Prof. Chachage alikataa ukuu wa Mkoa, Dr Kadeghe kashangilia ukuu wa Wilaya, Dr. Kafumu mhhhhh!

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Baada ya kuwa mwanamapinduzi wa kweli asiepindishwa katika ukweli anaouamini Marehemu Profesa Seith Chachage aliwahi kupewa nafasi ya ukuu wa Mkoa wa Mbeya na Rais aliyetangulia. Kwa kuheshimu dhana ya taaluma aliyonayo na mbinu chafu za serikali za kutaka kumziba mdomo, Prof Chachage alimshukuru Rais na kumwomba asimpe majukumu hayo kwani bado alikuwa anapenda kuendelea kufundisha wanafunzi pale UDSM.

Miaka michache baadae tunamwona Dr. Michael Kadeghe anafurahia kuwekwa katika kapu moja na Makada wachanga wa CCM wanaopewa promotion na chama chao kwa kupewa ukuu wa Wilaya.

Mtaalamu huyu wa elimu ya lugha wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam anashangilia kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya anaweka chaki chini anakwenda Wilayani kukimbizana na watanzania masikini ili walipe michango ya Mbio za Mwenge.

Kituko kingine ni pale Mtaalamu wa Madini, Dr. Dalali Kafumu anavua Ukamishna wa Madini (madaraka ya juu kabisa wizarani chini ya katibu mkuu) anavaa kofia na fulana ya kijani anapanda jukwaani kudanganya wananchi wa Igunga maisha bora. Kabla hata ya Mwaka mmoja kuisha anapoteza Ubunge wake kwa kutumia mbinu chafu kuingia madarakani. Masikini Dr. Kafumu hana Ubunge wala U-Kamishna tena, tamaa ya Mzee fisi kakosa sherehe zote mbili.

Hivi wataalamu wetu lazima wawe wanasiasa? nani mjinga kati ya mwananchi masikini ambaye hakwenda shule dhidi ya yule mtaalamu anaeacha kutoa huduma ya elimu aliyonayo, aliyosomeshwa na kodi za masikini anakana taaluma yake na kwenda kukimbiza mbio za mwenge?

Kwani Prof. Chachage hakujua ukuu wa Mkoa una masilahi zaidi ya kufundisha???
 
Mkuu umetukumbusha jembe letu Mzalendo wa ukweli Prof. Chachage, R.I.P, ambaye amefariki na UDSM imekufa!!
ulaaniwe sana Prof Mkandala.

Hapo pa buluu hapo, kama vile sijaelewa! Kaufafanuzi kidoogo pliiiiz!
 
Mkandala ndie anahusika na kushuka kwa hadhi ya mlimani Kama tanuru la fikra, yeye na bana na mwenzao kabudi ni wachumia tumbo, RIP chachage
 
Mkuu, baada ya Prof Mkandala kujua kuwa Prof. Chachage atachukua VC, ilibidi ametengenezee zengwe na kumuuwa ili asiwe na upinzani, pia akaona auwe nguvu za DARUSO.... anyway ulikisoma kitabu cha Prof Chachage MAKUWADI WA UCHUMI?

Ahsante kwa kuniongezea ufahamu. Hicho kitabu sijakisoma, je naweza kupata soft copy? (kama unayo)!
 
Mkandala ndie anahusika na kushuka kwa hadhi ya mlimani Kama tanuru la fikra, yeye na bana na mwenzao kabudi ni wachumia tumbo, RIP chachage

teh teh teh!...Sidhani kama uchaguzi wa viongozi wa chuo ulikuwa sahihi sana.Ila wanachuo wengi walitaka kuhakikisha Luhanga haachi nyuma wateule wake. Na Luhanga alikuwa kichwa kweli kweli pamoja na kuwa mr Misifa.
 
Baada ya kuwa mwanamapinduzi wa kweli asiepindishwa katika ukweli anaouamini Marehemu Profesa Seith Chachage aliwahi kupewa nafasi ya ukuu wa Mkoa wa Mbeya na Rais aliyetangulia. Kwa kuheshimu dhana ya taaluma aliyonayo na mbinu chafu za serikali za kutaka kumziba mdomo, Prof Chachage alimshukuru Rais na kumwomba asimpe majukumu hayo kwani bado alikuwa anapenda kuendelea kufundisha wanafunzi pale UDSM.

Miaka michache baadae tunamwona Dr. Michael Kadeghe anafurahia kuwekwa katika kapu moja na Makada wachanga wa CCM wanaopewa promotion na chama chao kwa kupewa ukuu wa Wilaya.

Mtaalamu huyu wa elimu ya lugha wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam anashangilia kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya anaweka chaki chini anakwenda Wilayani kukimbizana na watanzania masikini ili walipe michango ya Mbio za Mwenge.

Kituko kingine ni pale Mtaalamu wa Madini, Dr. Dalali Kafumu anavua Ukamishna wa Madini (madaraka ya juu kabisa wizarani chini ya katibu mkuu) anavaa kofia na fulana ya kijani anapanda jukwaani kudanganya wananchi wa Igunga maisha bora. Kabla hata ya Mwaka mmoja kuisha anapoteza Ubunge wake kwa kutumia mbinu chafu kuingia madarakani. Masikini Dr. Kafumu hana Ubunge wala U-Kamishna tena, tamaa ya Mzee fisi kakosa sherehe zote mbili.

Hivi wataalamu wetu lazima wawe wanasiasa? nani mjinga kati ya mwananchi masikini ambaye hakwenda shule dhidi ya yule mtaalamu anaeacha kutoa huduma ya elimu aliyonayo, aliyosomeshwa na kodi za masikini anakana taaluma yake na kwenda kukimbiza mbio za mwenge?

Kwani Prof. Chachage hakujua ukuu wa Mkoa una masilahi zaidi ya kufundisha???
a couple of months ago i told dr. kafumu about this anomally he was so irritative. now the truth is open . matarajio yake ya kuwa waziri yaliyeyuka na sasa ubunge nao umeambaa. na ucamissioner uliusurrender sijui itakuwaje? POLE SANA COMRADE KAFUMU. JIPE MOYO UTASHINDA KWA JINA LA YESU. MAANA KILICHOKUPONZA SI KINGINE NI KAMPANI YA MAGAMBA
 
Mkuu umetukumbusha jembe letu Mzalendo wa ukweli Prof. Chachage, R.I.P, ambaye amefariki na UDSM imekufa!!

Huyu ni miongoni mwa wanataaluma ambao watakumbukwa daima. Nakumbuka maneno ya Luhanga pale Nkrumah Hall, aliposema, kabla hajafanya maamuzi yoyote pale UDSM ilikuwa lazima afikirie na kujiuliza reaction ya Prof. Chachage.
Sasa hivi ma prof wamebakia kuganga njaa kwenye siasa na ndo hao hao wanatoa first class economist, Mwigulu Nchemba.
 
Kadeghe ful usanii,anayebisha afuatilie habari zake perfect vision.Pia ana unchemba nchemba vile
 
Nilijoin udsm 2006 mwezi wa tisa, ndo kwanza tuliwakuta wanafunzi wana majonzi, mzuka wa kusoma hawana, kuwauliza wanataja chachage. Kwangu lilikuwa jina geni lakini kupitia malalamiko ya wanafunzi, nilitambua he was smart, he was a great thinker
 
U've made my day Mungi
dah kweli tuna serikali kilaza
sitashangaa akapewa ubalozi
QUOTE=Mungi;4477356]Haitashangaza kuona serikali inatangaza mkoa mpya just in favor of Dr. Kafumu[/QUOTE]
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom