Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Leo Septemba 15, 2016 Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Twaweza imetoa matokeo ya utafiti uitwao "Rais wa Watu" tathimini na matarajio ya wananchi kwa serikali ya awamu ya tano, ambapo wamesema kuwa wananchi wanakubali hatua zinazochukuliwa na serikali mpya inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli, hususani kuhusu uondoaji wa wafanyakazi hewa, sera ya elimu bure na usimamishwaji wa watumishi wa Serikali kutokana na makosa mbalimbali.
Kufuatia ripoti hiyo, Profesa Mwesiga Baregu ameeleza kukosa uhakika na matokeo hayo ya utafiti kwani ulifanyika mwezi wa 6 huku mambo mengi yakitokea ndani ya miezi mitatu iliyopita, ambayo yamewabadilisha mtazamo wa watanzania kuhusu Rais.
Profesa Baregu, pia amesema kuwa utafiti huo umeonyesha asilimia 70 ya watanzania hawakuwa na uelewa wa kisiasa.
Chanzo: Dar24