Prof. Kabudi agoma kujibu swali la Zitto kuhusu kesi ya Acacia, ahisi huenda ametumwa

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Swali la Kwanza: Zitto Kabwe ameuliza Bungeni kwanini tushtakiwe na Acacia wakati tuna mazungumzo nao?

Swali la Pili: Serikali pia ilitoa taarifa kwa umma kuwa tuliahidiwa kishika uchumba cha dola milioni 300 sawa na Tsh bilioni 700 na mpaka sasa hatujapata, na sasa sasa serikali imefungua kesi dhidi ya makampuni tanzu ya Acacia ya Bulyanhulu na Pangea kwa masuala yanayohusiana na tax avoidance, na hili ndio suala ambalo Serikali ilitakiwa kufanya tangia mwanzo na sio kadhia zote zile za makinikia. Je, serikali imejifunza kutumia maarifa kwenye kukabiliana na changamoto mbalimbali za nchi badala ya kutumia mabavu?

Majibu: Serikali haitatamka jambo lolote kwa kuwa itahatarisha hoja za serikali katika kesi hizo, na mtego huo uwe wa bahati mbaya ama wa kutumwa, profesa Kabudi hatonasa kamwe....

 
Prof Kalamaganda si alishadanganya bunge akidai washalipwa hiyo hela ya kishika uchumba na kwamba nyumba yenye hela ndo inayoingiliwa na wezi. So naona hela ipo changanya na zile dollah bil 5 plus dollah mil 300 naona nyumba imejaa hela.

NB: Hivi mtu anayedanganya bunge afanywe nini maana sijui sheria zinasemaje
 
Kwani mazungumzo na Acacia yalikuwa ni issue ya bunge?
Kwa miaka yote hiyo bunge(zitto akiwemo) halikuwahi kuona kuna makinikia yanasombwa
Mkuu,tumia hicho kichwa kufikiri na sio kubebea meno.

Makinikia yalikuwa yanasombwa chini ya serikali ipi? Ya CHADEMA? Ya ACT au CUF?

Wabunge wa CHADEMA na ACT ndio wengi bungeni ndio maana wakawalazimisha wanaCCM kupitisha sheria ya kuwaruhusu hao kusomba makinikia?

 
Looks hujaenda shule au umetoka shule au university ya kata
Hongera sana uliyesoma Yale! Ndio maana upeo wako wa kufikiri unadhani elimu ya "chuo cha kata" ni tofauti na "chuo cha wilaya"
 
Hakuna cha Mtego wala cha kutumwa wala nini ,kwa namna ambavyo Serikali ya awamu hii inavyo penda Sifa sidhani kama Mazungumzo yangekuwa ktk Hatua nzuri kama ingekuwa na kigugumizi cha namna hii ktk kutoa Majibu kwa Wananchi wake.

Serikali ni lazima itambue tofauti yake na Masela tu wa Mtaani ..
 
Back
Top Bottom