Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haitakubali kudhalilishwa utu na heshima yake kama nchi huru, kupigishwa magoti kupata misaada na mikopo kutoka katika nchi yoyote duniani.

Akizungumza na wafanyakazi wa wizara ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kuongoza wizara hiyo, alisema Tanzania ipo tayari kushirikiana na nchi yoyote itakayoheshimu na kujali uhuru wake.

"Never Never (hapana) hatutaruhusu mikopo na misaada ambayo inadhalilisha nchi, hakuiruhusu wakati wa Mwalimu Julius Nyerere haitaruhusu katika utawala huu wa sasa," alisema.

Alisema Tanzania haijawahi kupigishwa magoti kwa ajili ya kupokea misaada na mikopo yenye masharti ya kudhalilisha nchi tangu wakati wa Mwalimu Nyerere.

"Alivunja uhusiano wa ubalozi wa Uingereza nchini 1965-1972 na kurudisha pauni milioni tano, pia alivunja uhusiano wa kibalozi na Ujerumani 1964 kwa kulazimisha kuvunja muungano wa Bara na Zanzibar na kurudisha fedha za nchini hiyo milioni 35 kutokana na kutaka nchi kukubali masharti yao,” alisema Kabudi.

“Nchi itasimamia heshima yake na haitapokea misaada na mikopo ambayo inavunja utu waje. Kati ya fedha na misaada, tutasimamia utu wetu. Hatutakubali kudharauliwa…sisi ni binadamu na tupo sawa na tupo tayari kuwasikiliza na kushirikiana kama yapo yaliyopungua kwao na kwetu kujadiliana."

Profesa Kabudi alisema nchi itashirikiana na wote walio tayari kushirikiana nayo kuzungumza kama kuna upungufu kwao na nchini, lakini hawatakuwa na mjadala kwa nchi itakayotaka kudhalilisha utu na heshima ya nchi.

Alisema Tanzania ipo tayari kujadiliana, kushauriana na haichagui rafiki na inakaribisha urafiki kutoka pande zote za dunia .

Alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuhakikisha kila balozi nchini inapata ilani ya uchaguzi na hotuba ya Rais John Magufuli ya kufungua Bunge la 12 Novemba 20 mwaka huu pamoja na ya kufunga Bunge aliyotoa Juni 16. Ameagiza pia wawe na waraka aliotoa Nyerere mwaka 1969 kwa watumishi wa ofisi ya Rais mambo ya nje.

Waziri Kabudi aliwashukuru watendaji wa wizara hiyo ambao katika kipindi cha miaka mitano wamechangia kupata mafanikio makubwa yakiwamo ya kufungua balozi mpya tano na pia imeimarisha na kuongeza fursa za uwekezaji kupitia diplomasia ya biashara kwa kushawishi wawekezaji kuja nchini.

Alitoa mfano wa namna wawekezaji walivyobadili mkoa wa Simiyu kutokana na mabalozi wa Tanzania nchni Malaysia na Singapore, Ramadhan Dau na Elizabeth Kione wa Uturuki kupeleka wawekezaji katika mkoa huo na mikoa mingine.

Aliwataka wafanyakazi wa ziara hiyo kusoma Ilani ya Uchaguzi yenye kurasa 303 kuangalia maeneo yanayowahusu na mengine wanayoweza kusaidia kuwezesha, kushauri na kutekeleza moja kwa moja.

Miongoni mwa mambo ambayo ilani ya Uchaguzi imeagiza ni kuhusu diplomasia ya uchumi kwa kutaka wizara na mabalozi kuongeza kasi ya kufanya uchumi na kuweka mikakati ya kuendeleza biashara ya Tanzania na nchi jirani.

Katibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wilbert Ibuge alisema wakati huu si wa kupeana raha ni kuchapa kazi kwa kasi na kujituma.

HabariLeo
 
Niweke hapa hiyo list kwani hapa ni bunge la ulaya? Hizo pesa hazikutolewa na bunge ulaya ripoti haiendi kwao. Inaenda kwa waliotoa pesa kazi ya bunge la ulaya sio kutoa pesa za misaada halina hela. Hela bunge walizonazo ni za wao kulipana mishahara na posho tu

Hapo alipokuwa anahutubia Kabudi ni kwenye bunge la ulaya?
 
Mkuu hongera.
Huyu Proffesa wetu tangu alipoteuliwa alianza kuonyesha shaka kubwa sana nakumbuka kipindi Rais alivyoendaga Zimbabwa alirudi na akawa anawaombea msaha wa Zimbabwe kuombewa vikwazo lakini wiki hiyo Proffesa akawa anazinanga Nchi za magharibi kuwa kuna wengine walimfuata kwa ajili ya kumwomba Mbowe achiwe huru.
Kwa ujumla huyu Proffesa ataharibu diplamasia yetu.


Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
Watu wanauana kila kukicha Duniani sio Tanzania tu... na hili mnasababisha wenyewe wapiga mayowe....mnainfluence vijana wasio na hili wala lile na kuwaaminisha yasiyokuwepo.....

Kila serikali Duniani ina dosari zake.....ukiwa na kundi lisilofikiria lkapata viongozi wahemkaji tarajia vifo.

Hoja ya kura ni mfu....ninachojua mimi hata kura ungehesabu wewe JPM angeshinda awamu hii.
Mku una alalisha hayo. Tanzania hayakuzoeleka hayo

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
Huyu Kabudi anajitutumua nini? Yeye mwenyewe kapitishwa kwa nguvu za Magufuli ingekuwa kwa kawaida asingeenda popote.

Anapiga kelele tu huyo Kabudi tukiwekewa vikwazo hatutoboi hata kidogo. Ni haki serikali ya Magufuli kuwekewa vikwazo kwa sababu Magufuli na serikali yake wamebaka Democracy waziwazi na kila mtu anajua, Wasijifanye hawajui, wanajua kuwa wameiba kura na kuua watu kwa ajili ya kura. Aibu kwako Kabudi na wewe Magufuli.

Mnaua Watanzania ili mbakie madarakani. AIBU. Ninyi JamiiForums naomba msifute au msinifungie. Sijatukana mtu yeyote maana ninyi siku hizi mmeshakuwa mouthpiece wa serikali hii dhalimu.
 
Umuofia kwenu wapendwa.

Ktk biblia imeandikwa kitabu cha mwanzo kisa cha Musa na Mungu kilichopelekea Musa kufichama.

Mungu alimuita Musaa naye akaitika naamu, Mungu akamuuliza uko wapi?
Swali hili lilikuwa geography question yaani aeleze location yuko wapi lakini cha ajabu Musa akajibu swali kinyume kabisa eti ni mwanamke huyu uliyenipa ndiye alinidanganya nikala.Ukichunguza vizuri utagundua Musa alikuwa anamlaumu Mungu wetu.

Huyu waziri Kabudi ameulizwa swali ajibu kuhusu pesa za korona walizochukua huku wakijua wazi kwa matamshi yao korona haipo nchini na kutumia pesa hizo kwa ajili ya kampeni za chama yeye amejibu kuwa tz ni nchi huru na wao hawawezi kuhusudu misaada isiyoheshimu utu wao, hiki ni kituko kama cha Musa tu.

Kabudi umeulizwa swali ueleze mapato na matumizi maana wenye pesa washaona kuna mislocation of fund na pia washaona kuna udanganyifu ulitumika ili kujipatia pesa hivyo wanahitaji ikibidi pesa yao iwarudie wewe unaleta comedian.

Ukikosa uaminifu uongo hutamalaki mno na utukufu kupungua au kuisha.

Suluhu ya mwisho kwa serikali hii ya ccm ikubali katiba mpya na tume huru ila iombe uchaguzi usirudiwe ili kuwepo na unafuu vinginevyo tutawaona akina Musa wengi kama prf Kabudi alivyoanza kwa kujibu OP.
 
Hivi, kwanini ni “Mambo ya Nje na ushirikiano wa Africa Mashariki” na sio ushirikiano wa Kimataifa?
 
Back
Top Bottom