Prof JOYCE NDALICHAKO haya yakufikie hata kama yatakuuma, lakini ndio ukweli wenyewe

kacnia

JF-Expert Member
Sep 16, 2014
3,893
15,247
Nakusalimu kwa jina la jamuhuri.

Katika hali ambayo ni ya kawaida, umezuka mjadala juu ya uwezo wako wa kujieleza kwa kutumia lugha ambayo kwa asilimia 90 ndio iliyokutunuku kiwango cha elimu ulicho nacho (prof) na watanzania wengi wameenda mbali na kusema kuwa elimu yako ni ya ubabaishaji.

Mimi napingana nao, naamini unaweza kufanya bora zaidi ya hapo na wala sibezi jitihada ulizofanya mpaka sasa katika kuboresha mfumo wa elimu yetu hapa nchini.

Kielelezo:
Katika mkutano ulioshiriki hivi karibuni umesema haya
"Also aah, we, we political aah will by ensuring that we we we make aah the result known for example we have exhibitions for students to participate in science and technology so those who are doing aah innovative things we make them aah, we make public exhibition, so that people can come and see and appreciate aah, whot why is it important to to to invest in education and our country is the among the 19 countries which we aah we commited to kenyata decleration ahh"

katika kufasiri hiki ulichokisema hapa kwa niaba ya watanzania wengi ambao hawajaelewa kabisa ulikusudia kusema nini ni kwamba
"sisi wanasiasa tunahakikisha kuwa matokeo yanakuwa bayana kwa mfano, tuna maonyesho kwa ajili ya wanafunzi kushiriki katika sayansi na teknolojia hivyo kwa wale wanaofanya uvumbuzi tunafanya maonyesho ya hadhara ili watu waje waone na kupongeza/kukubali ni kwanini ni muhimu kuwekeza katika elimu na nchi yetu ni moja kati ya nchi 19 ambazo ni washirika wa azimio la kenyata"

kutoka katika maelezo hayo ni wazi kwamba sio tu unawadanganya hao uliokaa nao katika kikao bali unakiri kabisa kuwa mfumo wa elimu uliopo Tanzania si muafaka katika dunia hii iliyo jipambanua kuwa inategemea sayansi na teknolojia katika maendeleo ya watu na vitu kwa kuzungumza mambo ambayo eti yanafanyika (maonyesho ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia) wakati hayafanyiki kwa kiwango cha kitaifa na kwa lugha yako mbovu iliyojaa makosa kibao.

naomba nikuulize swali hili, ni shule gani hapa nchini inafundisha sayansi na teknolojia katika kiwango cha kuamsha ari ya uvumbuzi kwa wanafunzi wake?

Binafsi ninafahamu kuwa elimu tuliyonayo imejaa nadharia kwa asilimia zaidi ya 80 na aslimia za vitendo zilizobaki ni vitendo vilivyofanywa na wazee waliosoma miaka ya 70 huko mpaka leo.

Mfano tangu miaka ya nyuma mafunzo kwa vitendo kidato cha nne kushuka chini ilihusisha panzi, tandu, samaki mihogo nk. mpaka leo ni hayo hayo, ni lini unategemea mwanafunzi anayefanya vitendo hivi kuwa mshindani na faida kwa taifa katika upande wa sayansi na teknolojia ambao sasa upande huu umejikita katika kurahisisha maisha ya watu kwa uvumbuzi ambao ni muafaka kabisa kulingana na mahitaji ya mwanadamu?

leo hii wewe waziri wa elimu unaonekana mjinga kwa sababu kiwango chako cha elimu na uwasilishaji wa yale yaliyomo kichwani kwako havina uhusiano kabisa na hii ni kwasababu ya mfumo huu mbuvu ambao umeshiriki katika kukujenga na kukufanya uwe na uwanja finyu wa utendi kuanzia katika ubongo wako mpaka matokeo ya masuala unayoyafanya. na hili si kwako tu, ni kwa watanzania wengi ambao nao wanashiriki kukucheka.

Ikumbukwe ujinga ni kivumishi kinachotumika kwa mtu au kikundi cha kijamii ambacho hakina ujuzi wa vitu. Neno ujinga linaweza kutaja mtu kukosa mafundisho au elimu.

nini kifanyike?
katika kipindi hiki ambacho wewe waziri mwenye dhamana ambaye niliwahi kusikia mahali kuwa katika usomaji wako umewahi kuwa Tanzania one, umeshikilia wizara hii nyeti, unahitaji kufumua mfumo mzima wa elimu kwa kuhakikisha kuwa mfumo mpya unaingizwa ambao sasa utajikita katika kuwajenga wanafunzi wa ngazi zote nchini wawe na ujuzi wa juu wa sayansi na teknolojia na pia wawe washindani katika taaluma zao watakazochagua kiutendaji kuliko nadharia hii iliyojengeka kuwa msomi anatakiwa awe na uwezo mzuri wa kujieleza kwa lugha ya kiingereza. (nadharia sasa ichukue asilimia 30 huku vitendo vikiwa asilimia 70.

hii itasaidia kuzalisha wasomi ambao watakuwa na uwezo wa kuigeuza elimu yao kuwa pesa kama mnavyohubiri kila siku kuwa wasomi wanapaswa kujiajiri ili kupambana na wimbi la ukosefu wa ajira unaokumba waja wengi hapa nchini,

yangu ni mengi lakini kwa haya machache niliyoyaandika natumaini utayafanyia kazi na kutusaidia kuzalisha wasomi ambao hawatakuwa aibu kitaifa na kimataifa.

Don't turn a blind eye on my article, otherwise historia itahukumu. ukweli unauma ila usiposemwa unaleta ugonjwa wa kiharusi kwa anayeuficha na mimi sitaki kiharusi.

kacnia.
 
Mnamsimanga,mnamnanga au mnamchamba?Lugha kwa baadhi ya watu ni vipaji.Mumuache mtu wa watu.Jua limeshakuwa "unusu kasarobo"!Hawezi tena kujifunza kwa kadiri ya matarajio yetu.Atavunjika ulimi,kichwa kuuma,magego kulegea na mwili hautokubali kudunda na ile iitwayo body-language.Tusikosee tena katika "kuteuana" hizo nafasi.
 
Also aah, we, we political aah will by ensuring that we we we make aah the result known for example we have exhibitions for students to participate in science and technology so those who are doing aah innovative things we make them aah, we make public exhibition, so that people can come and see and appreciate aah, whot why is it important to to to invest in education and our country is the among the 19 countries which we aah we commited to kenyata decleration ahh"
 
Also aah, we, we political aah will by ensuring that we we we make aah the result known for example we have exhibitions for students to participate in science and technology so those who are doing aah innovative things we make them aah, we make public exhibition, so that people can come and see and appreciate aah, whot why is it important to to to invest in education and our country is the among the 19 countries which we aah we commited to kenyata decleration ahh"[emoji154l
yani ni tafrani tupu
 
Also aah, we, we political aah will by ensuring that we we we make aah the result known for example we have exhibitions for students to participate in science and technology so those who are doing aah innovative things we make them aah, we make public exhibition, so that people can come and see and appreciate aah, whot why is it important to to to invest in education and our country is the among the 19 countries which we aah we commited to kenyata decleration ahh"
Our poor madam!Aliongea kwa malalamiko sana.Mateso mingi.Aah..eeh..mmmh! Humming under breath!
 
... won't affect your language grammar.
Mastering a Language does not necessarily make you superior in your field unless that field is that Language..., thus her effectiveness can and should be measured in other qualities.., though am not sure in her capabilities on those other departments.

The point am trying to make is a Mute person can well manage her Job..., unless otherwise that job is pure politically....
 
Mastering a Language does not necessarily make you superior in your field unless that field is that Language..., thus her effectiveness can and should be measured in other qualities.., though am not sure in her capabilities on those other departments.

The point am trying to make is a Mute person can well manage her Job..., unless otherwise that job is pure politically....
Kinachosisitizwa hapa ni angalau ile lugha nyoofu tu ya kuwasiliana na kueleweka.Si kwamba aongee kama mtaalamu wa English.Hapana.Ni kama kiswahili tu au lugha nyingine.Kuwe na mpangilio na kueleweka.Asitengeneze ambiguities,atoe understandings!
 
Back
Top Bottom