Prof. Ibrahim Lipumba na Maalim Seif wana wake, watoto (familia)?

chilamjanye

Senior Member
Oct 5, 2007
110
3
Wake Za Akina PR. Lipumba na Seif Sharifu Hamadi Kitendawili

Jamani wana JF sijawahi kusikia juu ya Mke wa Lipumba na Hamadi au bado wapowapo kwanza, Mwenye data Tufahamishe.

Hivi wameoa hawa maana nataka kuwajua mafirst lady wao

Hakuna mwenye habari ya hawa mafirst Lady wa mabwana hawa?

=======
Mwingine (Oktoba 2012):

Prof. Lipumba, Maalim Seif ni wahuni?

Tarehe 29/09/2012 Jumamosi muda wa saa nne asubuhi napigiwa simu nahitajika haraka Dar tarehe 30/09/2012 Jumapili kabla ya saa mbili asubuhi. Najaribu kutafakari haraka haraka nini chakufanya either nitumie usafiri binafsi au niwasiliane na Presicion kuangalia kama wangekuwa na ndege ya jioni. Ghafla mfanyakazi mwenzangu ananizindua katika tafakari "Mheshimiwa Ngongo usipate taabu nenda stand Sai Baba wana bus linaloanzia Karatu kwenda Dar linafika Arusha Saa tano mchana"Bila kuchelewa nafanya uamuzi wa kwenda stand ya mabus kweli nakutana na wakatisha tiketi wa Sai baba wananiahakikishia bus la Karatu kwenda Dar liko njia nilisubiri kwaajili ya safari ya kwenda Dar.

Saa tano na robo safari ya kwenda Dar inaanza bila matatizo,ninabahatika kukaa siti za mwanzo za watu wawili jirani yangu tunafahamiana sana ni mmiliki na mundeshaji wa Hotel 711 iliyoko maeneo ya Stand ya mabus makubwa. Muda wa saa nane tulikuwa tumeshafika maeneo ya Same tunakutana na mabus madogo mengi yakiwa na bendera za CUF. Mjadala unaanza wanachama wa CUF wanakwenda wapi dereva anatuzindua hamjui CUF watakuwa na mkutano mkubwa kesho [Jumapili] Arusha !. Tunaulizana kama mkutano unafanyika Arusha kwanini wasombe wanachama na wapenzi toka Dar ?. Muda unazidi kwenda giza linazidi kutanda tunakutana na bus la mwisho maeneo ya Kwedikwazu linakamilisha jumla ya mabus kumi na tano !.

Mwl Nyerere aliwahi kumwita Mheshimiwa John S Malecela mhuni kwasababu ya kushindwa kumudu majukumu ya kazi ya Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu wa JMT na kushindwa kumshauri vizuri Rais wa JMT wakati huo Mzee Ali Hassan Mwinyi .Nalazimika kukopa maneno ya Mwl Nyerere, Maalimu Seif Hamad,Prof Ibrahim Lipumba na viongozi wote wa CUF ngazi ya taifa na Mkoa wa Arusha ni wahuni wa kupindukia.

Ikiwa viongozi wa CUF wanaweza kusafirisha wapenzi na wanachama wake zaidi ya kilometa mia saba sasa naelewa ni kwanini mikutano yao inayofanyika Dar inakuwa na umati mkubwa wa wanachama na wapenzi lakini huo huo wanakosa mwakilishi [Mbunge] katika Jiji la Dar yamkini watakuwa wanasomba wanachama kutoka Rufiji, Pemba, Unguja, Lindi na Mtwara.

Naomba kuwasilisha.
Nakala Ritz , PakaJimmy, Buchanan, TUMBIRI, nngu007, Bigirita, Pasco, FaizaFoxy, Filipo, KakaKiiza , maggid, Preta, Matola, Nguruvi3, BAK, Mkandara, JokaKuu yegella, Ogah FJM, Richard, Crashwise, Molemo, Mzee wa Rula, Exaud Mamuya, Mzee Mwanakijiji

=======
Notable responses:

..mwaka 1995 Prof.Lipumba alikuwa anaandamwa na CCM kwa kuvunja ndoa ya mama mmoja wa Kichaga anaitwa Georgina.

..CCM walikwenda mbali zaidi na ku-question Uislamu wa Prof.Lipumba kwasababu ya kuwa involved na mwanamke Mkristo.

..baada ya uchaguzi ule na mpaka leo sijasikia tena kama alikuja kumuoa huyo mama au waliachana.

NB:

..hata Pius Msekwa naye alipoonyesha nia ya kugombea Urais naye alitumbukizwa ktk kashfa kwa kulazimika kuthibitisha kwamba ndoa yake na Anna Abdalah ni halali.
Prof. Lipumba ana mke na watoto. Mke wake anaitwa Georgina Mtenga anafanya kazi UNICEF hapa DAR. Ila alimuoa baada ya Georgina kutengana na mme wake wa kwanza (amezaa naye mtoto) anaitwa Kweka.

Ndio maana katika kampeni yake ya mwisho pale Jangwani Rais JK aliwakandia Pro. Lipumba na Dr. Slaa kwa kusema "Wengine walichukuwa wake za watu(Lipumba) na wengine wanachukua wake wa kuazima(Slaa)"

Habari zaidi kuhusu familia soma hapa=>Yaliyojiri Ubungo Plaza: Prof. Lipumba ametangaza nia ya kuchukua fomu ya kugombea Urais wa JMT
 
Mwiba na Kiranga wanaWAJUWA ati.

Mwiba hebu tuambie hawa mabana wawili, wake zao wapo au wao ni Wa-Anglican?

Mwiba Mwibaaa, where the hell r u when we need you? (Eminem about Kanye West).
 
Last edited by a moderator:
Lipumba ana mke ila ni Mkristo (if not mistaken) cause iliwahi kuandikwa kwamba huyo mama aliachana na bwana wake na yeye akachukua nafasi na anafanya kazi UN kama sikosei.

Mwenye data zaidi please...
 
Mbona mnahoji wake wa wagombea badala ya ilani zao.

Mafirst lady watasaidia nini. Salma JK anatusaidia nini zaidi ya kutumia raslimali yetu kumkampenia JK
 
Habarini ndugu zangu wana jamvi?wataalam mi nahitaji kujua kama profesor lipumba ana mke na watoto. Kwani sijawahi sikia kuhusu familia yake, wengine wananiambia hajawahi kuoa ka spendi maisha yake kwenye elimu. Je ni kweli? Kama ana mke na watoto nitashkuru kama ntafahamishwa. Sio umbea ila ni vizuri kumjua prominent figure kama yeye. Tokea 1995 anagombea urais na wala hachoki. Karibuni jamvini waungwana.
 
Hata mimi nasikia hana mke wala mtoto, ila sidhani kama kupiga kitabu could be an excuse of net getting mariied.
Mbona kuna maprofessor wengi tu wana wake/watoto. Labda ana shida kaka.
 
Najua kwamba hana mke ila sijui kama hakuwahi kuoa, aliachika au ilikuwaje hadi akawa hana mke
 
hata mie nilishasikia kuwa hajaoa, lakini nadhani ni maisha yake binafsi tusiyachimbe sana. ila kwa umri na nafasi yake ingependeza kuwa na familia kwa kweli
 
Heeeeeeeee mie nimesikia leo mara ya kwanza. Loooohhhh! hata hivyo ni maamuzi binafsi. Kuoa si lazima kama hakuna ulazima. Mbona mie sina mke?
 
ana mke bwana kama sikosei mchaga,na alikuwa na katoto niliwaona miaka labda mitano iliyopita
 
Mwambie am single/available!!!!:teeth::embarrassed:.......ukishakuwa public figure na hujaoa mambo yanakuwa complicated kidogo-mtu unayemtafuta kufit profile lako inakuwa kazi na wengi inabaki kuwa utata kakupenda wewe kama wewe au kakupenda sababu ni mtu mzito....mungu amuongoze ktk kukabiliana na huo utata!
 
matola dont be stupid and useless. Imagine kama angeshinda urais, ingekuaje bila first lady huoni kama ni kituko?bluu balaa na miss judith asanteni kwa busara zenu. Maisha yake yana tuhusu ni na lazima tuyajue. Je jogoo lake halipandi mlima? Wekeni mambo hadharani waungwana. Wengine kama imewachoma potezeeni sio lazima m coment.

huo sasa uchokozi....:redfaces::redfaces:
 
matola dont be stupid and useless. Imagine kama angeshinda urais, ingekuaje bila first lady huoni kama ni kituko?bluu balaa na miss judith asanteni kwa busara zenu. Maisha yake yana tuhusu ni na lazima tuyajue. Je jogoo lake halipandi mlima? Wekeni mambo hadharani waungwana. Wengine kama imewachoma potezeeni sio lazima m coment.

Mzee Moi alioa ? baada ya kumuacha mama Ngina mwaka 1983 . Jibu ni kwamba hakuoa . Rais wa sasa wa Botswana ndio anatafuta mchumba. urais sio ufalme.
 
Bruce Lee,

..mwaka 1995 Prof.Lipumba alikuwa anaandamwa na CCM kwa kuvunja ndoa ya mama mmoja wa Kichaga anaitwa Georgina.

..CCM walikwenda mbali zaidi na ku-question Uislamu wa Prof.Lipumba kwasababu ya kuwa involved na mwanamke Mkristo.

..baada ya uchaguzi ule na mpaka leo sijasikia tena kama alikuja kumuoa huyo mama au waliachana.

NB:

..hata Pius Msekwa naye alipoonyesha nia ya kugombea Uraisi naye alitumbukizwa ktk kashfa kwa kulazimika kuthibitisha kwamba ndoa yake na Anna Abdalah ni halali.
 
Wikipedia wanasema ameoa na ana family ila hawajafafanua zaidi mi nimeishia hapo mwenye info atuwekee
 
Back
Top Bottom