Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Mimi ni raia ambaye sina chama, na daima ninaongea kile ninachoamini. Rais Magufuli anahitaji watu wa kumsaidia afanikiwe, si watu wa kumwunga mkono na kumsifia kwa kila kitu. Wapambe na watendaji ndio wanamkwamisha. Ninamsikia akilalamika kila anapopita hadi akasema kuwa saa nyingine anakuwa na "frustrations."
Watendaji na wanaCCM waache hii jadi ya kumsifia tu Rais na kumwuunga mkono. Wawe wanamsaidia kufanikisha yale mazuri anayotaka kufanya, na papo hapo wawe wanamshauri na hata kumzuia mengine ambayo anataka. Yeye ni binadamu, na ana mapungufu. Watendaji wanapaswa wamsaidie kufanikiwa yale mazuri, vinginevyo wanamwangusha. Napenda nitoe mfano.
Wakati ndege yetu ilipokamatwa Canada kwa amri ya mahakama ya kule, Rais Magufuli aliamua kupeleka ujumbe kwa waziri mkuu wa Canada kuomba atusaidie. Waziri mkuu alijibu kwamba hangeweza kufanya lolote na kwamba alikuwa na imani na mahakama. Taarifa hii niliisoma katika gazeti la Toronto:
...
Huu ni mfano wa ninachomaanisha. Ilitakiwa watendaji wa Rais wamwambie kwa dhati kabisa kwamba ombi lake kwa waziri mkuu wa Canada halingetekelezwa kwa kuwa kuna suala la mihimili kujitegemea. Nina hakika kuwa serikali ya awamu ya tano ina wanasheria ambao wanategemewa kujua hili suala la mihimili kutoingiliana.
Sasa kwa kuwa jadi iliyopo katika awamu ya tano ni ya kuunga mkono na kusifia kila anachowazia au kufanya Rais Magufuli, watendaji wamemsababishia Rais Magufuli dosari kimataifa. Taarifa hizi zilizochapishwa zitawafanya watu waulize inakuwaje Rais wa Tanzania akaomba msaada kwa suala lililokuwa mahakamani. Wanaweza kujiuliza ni nchi ya namna gani hiyo.
Je, huku ndiko kumwunga mkono Rais Magufuli? Yaani hata akiwa anaelekea kwenye kichaka cha simba, watu wasimzuie? Wahusika wajirekebishe.

Tanzanian president asks Trudeau for Bombardier plane back after it’s seized by court
British construction company says Tanzanian government owes it millions of dollars for canceled road project, so asked Quebec court to hold plane
nationalpost.com