Prof Assad: Utawala wa Magufuli haukuwa na Nia njema na taifa letu

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
8,398
2,000
Kama alivyo nukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari.

Screenshot_20210411-095517.png


FB_IMG_16181241976031414.jpg
 

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
14,303
2,000
Kama alivyo nukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari.

View attachment 1749044

View attachment 1749045
Acheni asemwe !!. Kwani jua halitatoka kesho kwa sababu Maghufuli amesemwa mapungufu yake ?!. Jiwe lingeruhusu uhuru wa habari wala usingemuona wa kumfikiria ushujaa. Toka siku ya kwanza madhaifu yake yangelikuwa wazi. Sasa ilikuwa OLE WAKO useme. Na kwa aliethubutu magazine nzima alimiminiwa mwilini . Huyo Acha asemwe

Odhis *
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,797
2,000
Huyo proff anaj.amba jamba tu...
ilitakiwa aongee wakati Magu yupo.....ajibiwe
aache unafiki
Acha wazimu kijana. Mungu awalaani wote mnaotetea hili taifa kuangamizwa kwa utawala wa Mzee Wenu aliekwenda kuzificha nyaraka za MANUNUZI YA NDEGE/SGR/STIGLER'S kwake chato chini ya uvungu wa kitanda chake ili zisikaguliwe, mlaaniwe nyinyi pamoja na vizazi vyenu.

(1) Tundu Lissu aliongea ukweli kipindi cha huyo kichaa, aliishia kupigwa risasi 32.

(2) Ben Saanane aliongea ukweli, aliishia kupotezwa mpaka leo hajulikani alipo.

(3) Jakaya Kikwete aliongea ukweli kuhusu kuji mwambafai, aliishiwa kuambiwa na Magufuli kwamba "Anawashwa Washwa".

(4) Huyu Prof Assad aliongea ukweli kwamba Trillioni 1.5 hazijulikani zilivyotumika na akaishia kutukanwa, kudhalilishwa na kufukuzwa kazi hata kabla ya muda wake, na angeongea zaidi maswala haya ya kunyimwa nyaraka za SGR/AIR TANZANIA/STIEGLER'S pengine mngempiga mabomu ya kivita kabisa badala ya Risasi.

Kipindi cha utawala wa Magufuli, mtu aliesoma (PhD au Dr) akiongea ukweli alikua haeleweki na aliitwa msaliti, ila mnafiki akiongea uongo ndio anaeleweka na kusifiwa. Ilifikia hatua mpaka ma Profesa wakubwa walilijua hili wakaamua sasa na wao kuwa wanafiki wa kiwango cha 4G, ili wapate kula.

● CAG Kichere ameteuliwa na huyo huyo Magufuli, ila mbona amekua mkweli na ameweka wazi ufisadi wote hadharani???

● Speaker Ndugai ameteuliwa na huyo huyo Magufuli, na alikua akisifiwa na Magufuli, na alishiriki kumdhalilisha na kumtukana CAG Prof Assad, mbona ameanza kupata akili na amemgeuka Magufuli mbele ya bunge???

● Mama Samia alichaguliwa na huyo huyo Magufuli, ila mbona anaongoza nchi kwa uwazi, ukweli na uhuru bila kuwa mnafiki na muongo???

UTAWALA WA MAGUFULI HAUKUA NA NIA NJEMA KWA TAIFA LETU, ALIKUA MBINAFSI SANA, ALITAKA KUANZISHA MAMBO MENGI SANA YASIOWEZEKANA HALAFU RAIS AMBAE ANGEFUATIA YANGEMHARIBIKIA MIKONONI MWAKE. . . ILI YEYE MAGUFULI ANGESIFIWA BAADA YA KUONDIKA KWAMBA ALIANZISHA JAMBO FULANI NA FULANI NA RAIS AMBAE ANGEMFUATIA ANGETUKANWA KUSHINDWA KUYAENDELEZA.

#Wamejua kwamba zama za "UONGO, UONEVU NA UFISADI" umekwisha sasa, zama hizi ni za "UKWELI NA UWAZI" ukiwa muongo unaumbuliwa mchana kweupe na unapigwa chini.[/B]
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,827
2,000
Ana hoja ya msingi sana hata kama huikubali

Amejenga hoja kwa facts sio hisia

Yeye na wenzake watatu 2014 kabla hajawa CAG alitengeneza Business Plan ya ATC wakagundua kwa mazingira yetu haiwezi kuwa viable project wakashauri Serikal isilifufue shirika …

kumbuka wakati huo Mihemko ya Wanasiasa wa Upinzan na wana harakati ilikuwa tufufue shirika letu la ndege lakin wao wali base kwny facts wakashauri kitaalam tuachane nalo

JPM alipoingia akaanzisha Mchakato wa kufufua shirika kwa fedha nyingi tena cash payment

Akaomba feasibility study yake aisome ashauri akanyimwa

Akanyimwa haki ya kukagua nyaraka muhimu

Baadae tunajulishwa Shirika limetengeneza big loss japo lilipewa mtaji wa bure… ungekuwa Wewe ungesema mfanya maamuzi haya ana nia njema kwa Taifa?
Huenda huyu Prof. Assad alifanyiwa kitu kingine kikubwa sana zaidi ya kutumbuliwa maana sio kwa hizi statements anazozitoa. Ana kinyongo cha kutisha!
 

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
8,398
2,000
Ana hoja ya msingi sana hata kama huikubali

Amehenga hoja kwa facts sio hisia

Yeye na wenzake watatu 2014 kabla hajawa CAG alitengeneza Business Plan ya ATC wakagundua kwa mazingira yetu haiwezi kuwa viable project wakashauri Serikal isilifufue shirika

JPM alipoingia akaanzisha Mchakato wa kufufua shirika kwa fedha nyingi tena cash payment

Akaomba feasibility study yake aisome ashauri akanyimwa

Akanyimwa haki ya kukagua nyaraka muhimu

Baadae tunajulishwa Shirika limetengeneza big loss japo lilipewa mtaji wa bure… ungekuwa Wewe ungesema mfanya maamuzi haya ana nia njema kwa Taifa?
Mkuu unapoteza muda wako bure kumuelewesha huyo mataga . Mataga wote Ni zero iq
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,827
2,000
Kaongea sana wakati wa JPM sema kwa kiwango chako cha elimu hukuelewa

Sasa hivi umeelewa kwa kuwa wengi wamesaidia kutangaza habari yake na kuifasiri kwa lugha ya kinyonge ili uelelwa

Weee unadhan Paper kama ile kaiandaa ndani ya siku 21 za maombolezo?
Huyo proff anaj.amba jamba tu...
ilitakiwa aongee wakati Magu yupo.....ajibiwe
aache unafiki
 

ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
10,457
2,000
Kaongea sana wakati wa JPM sema kwa kiwango chako cha elimu hukuelewa

Sasa hivi umeelewa kwa kuwa wengi wamesaidia kutangaza habari yake na kuifasiri kwa lugha ya kinyonge ili uelelwa

Weee unadhan Paper kama ile kaiandaa ndani ya siku 21 za maombolezo?
Kiwango changu cha elimu hukijui
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom