Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

antimatter

JF-Expert Member
Feb 26, 2017
3,981
2,000
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haitakubali kudhalilishwa utu na heshima yake kama nchi huru, kupigishwa magoti kupata misaada na mikopo kutoka katika nchi yoyote duniani.

Akizungumza na wafanyakazi wa wizara ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kuongoza wizara hiyo, alisema Tanzania ipo tayari kushirikiana na nchi yoyote itakayoheshimu na kujali uhuru wake.

"Never Never (hapana) hatutaruhusu mikopo na misaada ambayo inadhalilisha nchi, hakuiruhusu wakati wa Mwalimu Julius Nyerere haitaruhusu katika utawala huu wa sasa," alisema.
Alisema Tanzania haijawahi kupigishwa magoti kwa ajili ya kupokea misaada na mikopo yenye masharti ya kudhalilisha nchi tangu wakati wa Mwalimu Nyerere.

"Alivunja uhusiano wa ubalozi wa Uingereza nchini 1965-1972 na kurudisha pauni milioni tano, pia alivunja uhusiano wa kibalozi na Ujerumani 1964 kwa kulazimisha kuvunja muungano wa Bara na Zanzibar na kurudisha fedha za nchini hiyo milioni 35 kutokana na kutaka nchi kukubali masharti yao,” alisema Kabudi.

“Nchi itasimamia heshima yake na haitapokea misaada na mikopo ambayo inavunja utu waje. Kati ya fedha na misaada, tutasimamia utu wetu. Hatutakubali kudharauliwa…sisi ni binadamu na tupo sawa na tupo tayari kuwasikiliza na kushirikiana kama yapo yaliyopungua kwao na kwetu kujadiliana."

Profesa Kabudi alisema nchi itashirikiana na wote walio tayari kushirikiana nayo kuzungumza kama kuna upungufu kwao na nchini, lakini hawatakuwa na mjadala kwa nchi itakayotaka kudhalilisha utu na heshima ya nchi.

Alisema Tanzania ipo tayari kujadiliana, kushauriana na haichagui rafiki na inakaribisha urafiki kutoka pande zote za dunia .

Alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuhakikisha kila balozi nchini inapata ilani ya uchaguzi na hotuba ya Rais John Magufuli ya kufungua Bunge la 12 Novemba 20 mwaka huu pamoja na ya kufunga Bunge aliyotoa Juni 16. Ameagiza pia wawe na waraka aliotoa Nyerere mwaka 1969 kwa watumishi wa ofisi ya Rais mambo ya nje.

Waziri Kabudi aliwashukuru watendaji wa wizara hiyo ambao katika kipindi cha miaka mitano wamechangia kupata mafanikio makubwa yakiwamo ya kufungua balozi mpya tano na pia imeimarisha na kuongeza fursa za uwekezaji kupitia diplomasia ya biashara kwa kushawishi wawekezaji kuja nchini.

Alitoa mfano wa namna wawekezaji walivyobadili mkoa wa Simiyu kutokana na mabalozi wa Tanzania nchni Malaysia na Singapore, Ramadhan Dau na Elizabeth Kione wa Uturuki kupeleka wawekezaji katika mkoa huo na mikoa mingine.

Aliwataka wafanyakazi wa ziara hiyo kusoma Ilani ya Uchaguzi yenye kurasa 303 kuangalia maeneo yanayowahusu na mengine wanayoweza kusaidia kuwezesha, kushauri na kutekeleza moja kwa moja.

Miongoni mwa mambo ambayo ilani ya Uchaguzi imeagiza ni kuhusu diplomasia ya uchumi kwa kutaka wizara na mabalozi kuongeza kasi ya kufanya uchumi na kuweka mikakati ya kuendeleza biashara ya Tanzania na nchi jirani.

Katibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wilbert Ibuge alisema wakati huu si wa kupeana raha ni kuchapa kazi kwa kasi na kujituma.


HabariLeo
 

Wo shi niubi

JF-Expert Member
Aug 14, 2015
942
1,000
Hii dunia ni ngumu sana kuielewa, kina Pompeo wanahubiri katika mataifa mengine free and fair election, viongozi wakubali matokeo ya uchaguzi wakati huo Pompeo hamtambui na kumkubali Biden kama mshindi halali wa USA, hii inatuambia nini ndugu zangu?
 

mbongo_halisi

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
5,129
2,000
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haitakubali kudhalilishwa utu na heshima yake kama nchi huru, kupigishwa magoti kupata misaada na mikopo kutoka katika nchi yoyote duniani.
Safi sana japo Lissu na Zitto watakuwa na hasira za sisi kukataa ushoga ila habari ndiyo hiyo. Tuwaachie wao wenyewe huo ushoga.
 

Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,345
2,000
Huyu jamaa alinifanya nihairishe kusomea PHD pamoja na kuchaguliwa kusomea kozi hiyo Mlimani.

Yaani ukimuangalia unaona kabisa anaongea aliyotumwa akaseme Prof mzima unalazimishwa kuongea pumba kwa ajili ya kulinda nafasi yako
Kipi bora kulinda taaluma au kulinda tumbo
 

Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,345
2,000
Hii dunia ni ngumu sana kuielewa, kina Pompeo wanahubiri katika mataifa mengine free and fair election, viongozi wakubali matokeo ya uchaguzi wakati huo Pompeo hamtambui na kumkubali Biden kama mshindi halali wa USA, hii inatuambia nini ndugu zangu?
Wao mawazo binafsi sio mawazo ya wote sisi mawazo binafsi ya mtawala ndiyo sheria.Wao uongozwa kwa katiba na sheria sisi uongozwa na maagizo
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,779
2,000
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haitakubali kudhalilishwa utu na heshima yake kama nchi huru, kupigishwa magoti kupata misaada na mikopo kutoka katika nchi yoyote duniani...
Hii wizara naona Prof Kabudi imeshampwaya kabisa, pengine wamjaribu sasa January Makamba ama Emmanuel Nchimbi ambaye pia anaweza kuteuliwa kuwa mbunge

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
408
1,000
Huyu ana ukichaa.

Kila siku anapigiwa simu na Magufuli usiku na kuambiwa mpumbavu (Rais Magufuli aliwaeleza Watanzania wote, ikiwa ni oamoja na wake na watoto wa Kabudi ja Mpango), naye anakenua meno. Kama angekuwa ni mtu anayejali heshima yake, si angejiuzulu siku hiyo alipoambiwa mpumbavu kwa mara ya kwanza.

Kila siku, yeye na Mpango wanaambiwa wapumbavu, wanakenua meno, halafu leo atuambie eti analinda utu na heshima ya Taifa. Ameshindwa kulinda utu na heshima yake binafsi, halafu anaongelea Taifa!!

Na Magufuli kawateua wao wawili tu ili apate wa kuwaambiwa wapumbavu kila siku, akijua kwa ujuha wao watafurahia. Nadhani wasipotukanwa huwa wanachanganyikiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

antimatter

JF-Expert Member
Feb 26, 2017
3,981
2,000
.......Ningependa kujua hao wapiga makofi ni akina nani. Bila shaka watakuwa ni akina Bia yetu, Johnthebaptist, magu2016, Jane Lowassa, mama D.... Nchi yaani ina watu wengi sana wasiojitambua. Wako kama mbwa. Wakipata chakula tu basi kazi yao ni kutikisa mkia tu kila wanapomwona anayewapa chakula!
Hawa watu ni wachumia tumbo hatari, hawana utu kabisaa. Labda hata siyo Watanzania
 

MrFroasty

JF-Expert Member
Jun 23, 2009
961
500
Niwakumbusheni tuu izo fedha za misaada zinatoka kwa wananchi walipa kodi barani ulaya. Wana haki ya kuhoji inakuwaje zinapewa serekali ambazo hazi heshimu haki za binaadamu.

Kuanza kutishia kama umeshinda vita ya Iddi Amini na kuanza kukimbilia kama TZ ni taifa huru. Nadhani ni yale yalioolezwa na hao wabunge namnukuu mmoja wao "..the relation with Tanzania has been difficult". Hii inatoa picha kamili kama uongozi wa Tanzania haufahamu kinachojadiliwa na kupelekea uhusiano wake kuwa mgumu kimataifa. Ukipewa msaada wa kukabiliana na covid na kupewa muongozo na WHO, halafu ukafanya tofauti sasa utarajie nini kutoka kwa mfadhili ? Ataridhishwa tuu na kuanza kupiga makofi ?

Nadhani uongozi wa Tanzania ujitafakari hususan katika masuala ya haki za binadaamu, demokrasia na uhusiano wa kimataifa.Prof. Kabudi na wenzake waache kuwa defensive na badala yake watumie mapungufu hayo kuboresha hali ilivyo. Huu ndio mtazamo wa mtu anaependa maendeleo.
 

mkamanga original

JF-Expert Member
Jan 21, 2015
334
500
Wakati tunajipanga kujidhatiti kutopokea mikopo toka nchi wahisani,tujipange kurudisha fedha zao Eu 27M,nadhani huo ndio uungwana na utu wenyewe ambao Kabudi anasisitiza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom