Prof. Idris Mtulia na changamoto za maendeleo Rufiji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Idris Mtulia na changamoto za maendeleo Rufiji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Aug 12, 2009.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Aug 12, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,755
  Likes Received: 4,976
  Trophy Points: 280
  ..nimeona niwaletee habari za Prof.Idris Mtulia na jimbo la Rufiji kama zilivyoandikwa na gazeti la Mwanahalisi.

  ..Rufiji ina ardhi yenye rutuba na rasilimali nyingi sana. jambo la kusikitisha ni kwamba wako nyuma mno kimaendeleo.

  ..Prof.Mtulia anaelezea challenges walizonazo, malengo, pamoja na matarajio waliyonayo.

  ===================

  NI hazina. Ni lulu. Si mwingine, bali ni Profesa Idrissa Ali Mtulia, mbunge wa Rufiji, mkoani Pwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Profesa Mtulia, ni mmoja wa wabunge wachache kutoka kundi la wabunge wa mkoa huo, waliobahatika kupata elimu ya juu na kuitumia elimu yao kwa manufaa ya wananchi.

  Ndani na nje ya Bunge, Profesa Mtulia hachoki kuzungumzia matatizo ya wananchi wa jimbo lake na mkoa wa Pwani kwa jumla.

  Hiki ni kipindi cha kwanza cha ubunge kwa Profesa Mtulia, lakini utadhani amekaa bungeni kwa miaka 20 kutokana na uzito wa hoja anazozijenga.

  Katika mahojiano na MwanaHALISI majuzi, mjini Dodoma, Profesa Mtulia, pamoja na mambo mengine, anasema, "wananchi wa mkoa wa Pwani wako nyuma kimaendeleo. Ni wachache waliobahatika kupata elimu, ukilinganisha na wananchi wa mikoa mingine."

  Profesa Mtulia aliyefanya kazi serikalini kwa miaka mingi, hadi kufikia ngazi ya katibu mkuu wa wizara ya afya kutoka mwaka 1995 hadi 2001, anasema anatamani kugombea tena ubunge, lakini "maamuzi ya mwisho yatakuwa ya wananchi."

  Anasema, "Ukiniuliza mimi, nitakwambia mara moja kwamba nitagombea tena kipindi cha pili. Lakini wenye uamuzi wa mimi kugombea, au kutogombea ni wananchi wenyewe."

  Moja ya sababu kubwa ambayo inamfanya Profesa Mtulia kutamani kugombea tena ubunge jimboni kwake, ni kukosekana kwa maendeleo wilayani Rufiji na uduni wa maisha kwa wananchi wake.

  Anasema, "miaka ya nyuma, Rufiji ilikuwa inajitosheleza kwa chakula na kuna wakati chakula kilikuwa kinauzwa nje ya wilaya yetu. Lakini sasa, Rufiji haijitoshelezi hata kwa chakula chake yenyewe."

  Mazao ya mpunga, mahindi na mihogo, ambayo yalikuwa yakilimwa kwa wingi Rufiji, sasa yamebaki historia. Anasema, kilimo kilichokuwa kimeshamiri, hivi sasa kimeshuka kutokana na ukosefu wa zana za kisasa za kilimo.

  "Udongo wa Rufiji, ni wa aina yake. Huwezi kuendesha kilimo kwa kutumia jembe la mkono au plau (jembe la kukokotwa na ng'ombe). Unaweza kuendesha kilimo Rufiji kwa kutumia trekta tu. Kukosekana kwa zana hizi za kisasa, ndiko kulikorudisha nyuma kilimo chetu," anasimulia kwa uchungu Profesa Mtulia.

  Anasema mji wa Utete, ambako ndiko iliko hospitali ya wilaya na makao makuu ya wilaya ya Rufiji, ulikuwa angalau na umeme wa jenereta. Lakini hivi sasa mji wote upo gizani baada ya jenereta iliyokuwapo kuharibika.
  Anasema hata barabara za uhakika za kuunganisha wilaya hiyo na wilaya nyingine zimekufa.

  Hata hivyo, Profesa Mtulia anajivunia juhudi zake za kufufua umeme katika wilaya hiyo. "Mipango ya kurudisha umeme Utete imekamilika. Kuna mradi mkubwa wa umeme na tayari nyaya zimeshasambazwa katika maeneo husika," anasema.

  Anasema: "Umeme huu, hautawafaa wananchi wa Utete tu, hapana. Utafika hadi Kiwanga, Chumbi, Utunge, Nyandakatundu hadi Kindwiti. Ni mradi mkubwa, na kwa hakika, wa aina yake kwa wananchi wangu."

  Profesa Mtulia anasema, anataka kuiona Rufuji ikipata maendeleo makubwa. Anataka kuona Rufiji inapiga hatua za maendeleo kwa haraka, kutoka shule sifuri hadi makumi ya shule za sekondari za kidato cha kwanza hadi cha nne.
  Anataka shule za sekondari za Muhoro, Utete, Ikwiriri, Nkongo, Kibiti, Rwauluke, Mahege na Kibiti, ambazo zimeishia kidato cha nne, zifikishe kidato cha sita.

  "Ndoto yangu ni kuona angalau Rufiji inakuwa na shule japo mbili za kidato cha tano na sita, kabla ya mwaka 2011," anasema.

  Anasema, "Mbali na kuwa hatuna shule za kidato cha tano na sita, hata hizi shule tulizonazo hazina walimu wa kutosha wa kufundisha. Kuna shule zina mwalimu mmoja tu."

  Mbali na tatizo hilo, Profesa Mtulia anasema hata walimu wa kufundisha masomo ya sayansi, hawapo katika shule hizo.

  Rufiji ndiyo kwanza imeanza, na hakika, utadhani ni wilaya iliyoanzishwa jana. Maendeleo yaliyokuwapo kabla na baada ya uhuru, sasa hayaonekani kutokana na viongozi waliokuwapo kushindwa kuyaendeleza.

  Barabara zinazounganisha Rufiji, zilikuwa hazipitiki. Lakini angalau sasa, barabara ya Kibiti, Mkongo, Utete-Nyamwage, pamoja na kwamba haijajengwa kwa kiwango cha lami, angalau inapitika ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

  Hata barabara ya Ikwiriri, Mkongo, Mloka, Vikumbulu, Kisarawe, Bagamoyo-Tanga, inayoweza kupitisha magari yatokayo mikoa ya kusini kwenda Morogoro, Dodoma, Tanga, Arusha hadi nchi za Kenya, Rwanda na Burundi, iko mbioni kujengwa.

  Profesa Mtulia anasema barabara hiyo, tayari imechukuliwa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads). Kabla ya kujengwa kwa "Daraja la Mkapa," barabara ya kusini ilikuwa inapitia Utete.

  Anasema, "Njia hii sasa imekufa kutokana na kuharibika kwa kivuko cha Utete. Tayari serikali imetenga fedha za kununua kivuko kipya cha Utete chenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 50 za mizigo."

  Barabara ya kutoka Ndundu hadi Somanga ambayo ina ukubwa wa kilomita 60 imeanza kujengwa. Profesa anasema, "barabara zilizobaki ni zile za wilaya, ambazo zitajengwa kupitia mfuko wa barabara."

  Hata barabara ya Kipatimu kwenda Nyamwage, Nambunju, Muhoro hadi Ndundutawa, ambayo ina ukubwa wa kilometa 80, na ile ya Muhoro hadi Ruma, nazo zimeahidiwa kujengwa katika mwaka huu wa fedha.

  Kuhusu miradi ya maji, Profesa Mtulia anasema tayari kuna mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

  Vilevile, serikali imekarabati jengo la mkuu wa wilaya ya Rufiji ambalo lilijengwa na utawala wa Kijerumani kwa zaidi ya Sh. 400 milioni.

  Wilaya ya Rufiji inaungana na wilaya ya Morogoro Vijijini, kupitia mbuga ya wanyama ya Selous na mkoa wa Lindi, kupitia wilaya za Kilwa na Liwale.

  Profesa Mtulia aliwahi kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kuanzia mwaka 2002 hadi 2007. Ameoa na ana watoto sita.
   
 2. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nilifikiri wewe ndio unatakiwa uamue kwamba utagombea au hugombei, halafu ndio wananchi waamue kukuchagua au la! Vipi tena Profesa, mbona unachanganya madawa?

  Kama tatizo ni udongo wa Rufiji , na unahitaji zana za kisasa, mbona umesema sekunde mbili zilizopita kwamba zamani mlikuwa mnajitosheleza kwa kilimo. What happened to the udongo? What happened to the zana za kisasa, zimeota kutu au mmeziuza, au udongo ume evolve? Kwa kweli sikuelewi, maana ulisema:
  Okay, so what happened? Unajiita profesa, unaweza uchambuzi. What happened to the udongo wa Rufiji???
  Una maana gani "mradi wa kurudisha umeme," mmetengeneza hiyo generator au mmegundua vitega umeme vipya? Au mmenunua generator mpya? Mnayo long term plan ya vitega umeme? Yani hiyo generator nayo ikifyatuka cable moja, Rufiji gizani! Una generator moja, inakufa unakaa gizani miaka mia, unaleta nyingine moja! Ndio mipango ya maendeleo hiyo? Amazing!
  Kama shule zilizopo zina mwalimu mmoja mmoja, sasa kuna mantiki gani ya kusema ndoto yako kubwa ni kujenga zingine? Ha ha haaaa! Duu...
  Kuna maji au hakuna maji? "Tayari kuna mradi wa maji" maana yake nini, mnachimba kisima au kuna mpango wa kukinga maji ya mvua?

  Shukuru Mola unaongea na press people vilaza wa Bongo, anakufagilia na kuku admire. Prof. Idrissa Mtulia, among the best and the brightest of Tanzania's sophisticated elite, anasema kwamba wananchi ndio wataamua kama atagombea! Kuna hitilafu na hawa watu.

   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Point yake ni politically valid, simply anasema anajaribu kusoma alama za nyakati kama anatakiwa na wananchi au hatakiwi, ili aamue kugombea au kutogombea,

  - I wish wanasiasa wetu wote bongo wangekua na hii tabia.

  Respect.

  FMEs!
   
 4. K

  Keil JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Prof. ana kazi ngumu sana kwa kuwa location ya Jimbo lake ina matatizo makubwa na hasa uwepo wa Mto Rufiji ambao kwa kiasi kikubwa sana una athiri usafiri pamoja na makazi.

  Nilitembelea Jimbo hilo mwaka 2000, shule nyingi za msingi zina uhaba mkubwa sana wa walimu, hata wazaliwa wa huko huko hawakubali kurudi kwao kwenda kufundisha. Shule nyingi sana za msingi zina mwalimu mmoja ama wawili na bado zina madarasa 7.

  Usafiri kwa vijiji vilivyo kwenye delta ni matatizo makubwa na nyumba zao ni vigorofa ambavyo chini vinakuwa supported na miti na kuanzia mita 2 au 3 kwenda juu ndiyo kuna vijumba, wamejenga kwa mfumo huo ili kuepuka adha ya mafuriko.

  Walimu wakipangiwa kwenda huko, siku wakienda kuripoti na kupandishwa kwenye mtumbwi ili kupelekwa kwenye kituo chake cha kazi, akiondoka harudi tena anaona ni heri aache kazi kuliko kwenda kuishi kwenye hayo mazingira magumu.

  Mji wa Kibiti ndio ambao umechangamka zaidi kuliko hata makao makuu ya wilaya ambayo ni Utete. Kwa kifupi wafanyakazi wengi wa serikali wakipangiwa kwenda Rufiji kufanya kazi anahisi kama vile kapewa adhabu hata kama anafanya kazi makao makuu ya wilaya, maana usafiri kutoka Makao Makuu ya Wilaya kwenda mahali popote ni matatizo makubwa, ni mwendo wa mitumbwi tu.

  Kwa hiyo Prof. Mtulia anatakiwa kukaza buti maana safari ndo kwanza inaanza na ni ndefu hasa. Ndoto ya maendeleo anayoyataka ni ngumu sana kuifikia na inaweza kumchukua miaka mingi sana kufika huko. Wingi wa shule bila walimu hauna maana yoyote.

  Ili kufikia hayo maendeleo kwanza anatakiwa kukazania usafiri wa kuaminika, japo sijui huko kwenye delta atafanya nini maana ni hatari tupu.
   
 5. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ninavyofahamu Prof. Mtulia sio mwanasiasa. Kulikuwa na vacuum kubwa ya viongozi waadilifu au niseme , kulikuwa na mmomonyoko wa uadilifu wa uongozi, nyakati za miaka ya mwisho ya mstaafu Mh. Ali Hassan Mwinyi.

  Kama sikosei, aliombwa kugombea ubunge-ili aweze kuongoza wizara. Nafikiri hili la kuwa Waziri liliwekwa pembeni baada ya 'system' kuji organise na kuleta 'mafisadi'- Huyu jamaa ni 'Msela'

  Dilunga you have not done him justice! Mengi yaliyoandikwa ni pamoja na tafsiri za mwandishi wa habari. Kuna ukweli lakini umekuwa toooooo direct naye kiasi inaonekana umekabwa na koo. Tema mate ndugu!:D


  I have too much respect for him... I shall leave it here.

  Tunahitaji wabunge wenye makini na udilifu wa kazi kama huyu bwana.
   
 6. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Duuh kazi ipo!!
   
 7. jimmyfoxxgongo

  jimmyfoxxgongo JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2016
  Joined: Jan 23, 2013
  Messages: 3,197
  Likes Received: 4,789
  Trophy Points: 280
  pumzika kwa amani mzee mtulia
   
 8. misasa

  misasa JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2016
  Joined: Feb 5, 2014
  Messages: 5,461
  Likes Received: 2,525
  Trophy Points: 280
  Amefariki?
   
 9. jimmyfoxxgongo

  jimmyfoxxgongo JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2016
  Joined: Jan 23, 2013
  Messages: 3,197
  Likes Received: 4,789
  Trophy Points: 280
  yap amefariki
   
Loading...