema , serikali itafanya marejeo ya mikataba hiyo iliyopo na kwamba taarifa ya mapitio hayo itatolewa kwa Bunge.
“Sasa tungeendelea na (mfumo wa) mikataba inamana tungekuwa tumevunja hiyo mikataba (iliyopo),” alisema Prof. Kabudi.
“Sisis tunasema njoo kwa majadiliano , na niseme hii ndio mikataba ya mwisho.”

Alisema kwa mikataba hiyo kuendelea kuendelea kutambulika, hakuna mwekezaji atakayeweza kuwaburuza kwenye mahakama za usuluhishi kwasababu mikataba yao haijavunjwa.
“Ila tunasema njooni tuzungumze. Lakini kuzungumza nini? Hapo tunaangalia mambo ambayo hayakubaliki .”

Hata hivyo kampuni ya acacia, moja ya makampuni ya uchimbaji madini nchini, juzi ilitangaza kufungua “kesi” ya kuomba upatanishi wa mgogoro unaoendelea baina yake na serikali kuhusu zuio la usafirishaji wa makanikia.

Taarifa iliyotolewa na Acacia ilisema kampuni hiyo imewasilisha taarifa hiyo ya kutafuta upatanishi kwa niaba ya kampuni zake tanzu za Bulyanhulu Gold Mine (BGML) na Pangea Minerals Limited (PML) inayomiliki mgodi wa Buzwagi.`

K
 
Anamfurahisha Dikitekta uchwara, Professor mzima anaiabisha taaluma yake kwa kumfurahisha Dikitekta. Wasomi wa Tanzania njaa zinawasumbua sana. Ni bora Taifa kutokuwa na wasomi kuliko kuwa na wasomi koko, wasomi wanaowafurahisha wanasiasa na kuramba miguu ya hawa wanasiasa ambao wengi wao ni magaidi kazi kutuangamiza watanzania kwa faida yao na wazungu wao walio migodini. Siioni faida ya wasomi wa Tanzania zaidi ya kuwatumikia Wazungu, wenyewe CCM wana waita wawekezaji. CCM ni Genge la Majasusi na wala siioni tofauti ya CCM na Dash. Mikataba yote ya kipuuzi waiisaini CCM kisirisiri halafu leo wanakuja kwetu tuwaone kuwa ni wazalendo kumbe ni wanafiki
 
Jf siku hizi inaletewa makapi ya Swahili times na Insta kwi kwi kwi!!

poleni kwa kukosa hoja
 
Ameshabadilisha rangi yake kuwa kijani mnategemea atatofautiana nao?

Ni msomi yupi alishaingia CCM toka kwenye taasisi za kitaaluma akabaki kuwa na akili na uwezo wake?
 
Nilishahisi kuwa huyu akishachanganyika tu na Ukoo wa Panya basi hatokuwa tena yule Prof Kabudi wa Tume ya Jaji Warioba.
Ujinga mtupu.

Hawa Watu tunaowaita wasomi ndio walioliangamiza hili taifa letu kwa mikataba ya kihuni, wajeuri na wanafiki kila siku wanataka waombewe wao tu pamoja na kuiba kote bado tuwaombee ili waendele kutuibia.

Maprofessor njaa tu hawa
 
Watanzania ni wagumu sana kuelewa,

kwanza nashukuru sana serikali kwa kubadili mfumo kutoka mkataba kwenda kwenye leseni, yaan ni hivi, Mwekezaji mpya akija kutaka kuwekeza kwenye sekta, atapewa Leseni ambayo itakuwa na masharti yote muhimu,

Vile vile, mikataba yote ya sasa iliyopo ndiyo itakuwa ya mwisho, kwa Lugha nyingine, hakuna tena mkataba bali leseni.

Tatu, Kwa mikataba hii ambayo ilishaingiwa, watakaa na wahusika ili ipitiwe upya tena, maana ndani ya mikataba hiyo kuna kipengele kinaruhusu kufanyiwa mapitio upya kila baada ya miaka 3&5.

narudia tena, Mikataba ya sasa itabaki kama ilivyo, hii ina maana kuwa leseni inayopendekezwa hawa haitawahusu.
 
Anamfurahisha Dikitekta uchwara, Professor mzima anaiabisha taaluma yake kwa kumfurahisha Dikitekta. Wasomi wa Tanzania njaa zinawasumbua sana. Ni bora Taifa kutokuwa na wasomi kuliko kuwa na wasomi koko, wasomi wanaowafurahisha wanasiasa na kuramba miguu ya hawa wanasiasa ambao wengi wao ni magaidi kazi kutuangamiza watanzania kwa faida yao na wazungu wao walio migodini. Siioni faida ya wasomi wa Tanzania zaidi ya kuwatumikia Wazungu, wenyewe CCM wana waita wawekezaji. CCM ni Genge la Majasusi na wala siioni tofauti ya CCM na Dash. Mikataba yote ya kipuuzi waiisaini CCM kisirisiri halafu leo wanakuja kwetu tuwaone kuwa ni wazalendo kumbe ni wanafiki

Wakati Magufuli anahangaika na makinikia nilikuwa namsikitikia sana kwa sababu anawadanganya watanzania wazi wazi,Anafanya vitu ambavyo haviwezekani kabisa nilijua tu anawadanganya watanzania,CCM n waongo sana kuwahi kutokea kwwnye dunia hii,Asingeweza kuvunja mikataba ilikuwa n poyoyo tu

Kamati alizounda ilikuwa ni kamati ya kufanya kazi kwa Kumfurahisha bwana yule...
 
Watanzania ni wagumu sana kuelewa,

kwanza nashukuru sana serikali kwa kubadili mfumo kutoka mkataba kwenda kwenye leseni, yaan ni hivi, Mwekezaji mpya akija kutaka kuwekeza kwenye sekta, atapewa Leseni ambayo itakuwa na masharti yote muhimu,

Vile vile, mikataba yote ya sasa iliyopo ndiyo itakuwa ya mwisho, kwa Lugha nyingine, hakuna tena mkataba bali leseni.

Tatu, Kwa mikataba hii ambayo ilishaingiwa, watakaa na wahusika ili ipitiwe upya tena, maana ndani ya mikataba hiyo kuna kipengele kinaruhusu kufanyiwa mapitio upya kila baada ya miaka 3&5.

narudia tena, Mikataba ya sasa itabaki kama ilivyo, hii ina maana kuwa leseni inayopendekezwa hawa haitawahusu.

Sasa leseni iliyotangazwa haitawahusu je kwann alikuwa anawadanganya watanzania kuwa atavunja mikataba ya madini wakati n kitu ambacho hakiwezekani?????
 
Back
Top Bottom