Paschal Matubi
JF-Expert Member
- Sep 15, 2008
- 235
- 302
**********************************************************
Waweza kusoma habari hii hapa chini au attachment niliyoambatanisha humu ambayo ni scan ya gazeti la TUMAINI LETU.

{Prof. Baregu aanza kazi SAUT}
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Tanzania (SAUT) kinachomilkiwa na Kanisa Katoliki nchini kimeingia mkataba na Profesa Mwesiga Baregu ambapo atafundisha katika chuo hicho kulingana na mkataba huo.
Hatua hiyo ya Profesa Baregu kujiunga na SAUT inkauja baada ya suala lake na Chuo Kikuu cha D'Salaam kumalizika na kwamba ujio wa profesa huyo unaleta changamoto katika maendeleo ya taaluma ya uandishi wa habari na mawasiliano nchini.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa Profesa Baregu tayari amekwishaanza kufundisha katika kampasi ya D'Salaam ya SAUT ambako kuna wanafunzi wa shahada ya uzamili (MA) na uzamivu (PhD).
Akizungumza na TUMAINI LETU kwa njia ya simu, mkuu wa idara ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Padri (Dk.) Joseph Matumaini alithibitisha tarifa hiyo na kwamba tayari wameingia mkataba na Profesa Baregu na atakuwa akifundisha katika kampasi ya D'Salaam na Mwanza yaliko makao makuu ya SAUT.
Dk. (Padri) Matumaini alisema kuwa kuwepo kwa profesa huyo hapo chuoni SAUT kunaleta matumaini mapya na changamoto katika tasnia ya habari kwa kuwa ana uzoefu mkubwa katika fani mbalimbali kitaaluma.
"Ni kweli Prof. Baregu amekwishaanza kazi SAUT kwa sababu tunatambua mchango wake na tunaamini ataongeza nguvu katika kukiimarisha chuo chetu katika utoaji wa elimu bora", alisema Dk. (Padri) Matumaini ambaye pia ni mhadhiri katika chuo hicho.
Alifahamisha kuwa ni matumaini ya SAUT kuwa Profesa huyo atatumia uwezo na ujuzi wake kitaaluma kuwanufaisha wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho kinacholenga kuleta mapinduzi ya tasnia ya habari na mawasiliano ya umma nchini.
"Sisi tunafahau kuwa Profesa bareu ana mchango mkubwa sana kitaaluma, hivyo tunategemea tutabadilishana naye mawazo kitaaluma katika nyanja tofauti ili kusaidia utoaji wa elimu ukizingatia kwamba chuoa chetu ni ca kwanza kutoa shahada ya uzamili na uzamivu katika tasnia ya habari na mawasiliano", alisisitiza Dk. (Padri) Matumaini.
Alifahamisha kuwa mkataba alioingia profesa huyo ni wa miaka mitatu ambao hata hivyo unaweza kupitiwa upya kila unapomalizika.

Chanzo: Gazeti la TUMAINI LETU
Mmiliki wa gazeti: Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la D'Salaam
Toleo la Gazeti: Namba 00298, February 19, 2010
Sehemu ya Gazeti yenye habari: Ukurasa wa 04