Prof Assad: Utawala wa Magufuli haukuwa na Nia njema na taifa letu

Acha wazimu kijana. Mungu awalaani wote mnaotetea hili taifa kuangamizwa kwa utawala wa Mzee Wenu aliekwenda kuzificha nyaraka za MANUNUZI YA NDEGE/SGR/STIGLER'S kwake chato chini ya uvungu wa kitanda chake ili zisikaguliwe, mlaaniwe nyinyi pamoja na vizazi vyenu.

(1) Tundu Lissu aliongea ukweli kipindi cha huyo kichaa, aliishia kupigwa risasi 32.

(2) Ben Saanane aliongea ukweli, aliishia kupotezwa mpaka leo hajulikani alipo.

(3) Jakaya Kikwete aliongea ukweli kuhusu kuji mwambafai, aliishiwa kuambiwa na Magufuli kwamba "Anawashwa Washwa".

(4) Huyu Prof Assad aliongea ukweli kwamba Trillioni 1.5 hazijulikani zilivyotumika na akaishia kutukanwa, kudhalilishwa na kufukuzwa kazi hata kabla ya muda wake, na angeongea zaidi maswala haya ya kunyimwa nyaraka za SGR/AIR TANZANIA/STIEGLER'S pengine mngempiga mabomu ya kivita kabisa badala ya Risasi.

Kipindi cha utawala wa Magufuli, mtu aliesoma (PhD au Dr) akiongea ukweli alikua haeleweki na aliitwa msaliti, ila mnafiki akiongea uongo ndio anaeleweka na kusifiwa. Ilifikia hatua mpaka ma Profesa wakubwa walilijua hili wakaamua sasa na wao kuwa wanafiki wa kiwango cha 4G, ili wapate kula.

● CAG Kichere ameteuliwa na huyo huyo Magufuli, ila mbona amekua mkweli na ameweka wazi ufisadi wote hadharani???

● Speaker Ndugai ameteuliwa na huyo huyo Magufuli, na alikua akisifiwa na Magufuli, na alishiriki kumdhalilisha na kumtukana CAG Prof Assad, mbona ameanza kupata akili na amemgeuka Magufuli mbele ya bunge???

● Mama Samia alichaguliwa na huyo huyo Magufuli, ila mbona anaongoza nchi kwa uwazi, ukweli na uhuru bila kuwa mnafiki na muongo???

UTAWALA WA MAGUFULI HAUKUA NA NIA NJEMA KWA TAIFA LETU, ALIKUA MBINAFSI SANA, ALITAKA KUANZISHA MAMBO MENGI SANA YASIOWEZEKANA HALAFU RAIS AMBAE ANGEFUATIA YANGEMHARIBIKIA MIKONONI MWAKE. . . ILI YEYE MAGUFULI ANGESIFIWA BAADA YA KUONDIKA KWAMBA ALIANZISHA JAMBO FULANI NA FULANI NA RAIS AMBAE ANGEMFUATIA ANGETUKANWA KUSHINDWA KUYAENDELEZA.

#Wamejua kwamba zama za "UONGO, UONEVU NA UFISADI" umekwisha sasa, zama hizi ni za "UKWELI NA UWAZI" ukiwa muongo unaumbuliwa mchana kweupe na unapigwa chini.[/B]
Achana na fala hilo... Kunuelewesha fala ni kupoteza nguvu zako tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Assad inatosha sasa mwanaume kuwa mtu wa visasi ivo haipendezi tena kwa marehemu ambae hawezi hata kukujibu kama ulikuwa Unania ya kukosoa ungesema wakati yu ngali hai ili upambane nae ila kwa sasa tunakuona mnafiki tu, Tena nashauri mama akuweke kando tu mana unaonesha kujua kila kitu kitu ambacho ni kibaya kwa kiongozi, TUMEKUCHOKA
 
Ili Prof Assad na wengine wote wanaotaka kuichafua oil chafu wanatakiwa wafanye kinyume na Magufuli kama
"NAAAM....!

Miradi yake mingine inaleta foleni na mingine hasara? Ni rahisi tu, kwa nini tuendelee na Ma-foleni na Ma-hasara? ...Nashauri Vunjeni Madaraja na Flyovers zote, Ng'oeni reli zote especilly SGR, uzeni Ndege zote na vivuko vyote nchini, Uza Meli zote Mpya zilizozinduliwa, kule Ziwa nyasa, simamisheni Ujenzi wa Bwawa la umeme, Gaweni Migodi yote, Binafsisheni Milima, Maziwa na Mbuga.

Bomoa Bandari zote zilizoboreshwa ikiwemo Mtwara, Tanga na Dar, Jengeni moja ya Wachina kwa mkataba wa miaka 100...rudisheni Ada shuleni tukuze uchumi, Wapeni Matajiri Exemptions za kodi, Ruhusuni Makinikia kwenda nje, Vunjeni Masoko mapya ya Madini mikoani, ...Charaza Bakora Machinga mjini, Mwaga wali wa Mama Ntilie.

Vunja vyama vya wakulima na utaratibu wa stakabadhi ghalani, Ruhusuni Uhuru wa Mashoga, Mateja kwa wingi mtaani, madawa ya kulevya n.k....pia Msisahau kuifunga ile Mahakama ya Mafisadi,....kwa uchache tu Hakika hapo sasa pengine Tanzania itakuwa kama ULAYA, Tanzania ya Asali na Maziwa!.

Vunjeni makao makuu Dodoma mrudishe serikali Dar.

Hapo sasa mtakuwa mmemkomoa Magufuli na watoto wake watashinda njaa ili anyooke kabisa.



Nawasilisha
Asad na type ya wanakosoa kila kitu cha mwendezake ni Njaa kali wanazo , huyu mzee inaonesha anataka kuridi kwenye regime ya mama tena kwa top position, Tunamshauri mama aendelee kumuacha nje ya ulingo wa kisiasa
 
Kama ana kisasi cha kufukuzwa kazi aseme tu, ukiachana na Ndege, bwawa la umeme, na sgr... Utawala wa Magufuli ulijenga zahanati na vituo vingi vya afya kuliko idadi ya vilivyokuepo toka tumepata uhuru. Magufuli alitoa elimu bure toka primary mpaka secondary, pia idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu ilikua kubwa than ever before...

Assad atuambie utawala wa awamu ipi ulikua na dira anayoiona yeye? Hata kama wanatumwa hii ni too much hata sie tusiosoma tunaanza kushtuka.
 
Assad inatosha sasa mwanaume kuwa mtu wa visasi ivo haipendezi tena kwa marehemu ambae hawezi hata kukujibu kama ulikuwa Unania ya kukosoa ungesema wakati yu ngali hai ili upambane nae ila kwa sasa tunakuona mnafiki tu, Tena nashauri mama akuweke kando tu mana unaonesha kujua kila kitu kitu ambacho ni kibaya kwa kiongozi, TUMEKUCHOKA
Angeuliwa familia yake ungeihudumia wewe?
 
Kuliko kufuata ushauri wa profesa wa Tanzania ni bora ukafuate ushauri wa darasa la saba Kishimba utafanikiwa.


Maprofesa muda wote ni theory tu, sasa watu hawali theory
Ahahahaaaa . Kwa kweli Kishimba ni nouma , namkubali humo bungeni.

Lakini Assad alikuwa sahihi . Sema mwendazake alipendelea upande wa sifa nzuri na si negative kwake

Odhis *
 
Kama ana kisasi cha kufukuzwa kazi aseme tu, ukiachana na Ndege, bwawa la umeme, na sgr... Utawala wa Magufuli ulijenga zahanati na vituo vingi vya afya kuliko idadi ya vilivyokuepo toka tumepata uhuru. Magufuli alitoa elimu bure toka primary mpaka secondary, pia idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu ilikua kubwa than ever before...

Assad atuambie utawala wa awamu ipi ulikua na dira anayoiona yeye? Hata kama wanatumwa hii ni too much hata sie tusiosoma tunaanza kushtuka.
Huna hata mtoto, ungekuwa naye basi kagua madaftari yake uone hiyo elimu bure mwanao anayoipata ndipo ulie na kusaga meno.
 
Huenda huyu Prof. Assad alifanyiwa kitu kingine kikubwa sana zaidi ya kutumbuliwa maana sio kwa hizi statements anazozitoa. Ana kinyongo cha kutisha!
Labda alipimwa Covid-19 kwa kutumia kile kipimo cha China. You never know buana!
 
Back
Top Bottom