Prof. I. Lipumba: Vyama Vya Upinzani Kuaandaa Maadamano Nchi Nzima Kumshinikiza JK Kuchukua Hatua.

ni muda muafaka na ishara njema kwa vyama vya siasa kuunganisha nguvu na kuweka mbele maslahi ya taifa kwanza kabla ya vyama vyao na kujenga imani kwa watanzania walio wengi kuwa vyama ya upinzani viko makini katika kusimamia mabo ya msingi na kupingana na kila aina ya dhuluma na ufisadi ambao unapelekea wo kuishi maisha ya kubahatisha. kwa cdm ni turufu kwani usahiba wao unaweza kuwasaidia kuingoa ccm madaarakanikwa urahisi zaidi kwa pandee zote mbili za muungano. japokuwa kwa cuf naona kunaviongozi 2 tu kwa upande wa bara pro lipumba na julius mtatiro. kwa upande mwingine naona hii inaweza kuwaadvantage kwa cdm kupenya maeneo cuf yenye ushawishi mkubwa kwa mgongo wa opposition partinesrship, na hii ni kwa sababu cdm wana viongozi wengi wenye ushawishi mkubwa wa siasa za majukwaani kama G lema, sugu mnyika kabwe, nassari, mdee, kakunguru ben sanare etc. pia ni wakat mzuri kwa viongozi wa TLP nA nccr kujitambulisha kwa wananchi katika sehemu mbalimbali za nchi. pamoja na hayo naona ni wakati mzuri kwa vyama hivi kuendelea kuvuna wanachamana viongozi kutoka ccm na kujiongezea nguvu kama mataji kwa ajili ya chaguzi zijazo. washikane katika hoja hizi za kitaifa. Pamoja tutafika!
 
Nina unga mkono mpango wa maandamano ya nchi nzima.Nchi imekosa dira na mwelekeo. RIP Horace Kolimba
 
Sababu kubwa Chadema wanasema CUF ni CCM B sasa kuna maandamano hapo kama yatakuwepo Chadema hawawezi kushiriki.

Na kwa hiyo yatakuwa maandamano ya vyama vyote maana CCM itawakilishwa na CUF.
Siasa kweli kazi, wataalamu wetu msitoke kwenye fani zenu kukimbilia siasa maana ni maigizo.
 
Sababu kubwa Chadema wanasema CUF ni CCM B sasa kuna maandamano hapo kama yatakuwepo Chadema hawawezi kushiriki.

Wewe unasema kama nani vile ndani ya CDM? Ninavyo elewa mimi mwana CDM hutanguliza maslahi ya Taifa mbele.KUWA MJANJA KAMA NYOKA NA MPOLE KAMA NJIWA BANA
 
Watanzania sasa tunayo kazi moja tu, nayo ni kuiondoa ccm madarakani ifikapo 2015. sababu tunazo, nia tunayo, na uwezo tunao! Ccm wamekuwa chama cha janga kwa taifa letu.
 
Sababu kubwa Chadema wanasema CUF ni CCM B sasa kuna maandamano hapo kama yatakuwepo Chadema hawawezi kushiriki.

Kwa hiyo yatakuwa maandamano ya vyama vyote maana CCM itawakilishwa na CUF.

Siasa kweli mazingaombwe.
 
Haya yakiwa ni maandamano ya wapenda maendeleo na wapiga ufisadi yatakayo wahusisha vyama vyote hata kama ni ccm wenye uchungu na nchi watasaidia sana kuangusha ngome ya mafisadi. Sote kwa pamoja inawezekana
 
Sababu kubwa Chadema wanasema CUF ni CCM B sasa kuna maandamano hapo kama yatakuwepo Chadema hawawezi kushiriki.
Nafikiri kwa hali ilivyo hivi sasa, Lipumba ameamua kurudisha heshima ya chama chake. Ndiyo maana kwenye petition ya Zitto aliwaagiza wabunge wa CUF wote kusaini ile petition. Otherwise angeweza kuendeleza msimamo wao wa awali wa kupinga kila kitokacho kwa CHADEMA. Kwa kuwa wakati wote chadema wamekuwa wakitetea maslahi ya nchi, nina uhakika hawatakuwa na ajizi kuungana na vyama vingine kwa ajili ya hili.
 
Hayo maandamano sidhani kama Chadema watakubali kushiriki...

C.d.m sio chama cha upinzani au unaona cuf ni c.c.m?cuf bara na cdm wote ni wapinzani,magamba mlifanya hila tu kuwachachafya cuf Znz ili waingie ndoa ya lazima na nyie!bara mmejaribu kuleta sumu zenu za udini ili kudhohofisha upinzani ila mmestukiwa,wapinzani wanaanza kuwa na lengo moja sasa!sahihi za kutokua na imani kwa pm nh mwanzo mzuri
 
wamemiss virungu na maji ya kuwasha...ila itapendeza kama kwenye hayo maandamano viongozi ndio watakuwa mbele.

Giza lililomo kichwani mwako ni la kutisha mno. Kama una masilahi na hao mafisadi jiandae kutafuta njia mbadala. Utalia na kusaga meno.
 
Kwa hiyo yatakuwa maandamano ya vyama vyote maana CCM itawakilishwa na CUF. Siasa kweli mazingaombwe.

Good observation.

Siasa bana! Huyo Lipumba na chama chake wanatafuta namna ya kutoka baada ya kuanza kusahaulika. Well, la msingi huyo mtu anayeitwa Jusa huko huko Zanzibar. Kwa ubaguzi wake hahitajiki Tanganyika.
 
Na mimi naingia barabarani kwa ajili ya taifa langu na vizazi vijavyo!itikadi pembeni,ila hz ni dalili nzuri,maana mzuka waliokua nao wananchi tunasubiri wa kuanzisha tu!mambo yanaweza yakakolea na tusifike 2015 kama hawaamini wasubiri waone!
 
Haya yakiwa ni maandamano ya wapenda maendeleo na wapiga ufisadi yatakayo wahusisha vyama vyote hata kama ni ccm wenye uchungu na nchi watasaidia sana kuangusha ngome ya mafisadi. Sote kwa pamoja inawezekana

Pokea 'like' kabisa!!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom