Mjomba wa taifa
JF-Expert Member
- Apr 20, 2012
- 231
- 161
Baada ya kuwa mwanamapinduzi wa kweli asiepindishwa katika ukweli anaouamini Marehemu Profesa Seith Chachage aliwahi kupewa nafasi ya ukuu wa Mkoa wa Mbeya na Rais aliyetangulia. Kwa kuheshimu dhana ya taaluma aliyonayo na mbinu chafu za serikali za kutaka kumziba mdomo, Prof Chachage alimshukuru Rais na kumwomba asimpe majukumu hayo kwani bado alikuwa anapenda kuendelea kufundisha wanafunzi pale UDSM.
Miaka michache baadae tunamwona Dr. Michael Kadeghe anafurahia kuwekwa katika kapu moja na Makada wachanga wa CCM wanaopewa promotion na chama chao kwa kupewa ukuu wa Wilaya.
Mtaalamu huyu wa elimu ya lugha wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam anashangilia kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya anaweka chaki chini anakwenda Wilayani kukimbizana na watanzania masikini ili walipe michango ya Mbio za Mwenge.
Kituko kingine ni pale Mtaalamu wa Madini, Dr. Dalali Kafumu anavua Ukamishna wa Madini (madaraka ya juu kabisa wizarani chini ya katibu mkuu) anavaa kofia na fulana ya kijani anapanda jukwaani kudanganya wananchi wa Igunga maisha bora. Kabla hata ya Mwaka mmoja kuisha anapoteza Ubunge wake kwa kutumia mbinu chafu kuingia madarakani. Masikini Dr. Kafumu hana Ubunge wala U-Kamishna tena, tamaa ya Mzee fisi kakosa sherehe zote mbili.
Hivi wataalamu wetu lazima wawe wanasiasa? nani mjinga kati ya mwananchi masikini ambaye hakwenda shule dhidi ya yule mtaalamu anaeacha kutoa huduma ya elimu aliyonayo, aliyosomeshwa na kodi za masikini anakana taaluma yake na kwenda kukimbiza mbio za mwenge?
Kwani Prof. Chachage hakujua ukuu wa Mkoa una masilahi zaidi ya kufundisha???