Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

Zamani nilikuwa nikiona mtu anaitwa Profesa au Dr najua ana akili kwelikweli wakati huo nilikuwa sijakutana na hawa kina Kabudi. Ndio maana kumbe watu wenye pesa zao hawataki watoto wao wasome vyuo vya hapa Tanzania.
 
Ni wazi sasa Tanzania munaongozwa na genge la watu wahuni wachache, tayari matabaka yanatapakaa, ni matokeo ya uongozi mbovu zaidi na watakao umia ni wananchi maskini. Kabudi anajua future yake tayari na familia yake, yaani inasikitisha sana kwa viongozi wenye roho mbaya kama hawa.
 
Kama tuna nguvu ya kusimama wenyewe sioni haja ya kupiga kelele, tuonyeshe kwa vitendo.
 
Jamaa usee umemvaa vibaya,uyu si ndio yule alienda Madagascar na kurudi na vichupa vya dawa ya korona,jamaa hamna kitu ,akizungumza unahisi ni mtu anaefata jazba akipigiwa makofi ndio husidi kupoteza muelekea.

Jamaa amevuruga sana au hawa ndio watu wanaosaboteji utawala wa Magufuli,kabudi amevuruga vibaya mno ,hafai hata dakika moja kuwepo katika wizara na uwaziri huo.
 
Kama hatuhitaji urafiki wa "Mabeberu" sasa mbona tulikuwa tunapigania Zimbabwe wafanyiwe wepesi? Au hatujui sababu za Zimbabwe kufikia huko?
 
Loo, mkuu 'MLA PANYA SWANGA', nimekusoma vizuri sana. Una njia yako ya kipekee ya kueleza jambo na likaeleweka.

Hiyo mistari ya mwanzo juu ya biblia, ilitaka kunitoa kwenye reli, lakini ulivyoiunganisha kwa hoja uliyonuia kuieleza kiufundi kabisa, nilisimama vyema kwenye ile reli.

Hongera kwa kipaji chako hiki.
 
Huyu kabudi na wenzie wangekuwa watu wenye chembe hata ndogo ya aibu, asingethubutu kusema haya aliyosema kwenye mkutano huo.

Ni kama vile alikuwa anawahutubia watu wasiokuwa na akili kichwani; watu wasioweza kutambua kitu chochote.

Kabudi na Magufuli wanadhani wamewashikia waTanzania akili zao. Wanachowaza wao ndicho wanachodhani waTanzania wote na jamii yote ya kimataifa ndicho wanachopaswa kufikiri.

Wanadhani wanapochomekea aliyofanya Mwalimu, watu watawapa hadhi ya uzalendo wasiyoistahili. Aliyoyafanya Mwalimu na wanayoyafanya wao ni mambo tofauti kabisa.

Hawa watu mwisho wao utakuwa wa aibu kubwa.
 
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haitakubali kudhalilishwa utu na heshima yake kama nchi huru, kupigishwa magoti kupata misaada na mikopo kutoka katika nchi yoyote duniani.

Akizungumza na wafanyakazi wa wizara ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kuongoza wizara hiyo, alisema Tanzania ipo tayari kushirikiana na nchi yoyote itakayoheshimu na kujali uhuru wake.

"Never Never (hapana) hatutaruhusu mikopo na misaada ambayo inadhalilisha nchi, hakuiruhusu wakati wa Mwalimu Julius Nyerere haitaruhusu katika utawala huu wa sasa," alisema.
Alisema Tanzania haijawahi kupigishwa magoti kwa ajili ya kupokea misaada na mikopo yenye masharti ya kudhalilisha nchi tangu wakati wa Mwalimu Nyerere.

"Alivunja uhusiano wa ubalozi wa Uingereza nchini 1965-1972 na kurudisha pauni milioni tano, pia alivunja uhusiano wa kibalozi na Ujerumani 1964 kwa kulazimisha kuvunja muungano wa Bara na Zanzibar na kurudisha fedha za nchini hiyo milioni 35 kutokana na kutaka nchi kukubali masharti yao,” alisema Kabudi.

“Nchi itasimamia heshima yake na haitapokea misaada na mikopo ambayo inavunja utu waje. Kati ya fedha na misaada, tutasimamia utu wetu. Hatutakubali kudharauliwa…sisi ni binadamu na tupo sawa na tupo tayari kuwasikiliza na kushirikiana kama yapo yaliyopungua kwao na kwetu kujadiliana."

Profesa Kabudi alisema nchi itashirikiana na wote walio tayari kushirikiana nayo kuzungumza kama kuna upungufu kwao na nchini, lakini hawatakuwa na mjadala kwa nchi itakayotaka kudhalilisha utu na heshima ya nchi.

Alisema Tanzania ipo tayari kujadiliana, kushauriana na haichagui rafiki na inakaribisha urafiki kutoka pande zote za dunia .

Alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuhakikisha kila balozi nchini inapata ilani ya uchaguzi na hotuba ya Rais John Magufuli ya kufungua Bunge la 12 Novemba 20 mwaka huu pamoja na ya kufunga Bunge aliyotoa Juni 16. Ameagiza pia wawe na waraka aliotoa Nyerere mwaka 1969 kwa watumishi wa ofisi ya Rais mambo ya nje.

Waziri Kabudi aliwashukuru watendaji wa wizara hiyo ambao katika kipindi cha miaka mitano wamechangia kupata mafanikio makubwa yakiwamo ya kufungua balozi mpya tano na pia imeimarisha na kuongeza fursa za uwekezaji kupitia diplomasia ya biashara kwa kushawishi wawekezaji kuja nchini.

Alitoa mfano wa namna wawekezaji walivyobadili mkoa wa Simiyu kutokana na mabalozi wa Tanzania nchni Malaysia na Singapore, Ramadhan Dau na Elizabeth Kione wa Uturuki kupeleka wawekezaji katika mkoa huo na mikoa mingine.

Aliwataka wafanyakazi wa ziara hiyo kusoma Ilani ya Uchaguzi yenye kurasa 303 kuangalia maeneo yanayowahusu na mengine wanayoweza kusaidia kuwezesha, kushauri na kutekeleza moja kwa moja.

Miongoni mwa mambo ambayo ilani ya Uchaguzi imeagiza ni kuhusu diplomasia ya uchumi kwa kutaka wizara na mabalozi kuongeza kasi ya kufanya uchumi na kuweka mikakati ya kuendeleza biashara ya Tanzania na nchi jirani.

Katibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wilbert Ibuge alisema wakati huu si wa kupeana raha ni kuchapa kazi kwa kasi na kujituma.


HabariLeo
 
Back
Top Bottom