Prof Kabudi agonga mwamba katiba mpya, alianza kwa matamko

Chifyono

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
921
1,658
Wakuu

Mtakumbuka baada ya prof. Kabudi Palamagamba kupata teuzi ya kuwa waziri wa katiba na sheria hapa nchini alianza kwa kasi kubwa na ya ajabu, waswahili wengi tulimuunga mkono na tukawa na imani naye kwamba katiba mpya inakuja

Prof Kabudi alianza kwa kuweka katiba mpya kama kipaumbele chake pindi anapoanza kuitumikia wizara yake, hili lilikuwa ni tamko tu lisilotekelezeka kama yalivyomatamko ya mawaziri wengine wanavyojitutumua wakipata teuzi

Ni wazi sasa Prof Kabudi amefail katika hili kutokana na kauli ya waziri mkuu kwamba hiki si kipaumbele cha awamu ya 5

Yuko wapi prof Kabudi waziri wa sheria na katiba, walau alitolee neno hii kauli ya waziri?

Kwa kuwa kipaumbele chake kimeshindwa, anaonaje akijiuzuru kwani mtazamo wake uko against na awamu hii kupisha waziri mwingine atakayeendana na serikali hii
 
katiba mpya si kwamba ni muhimu tu bali ni lazima kabla ya kuingia uchaguzini 2020.... na itapatikana tu by hooks and crooks.

tunamsubiri Lissu wetu (mbabe wao) arejee!
 
Mtatafuta kila aina ya fitna
Lkn mwishoe mtabakia midomo wazi
Wakati hao hao walishapewa na vyeti vya kuwatunuku kwa kutetea mali za wa tanzania
Mkuu nakushauri uje na gia ingine hii imeshapanguliwa
 
Waziri asiye na mbwembwe ni Dr. Hussein Mwinyi tu! Wengine wengi ni wakurupukaji.

Lwenge wa Maji nae Hakuwa na Mbwembwe lakin imem cost na nasikia Jimbo lake la Wang'hombe sijui anaandaliwa Gryson Msigwa 2020

Hata Dkt Mahiga nae Hana Mbwembwe!

Mzee hataki Mwanasiasa vuguvugu ni ama uwe Moto au baridi !

Hussein huenda anaadaliwa kwa Znz 2020 na ikishindikana nae ajiandae kupumzishwa kwa 'utendaji usioridhisha'
 
sijui kama status ya mtu itabaki km ilivyokuwa mwanzo.time will tell I think.wakati mwingine naona ni bora wanazuoni wakabaki kama wanazuoni badala ya kupelekwa kwenye siasa japo kuna ugumu wa kutofautisha.
 
Lwenge wa Maji nae Hakuwa na Mbwembwe lakin imem cost na nasikia Jimbo lake la Wang'hombe sijui anaandaliwa Gryson Msigwa 2020

Hata Dkt Mahiga nae Hana Mbwembwe!

Mzee hataki Mwanasiasa vuguvugu ni ama uwe Moto au baridi !

Hussein huenda anaadaliwa kwa Znz 2020 na ikishindikana nae ajiandae kupumzishwa kwa 'utendaji usioridhisha'
Mkuu umenikumbusha kijiji cha Ikingulla na Mdandu, na pale " nyumbanitu" penye miujiza ya kibena!!
 
Kwa sasa ukiniambia kama KATIBA itatuondolea foleni za magari, kuleta maji ya kutumia nyumbani (ndani), umeme, miundo mbinu kuwa bora (hasa baada ya mvua kutuumbuwa tena), uwajibikaji, huduma za afya bora, ustawi wa jamii, wazee kuangaliwa, kina mama kuwezeshwa, basi mimi niko na wewe kuitaka sasa hivi...
Otherwise itakuwa kama Bible tu, kitabu cha sheria, karatasi tu...
 
Back
Top Bottom