Prof. Baregu na Prof. Safari mpo wapi katika kuanguka huku kwa CHADEMA?

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,698
4,693
Maprofesa wawili mulioko ndani ya CHADEMA munafahamika vizuri sana kwa ubobezi wenu. Prof. Baregu ni mzuri sana katika sayansi ya siasa, umewafundisha wengi na wamefanikiwa. Prof. Safari yuko vizuri katika sheria. Ni kesi nyingi umeonesha umwamba wake. Wanasheria wengi ni matokeo ya juhudi zako na uwezo wako. Wote munastahili sifa.

Watu hawa wawili nimekuwa nikiwatumainia sana muisaidie CHADEMA. Sifahamu kwanini kipindi hiki mumekuwa kimya kiasi kwamba msaada wenu hauoneakani. Yawezekana msada wenu hauhitajiki. Muelekeo wa CHADEMA kwa sasa ni aibu kwenu ambao mulistahili kuonesha muelekeo unaofaa.

Binafsi nahisi labda mulifanya makosa kuona malengo ya CHADEMA yalikuwa ni yapi. CHADEMA hawako ktk siasa, wako ktk biashara na bahati mbayamaprofesa wawili, kwa pamoja. Biashara ya udanganyifu hamuiwezi.
 
Chadema inaanguka au hayo ndio matamanio ya ccm? Mmepiga propaganda wenyewe, mmewanunua baadhi ya viongozi wa cdm kwenye ile nia ya Magufuli kuhakikisha anaiua chadema, sasa naona mnajaribu kuchukua mrejesho kama chadema imekufa. Sisi washabiki wa cdm tuko imara na hatuyumbi kwa hizo hujuma za wazi. Hizo mbinu mnazotumia sasa hivi ccm mlifanikiwa enzi za kizazi kilichopita cha NCCR ya Mrema, CUF ya Lipumba nk, ila kwa mbinu hizo za kichovu, sio rahisi kuwapata watu wa kizazi hiki.

Kizazi hiki Ni next level, Kiko digital tayari huku ccm ikiwa bado analogia, ndio maana mbeleko halisi ya ccm ni vyombo vya dola na kundi la watu wasiojulikana. Ili mjue kizazi hiki sio cha kuongozwa na ccm tena, acheni tume huru ya uchaguzi, kisha tuingie kwenye uchaguzi kila mtu awe na nguvu yake ya kisiasa kisha mje mlete mrejesho hapa jukwaani.
 
maprof wana ikili hao, yaan wajiingize kwenye mambo yakipuuz yakina juakal,silinde na wale mamaza wahuni, hawa wanasovu ishu mchangamano sio umbea na wawale mamaza wahuni
Safari alishakaa pembeni usimuunganishe na hao wengine, anajitambua
 
Nilidhani una nia ya dhati kusaidia nchi.Wawili hao ukiwalinganisha na utitiri wa "wasomi wenye digrii zaidi ya 4"walioko ccm na serikalini walioshindwa kusaidia nchi kuwa sehemu yenye amani,ustawi na haki unaona wanastahili kutupiwa mzigo wote wa lawama?

Kuna ma-Dr.waliotenguliwa teuzi wakaanza kulia lia na wengine kusema "waliokotwa majalalani"achilia mbali waliosema ccm kutumia mabavu kubaki madarakani ni halali. Hayo ni matokeo ya Elimu yetu,usiwalaumu
 
Nilidhani una nia ya dhati kusaidia nchi.Wawili hao ukiwalinganisha na utitiri wa "wasomi wenye digrii zaidi ya 4"walioko ccm na serikalini walioshindwa kusaidia nchi kuwa sehemu yenye amani,ustawi na haki unaona wanastahili kutupiwa mzigo wote wa lawama?

Kuna ma-Dr.waliotenguliwa teuzi wakaanza kulia lia na wengine kusema "waliokotwa majalalani"achilia mbali waliosema ccm kutumia mabavu kubaki madarakani ni halali. Hayo ni matokeo ya Elimu yetu,usiwalaumu.
Kwa hiyo CCM ikishindwa, ni halali pia CHADEMA kushindwa? Love of comfort.
 
Kwa hiyo CCM ikishindwa, ni halali pia CHADEMA kushindwa? Love of comfort.
Sijatumia neno "kushindwa". Nimesema "kulaumu".Waliotajwa ni Prof.Safari na Baregu na nimezungumzia mfumo! Hata kina Lamwai hawakuweza kuinusuru NCCR -MAGEUZI kuporomoka. Hawakujua mfumo (siasa na elimu"una nafasi gani.
Yaonekana tunashindwa kuelewana nini tunachozungumzia.
 
maprof wana ikili hao, yaan wajiingize kwenye mambo yakipuuz yakina juakal,silinde na wale mamaza wahuni, hawa wanasovu ishu mchangamano sio umbea na wawale mamaza wahuni
Sijui kama unajua kuwa Prof. Safari aliishaondoka Chadema kwa sababu hizo hizo unazozisema.
 
Sijatumia neno "kushindwa". Nimesema "kulaumu".Waliotajwa ni Prof.Safari na Baregu na nimezungumzia mfumo! Hata kina Lamwai hawakuweza kuinusuru NCCR -MAGEUZI kuporomoka. Hawakujua mfumo (siasa na elimu"una nafasi gani.
Yaonekana tunashindwa kuelewana nini tunachozungumzia.
Lugha anayoijua huyo mlumumba ni moja tu; ya mapambio, ambayo ndio muhimu zaidi kwa tumbo lake.
Kamwe hawezi kuelewa lugha ya mchangiaji anaefikiri na kuchambua maswala
 
Nani ayekwambia kwamba chadema inaanguka? Yaani kuondoka kwa wachumia tumbo ndio kuanguka? Kama mna uhakika Chadema imeanguka wekeni tume huru na msitumie Policcm muone NGONDOIGWA.
 
Utakaa sana,Chadema ipo na itakuwepo,kesho ni njema kuliko jana.
Chadema haifi. Msimu huu wa uchaguzi tunatazamia kuona watu wengi wakihama na hasa wale walikuwa viongozi na wakiangalia hali wanaona hawatapita kwenye mchujo ndani ya Chama. Tunatazamia kuwaona kina Lijualikali wengi. Hasa wakati ule wa kikao cha mwisho cha mchujo wengi watatangaza kuhama. Tumejiandaa kisaikolojia. Chadema ni taasisi imara na hakifi. Safari hii ushindi utakuwa mkubwa sana kuliko uchaguzi uliopita. Kama tu uchaguzi ungekuwa huru chini ya tume huru ya uchaguzi, Chadema kina nafasi na uwezo wa kushinda ngazi ya uraisi na wabunge zaidi ya nusu. Hamahama hiyo ni kawaida na hatutishiki wala hatudanganyiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom