Jioni ya leo tarehe 19/09 kumetokea hali ya sintofahamu Jimbo la Mtama baada ya Prof. Beregu kushindwa kupata Suluhu ya nani asimame kugombea Ubunge jimbo la Mtama Kati ya ndg. Selemani Methew Luwongo wa CHADEMA na ndg Mchinjita wa CUF.
Hali hiyo imetokea leo majira ya saa kumi na moja jioni kwenye kikao kilichofanyika mkwajuni - Mtama kwenye kikao cha ndani ambapo kila mgombea alitoa maelezo yake na Prof. Beregu aliona maelezo yote yana mashiko ndipo aliposema kuwa asimame mbunge wa CHADEMA hapo hapo watu wa CUF waliopo ndani ya kile kikao wakasimama na kusema kwa hasira huku wakimuonyeshea kidole Prof. Beregu kuwa amekuja kuua CUF kwani Jimbo linajulikana ni la CUF na kuanza kuzomea na kusababisha kikao hicho kufungwa Bila maridhiano.