Prof. Baregu aitahadharisha CHADEMA kuhusu Zitto

CHADEMA Mpya

Member
Jun 5, 2012
84
22
Dar es Salaam. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amewataka viongozi wa chama hicho kutafakari na kudhibiti madhara yanayoweza kukikumba hasa baada ya hatua yake ya hivi karibuni ya kumvua nyadhifa zote, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili.

“Bahati nzuri wamevuliwa uongozi siyo uanachama, binafsi nadhani viongozi wanatakiwa kutafakari na kudhibiti madhara zaidi kwa chama, wakishupaza shingo, lolote litakalotokea watakuwa ni sehemu ya lawama,” Profesa Baregu alisema Dar es Salaam jana.

Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walivuliwa uongozi Novemba 22 mwaka huu, kwa tuhuma za kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho kinyume na katiba, sheria na itifaki za chama.

Profesa Baregu alisema pamoja na viongozi hao kuvuliwa madaraka, mema waliyokifanyia chama hicho hayawezi kuyeyuka na kwamba makosa yao yasikuzwe kiasi cha kufuta mazuri yao katika kujenga chama hicho.

“Ni vigumu kuamini kwamba makosa ya Zitto, Dk Kitila na Samson Mwigamba yanaweza kuyeyusha mema waliyokifanyia chama kama barafu inavyoyeyuka juani.”

Profesa Baregu ambaye alikuwapo katika kikao kilichowavua uongozi Zitto na wenzake alisema kinachotakiwa kufanyika sasa ni kujenga uhusiano ndani ya chama na hasa kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ambao umeanza Novemba 22 na unatarajiwa kumalizika Juni mwakani.

Alitaka hatua dhidi yao zizingatie Katiba ya chama hicho ili kuhakikisha kuwa hazivurugwi na mamlaka nyingine zilizopo ndani ya Chadema akisema mkutano wa Baraza Kuu unaweza kubadili uamuzi wa Kamati Kuu.

“Kinachotakiwa kufanywa ni kuwatangazia wanachama misingi, taratibu na kanuni za kuzingatia katika harakati zao ili kuondoa hali ya watu kufanya mambo kwa kificho,” alisema na kuongeza:

“Ni wazi wengi wapo katika kampeni, ichukuliwe kuwa walioshughulikiwa wamebambwa na iwe njia ya kuonyesha ukomavu katika kustahamiliana.”

Alisema asingependa kuona siasa za kulipizana visasi na kusisitiza kwamba hata kama mwanachama ana chuki binafsi na mwenzake, hatakiwi kutumia chuki hiyo kumhukumu.

“Tuhuma zinazotolewa dhidi ya Zitto na wenzake kwamba wamenunuliwa na chama fulani cha siasa zinahitaji maelezo na vielelezo vya kina ili kuwaaminisha wengi. Nasema hivi kwa sababu historia yao inadhihirisha kuwa wana uchungu na chama chao. Chama kinachoongozwa kwa demokrasia na kinachotarajiwa kushika madaraka ya kuongoza nchi, lazima kionyeshe uwezo mkubwa wa kuvumiliana, kutafakari, kusamehe, kuaminiana na kujenga umoja wenye lengo la kuelekea kusudio lake.”

Source Mwananchi
 
Maji na mafuta siku zote havichanganyiki! Tatizo la CHADEMA ni akili ndogo kuongoza akili kubwa.

Sasaa unategemea nini kipofu akiongoza? Leo hii professor anaongozwa na mhitimu wa elimu ya secondari eti kwa vile tu ni mfadhili wa chama!
 
Kikwete anamuongoza prof j4 magimbi,prof mwandosya,dr mwaki-embe,prof maji marefu nk...
 
Maji na mafuta siku zote havichanganyiki! Tatizo la CHADEMA ni akili ndogo kuongoza akili kubwa.

Sasaa unategemea nini kipofu akiongoza? Leo hii professor anaongozwa na mhitimu wa elimu ya secondari eti kwa vile tu ni mfadhili wa chama!

We jamaa bhana..
Kuna tofauti ya uwezo wa kuwa kiongozi na sifa za kuwa kiongozi!! We endelea kukariri tu mambo!
 
Mwananchi wako kazini badala ya Zitto ndiyo maana kila kukicha ni kampeni .Wanatafuta huruma ya CC muda huu .Mbona wakati akiwatumia kumwandika na kuwalipa huwa hawampatii ushauri juu ya madhaa kwa Chama na Taifa ? Walicheza na watu wenye nia sasa wamesha ona kwamba ukiharibu kila kitu chako kizuri kinapotea na mabaya pekee yanaonwa .Zitto kaanza muda mrefu sna kusaliti Chama hakuanza juzi .Baregu ulimweleza Zitto ? Mwananchi mliandika ?
 
Tatizo Baregu naye ni miongoni mwa watu walio kwenye blacklist ya akina MBOWE na SLAA
 
Huyo Mwandishi wa Mwananchi nae ni Gamba tu... Mabaya yamezidi mazuri x 70! Mbwa akipata kichaa kasha akaanza kumdhuru bwana wake huwa anauawa tu hakuna namna...
 
We jamaa bhana..
Kuna tofauti ya uwezo wa kuwa kiongozi na sifa za kuwa kiongozi!! We endelea kukariri tu mambo!

Tatizo la viongozi wa CHADEMA ni kuwa hawana elimu lakini pia hawana sifa ya kuwa viongozi
 
Huyo Mwandishi wa Mwananchi nae ni Gamba tu... Mabaya yamezidi mazuri x 70! Mbwa akipata kichaa kasha akaanza kumdhuru bwana wake huwa anauawa tu hakuna namna...

Yaani katika watu nilioona humu JF, wewe ni mjinga kuliko wote. Iweje umshambulie mwandishi wa habari badala yaa kumlaumu Baregu aliyenukuliwa maneno hayo? hii kweli ni balaa. akili za bavicha zimefika ukingoni
 
Mwananchi wako kazini badala ya Zitto ndiyo maana kila kukicha ni kampeni .Wanatafuta huruma ya CC muda huu .Mbona wakati akiwatumia kumwandika na kuwalipa huwa hawampatii ushauri juu ya madhaa kwa Chama na Taifa ? Walicheza na watu wenye nia sasa wamesha ona kwamba ukiharibu kila kitu chako kizuri kinapotea na mabaya pekee yanaonwa .Zitto kaanza muda mrefu sna kusaliti Chama hakuanza juzi .Baregu ulimweleza Zitto ? Mwananchi mliandika ?
kama ambavyo daima lipo bize nyuma ya chadema kupamba uongo na uzushi wa chadema
 
Walichokifanya CHADEMA wamenikumbusha mwalimu wangu wa history Tunduru Secondary School(TSS). Mama yule alikuwa anatoa adhabu then anakaribisha utetezi baada ya kuwa umefanya adhabu. Ila yeye alikuwa na busara kidogo anakupa kwanza makosa yako bila kusikiliza upande wako anakuadhibu,cdm wanakuadhibu then makosa yako wanakupa baada ya adhabu. Tehetehetehetehe! Akili kubwa imetawaliwa na akili ndogo kutoa maamuzi. Ninamkubali Lissu lakini kwa hili ameburuzwa
 
Prof Baregu anafaa kuwa kiongozi, lkn kwa ukabila na ukanda wa Chadema hatopata.

Hongera prof kwa kuwa na mawazo huru na si kuwa kibaraka wa Mbowe.
 
Mwananchi wako kazini badala ya Zitto ndiyo maana kila kukicha ni kampeni .Wanatafuta huruma ya CC muda huu .Mbona wakati akiwatumia kumwandika na kuwalipa huwa hawampatii ushauri juu ya madhaa kwa Chama na Taifa ? Walicheza na watu wenye nia sasa wamesha ona kwamba ukiharibu kila kitu chako kizuri kinapotea na mabaya pekee yanaonwa .Zitto kaanza muda mrefu sna kusaliti Chama hakuanza juzi .Baregu ulimweleza Zitto ? Mwananchi mliandika ?

Mkuu, aliyenukuliwa ni Prof BAREGU, mjumbe wa CC ya CHADEMA. Mwananchi wameripoti tu taarifa hiyo. nakushangaa kuilaumu mwananchi
 
Baregu alitakiwa kumtahadhalisha Zitto kuhusu mipango yao ya mapinduzi.
Ila kama kawaida, alikaa kimya akidhani mipango ile ingetimia.
Sasa anatapa-tapa kujaribu kumuokoa Zitto.
Zitto ameshakwisha, anachoweza kufanya Zitto ni kukimbilia mahakamani. Kesi itanguruma mpaka baada ya uchaguzi mwaka 2015.
Hataweza kugombea wadhifa wowote ule, na akishinda, sana sana atabaki kuwa mwanachama wa Chadema, bila ubunge wala cheo chochote kile.
Zitto kwisha kazi yake, akadai mafao yake CCM, atulie.
 
Naomba kujua Chadema hakina msemaji wa Chama? kila mtu anasema maana yake ni nini? au ndo utawala wa kambale kuwa kila mmoja ana sharubu? Kama mtu alikuwa kwenye kikao cha CC na akashiriki katika maamuzi yaliyofikiwa inakuaje sasa anazungumza kama mtu ambaye hakuwepo kwenye kikao? kama ni suala la kuonya kwa nini hakufanya hivyo kwenye kikao? Na viongozi wanoitisha press conference kwa ajili ya kusemea jambo hilo, naomba niwaulize chama chenu hakina utaratibu wa msemaji wake? kwani CC imeomba maoni katika uamuzi waliofanya? Nashindwa kuwaelewa viongozi wa leo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom