Prof. Joseph Mbele arusha jiwe gizani

Adrian Stepp

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
2,764
2,581
Nimeona niseme neno kuhusu tamko la Lawrence Masha kujitoa CHADEMA, mimi raia ambaye sina chama.

Kwanza, ni muhimu tukumbushane kuwa kwa mujibu wa tangazo la kimataifa la haki za binadamu, ni haki ya kila binadamu kujiunga na wenzake katika kufuatilia au kufanikisha malengo halali, kama vile ya kisiasa. Ni haki ya kila mtu kujiunga na chama cha siasa.

Kujitoa katika chama na kujiunga na kingine ni haki ya kila mtu.
Kwa hivyo, kuwadhalilisha watu wanaojitoa kwenye chama fulani na kuingia kingine ni kuwakosea haki.

Hivi karibuni, kwa mfano, baada ya Lazaro Nyalandu kuhama CCM, tumemsikia Rais Magufuli akitamka kuwa watu hao wanaohama CCM ni mafisadi na majizi.

Kauli hiyo ya Rais inakiuka haki za binadamu, mojawapo ikiwa hiyo niliyotaja hapa juu.

Nyingine ni haki ya kila binadamu ya kutambuliwa kwa utu wake na kuheshimiwa, pasipo kudhalilishwa.
Hakuna mtu anayestahili kuitwa fisadi au jizi bila mahakama kuthibitisha ana hatia.

Hao ambao Rais Magufuli anawaita mafisadi na majizi hawajathibitishwa hivyo na mahakama yoyote.

Rais anakosea kwa hilo, na sherti akosolewe. Azingatie haki za binadamu.

Kwa mujibu wa tangazo la kimataifa la haki za binadamu, na kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, mtu akituhumiwa kwa kosa lolote, ana haki ya kuhesabiwa kuwa hana hatia hadi mahakama ithibitishe kuwa ana hatia.

Mahakama ziko kwa ajili ya kulinda haki, pamoja na haki za watuhumiwa.

Zaidi ya hilo suala la haki za binadamu, barua hii ya Masha ina ujumbe muhimu kwa CCM na CHADEMA.

Inaikumbusha CCM kwamba wapinzani wana wajibu na haki ya kuikosoa serikali inapobidi. Hilo ni fundisho kwa serikali ya awamu ya tano, ambayo inakuwa mbogo dhidi ya wakosoaji.


Tena ni ajabu kuwa serikali inayosemwa kwamba ina wasomi wengi iwe haivumilii kukosolewa. Msomi wa kweli ni mtu anayetambua na kuthamini hoja, zikiwemo hoja kinzani. Anathamini kuhoji, kujihoji, kuhojiana, na malumbano ya hoja. Anathamini kukosoa, kukosolewa, na kukosoana. Wasomi wa serikali ya awamu ya tano ni wasomi wa dizaini ya pekee.

Ni vigumu kuamini kama walizingatia masomo au walipitapitaje vyuoni.


Kwa upande wa CHADEMA, barua ya Masha ina fundisho pia.

Amewakosoa vizuri kwamba wanapaswa waende mbali zaidi ya kutegemea tu madhaifu ya CCM. Wajikite katika kutunga na kufafanua sera.

Binafsi, nimevutiwa na hoja hiyo. Kazi kwao.

Nini maoni yako?

Kwa ufupi:

Prof.Joseph Mbele alifundisha Literature Chuo kikuu cha DSM kuanzia Mwaka 1976 kisha Kuhamia Chuo cha Mt.Olaf Marekani kuanzia 1990 mpaka hivi sasa ambapo ni Mhadhiri Mwandamizi wa Literature!

Ni intake ya Marehemu Mbunda Msokile aliyekua mwalimu wa Kiswahili UDSM!
 
Kwahiyo kama ni fact kuwa wanahamia cdm ni majizi tatizo nini? Haki za binadam zingevunjwa kama huyo fisadi angezuiwa kuhama chama
 
Wasomi wetu wengi walimaliza vyuo ila hawakuelimika na hawaelemiki
 
Du Mbunda Msokile!Jina kubwa sana kwenye kiswahili cha Tanzania.Siasa za Tanzania kwa sasa zina ukakasi hakuna majukwaa huru ya mijadala,hakuna mikutano,kuna msamiati mpya "UCHOCHEZI"kwa mwendo tutajua kweli sera za vyama?Ukweli ni kwamba tumerdishwa nyuma hadi 1959!
 
Siasa ni Unyama , unyamani kiasi kwamba hizo haki za binadamu huwa zinakuja baada ya majanga.

USA wenyewe watunga haki za binadamu na wanaojidai wana democracy ila Trump alishinda huku akitumia lugha chafu sana ya matusi dhidi ya mama Clinton.

Siasa ni kujitoa utu na ufahamu, mwambie profesa awe mpole.
 
Bora waongee wakiwa huko ughaibuni kwani huku ndani pyupyu ingemhusu!
Nami nimuongezee prof kuwa huwezi kupata maendeleo ya aina yoyote kama utakataza watu kuwasiliana na kujadiliana. Niwashauri hao ccm wasome historia za kikomunisti za one man show zilivyodororesha chumi za nchi zao na kuzifanya maskini!
 
Kwahiyo kama ni fact kuwa wanahamia cdm ni majizi tatizo nini? Haki za binadam zingevunjwa kama huyo fisadi angezuiwa kuhama chama
Kabla ya kuhama wanakuwa siyo majizi ila wakiondoka tu kabla ya kufika chadema hapo njiani katikati wanakuwa wezi. Wakitua tu chadema, tayari ni majizi
 
Profesa ameshindwa kabisa kuchambua logic ya kitoto ya Masha kuhama CHADEMA.
Kivipi?
Laurence Masha alihamia CHADEMA kwenda kufuata nini? Kutalii? Kuangalia wanavyofanya siasa? Kusaka vyeo? Kujenga tena umaarufu wake?

Maswali yote hayo yanalipuka kwa sababu, Masha toka ahamie CHADEMA amekuwa akifanya siasa hizo hizo za CHADEMA ambazo leo hii anasema hazina mpango wa kuchukua dola. Nani alimkataza kufanya siasa anazoziamini yeye kuwa zitachukua dola? Nani wakuzifanya hizo siasa kama sio yeye aliyeziona kuwa zinafaa?
 
Kabla ya kuhama wanakuwa siyo majizi ila wakiondoka tu kabla ya kufika chadema hapo njiani katikati wanakuwa wezi. Wakitua tu chadema, tayari ni majizi
Kabla ya kuhama wanakuwa majizi ila wakihama tu kabla ya kufika chadema hapo njiani katikati wanakuwa wasafi. Wakituwa tu chadema wanakuwa wanatakasika.
 
Awe poropesa au profeseli hata lipumba amefundisha Stanford University, Sembuse huyo chuo hata Top 50 hakipo duniani, Maprofesa wote wa Kitanzania njaa inaanzia kichwani
Hoja zake zina mazingatio mengi, kama unampinga, mpinge kwa hoja
 
Mwambieni Mbele Mafisadi wanaotajwa tuhuma zao zimethibitishwa na chombo kingine kinachotunga sheria (BUNGE) ambacho hakiingiliwi na mhimili mwingine. BUNGE linapounda kamati kuchunguza mwenendo wa kiongozi linafanya kazi kama mahakama ndio maana wajumbe wake ni wanasheria, linakamata, na watuhumiwa wanaruhusiwa kuwa na wakili ikibidi na kutoa mapendekezo ya adhabu. Mafisadi wote waliohamia Chadema wamepitia ochungu hiki na walijiuzuru tokana na kutiwa hatiani na tume zilizowachunguza. Ndio HUKUMU yao
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom