Prof. Assad: Niliondolewa kazini kinyume na taratibu kwasababu nilikuwa sifuati maelekezo ya Mtu

Shehullohi

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
2,545
2,000
Akae kimya, angesema wakati JPM yupo ningemuona kidume.

Atakuwa na matatizo ya usahaulifu huyu alinyanyuliwa na JPM mbele ya kamera na dunia ikitazama akaulizwa Professa kuna tatizo lolote kwenye ukaguzi wako na dhani kuhusu manunuzi ya ndege(niko tayari kusahihishwa) aliufyta akasema hakuna, leo hii anataka kumdanganya nani ili afaidike na nin?. Na alinyoshwa na Spika Ndungai vilevile, atulie alee vitukuu.

Kutoa kauli kama hii ni kuwadharau wengine na kuwaona wana akili za usahaulifu kama kuku buroila.
 

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,668
2,000
Mpaka Leo zile 1.5 trillion alizohoji CAG Assad hazijawahi kutolewa majibu yenye mashiko. Chattel Chattel priorities.
 

doctorz

JF-Expert Member
Aug 10, 2010
917
250
Profesa uchwara aliyejifanya mhimili wakati mihimili iko 3 tu.

Ajaribu kugombea urais basi labda timu gaidi watamsajili 2025.
Siku zote ukweli una uma. Hajadai urais bali ametoa hoja yake ya kuondolewa nafasi ya kazi ajili ya kufata taratibu za kazi na sio maagizo ya mtu. Jibu kwa hoja.
 

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
3,487
2,000
acha kujichekesha kwangu,wewe ni nani mpaka uwapangie watu wakati gani aongee nini. BTW Assad hii sio mara ya kwanza kuongea hiki,au ulitaka akiongea aje akupe ripoti?
Sasa na wewe uache kuni bebisha kwangu....wewe ni nani mpaka unipangie cha kuandika? Umezungusha mikono mpaka akili nayo imezunguka... Lowassa fisadi au si fisadi?
 

doctorz

JF-Expert Member
Aug 10, 2010
917
250
Analazimisha kuonekana ni mtu msomi anaejielewa ana misimamo.

Bahati mbaya alikutana na Chuma.

Nilichokuwa nampendea yule baba JPM ukijifanya wewe ni wa muhimu sana kwenye hii nchi yeye anakuonesha namna ulivyo takataka tu na nchi inaweza kwenda mbele bila wewe hahahah.

Profesa uliondolewa na kidume sasa unalialia nini!!?
Jibu hoja alio toa ni kweli au sio kweli na toa ushahidi toka katiba na sheria za nchi. Labda kama unakubali na wewe yakufike.
 

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
5,641
2,000
Ripoti tu ya soko la k/koo waziri mkuu alitoa wiki hadi leo imekata miezi kimya.
Mpaka Leo zile 1.5 trillion alizohoji CAG Assad hazijawahi kutolewa majibu yenye mashiko. Chattel Chattel priorities.
 

Mulokozijr12

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
2,781
2,000
Analazimisha kuonekana ni mtu msomi anaejielewa ana misimamo.

Bahati mbaya alikutana na Chuma.

Nilichokuwa nampendea yule baba JPM ukijifanya wewe ni wa muhimu sana kwenye hii nchi yeye anakuonesha namna ulivyo takataka tu na nchi inaweza kwenda mbele bila wewe hahahah.

Profesa uliondolewa na kidume sasa unalialia nini!!?
Auditing ni muhimu sana kwa makampuni yanaongozwa na company act na procedures zinaeleweka za kumu engage auditor users wake ni Shareholders and other interested users ila kwa nchi kitu pekee kinachomuongoza CAG ni Katiba tuu ambayo inaelezea kuanzia engagement yake mpaka mengine, na users wake ni General public.

Mwanataaluma huyu anachoongea sio cha kubeza japo yaliopita si ndwele tugange yajayo.
 

REALNEGRONEVABROKE

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
3,483
2,000
Assad ni profesa gani huyu asiyejua kusoma katiba. CAG anateuliwa kwa kipindi cha miaka mitano, baada ya hapo anaweza kuteliwa tena kwa kipindi cha miaka mitano minge kwa ukomo wa miaka kumi. Yeye anseoma kuwa anatakaiwa awe CAG kwa miaka kumi? Alimaliza kipindi cha miaka mitano, halafu hakupewa kipindi kingine cha miaka mitano. Sasa analialia nini, CAG huteliwa na Rais, hachaguliwi na wananchi.

Kumbe ilimuuma sana, ndiyo maana mara tu baada ya JPM kufariki akaanza kelele; anatumaini mama atamrudisha! Halafu ofisi ya CAG ni taasisi siyo mtu; yeye mwenyewe Assad hakuwa anakagua vitabu bali kuna wakaguzi chini ya ofisi ya CAG. Sasa anataka kutuambia kuwa yeye ndiye aliyekuwa anafanya kila kitu bila kufuata eti "maelekezo;" mpuuzi sana huyu.

Kama kuna wakati hela za umma zilitumika vibaya ni wakati wa Kikwete; kuna kipindi ofisi ya rais ilipewa supplementary budget baada ya kukomba hela zote zilizokuwa zimetengewa kabla ya mda wake.
Hasira za Tril 1.5 alizopiga hayati na zile million 400( za umma) za matibabu ya Ndguyai nchini India ndizo zilizotengeneza fitna na hila kumtoa Prof Assad ofisini kabla miaka yake miwili ya kustaafu haijafika.
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
12,214
2,000
Hasira za Tril 1.5 alizopiga hayati na zile million 400( za umma) za matibabu ya Ndguyai nchini India ndizo zilizotengeneza fitna na hila kumtoa Prof Assad ofisini kabla miaka yake miwili ya kustaafu haijafika.
Some katiba kuhusu muhula wa CAG; ni miaka mitano, ambayo Assad alimaliza. Baada ya hapo, Rais anaweza kumteua tena kwa muhula mwinginemmoja wa miaka mitano tena, lakini JPM hakumteua. Asilalamike bali asome Katiba ajue inasemaje.
 

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,037
2,000
Kidume hakipo ila watu kawaachia maumivu makali hawataa wapate recovery...ni kulialia mpaka wanakufa nao
Magufuli pia walimuua kwa kujifanya anajua sana, ndio maana kifo chake kilikuwa na utata mwingi

Na yeye ndio alikuwa akijiona bila yeye nchi haitaenda,
 

goroko77

JF-Expert Member
Jul 9, 2019
1,563
2,000
Hasira za Tril 1.5 alizopiga hayati na zile million 400( za umma) za matibabu ya Ndguyai nchini India ndizo zilizotengeneza fitna na hila kumtoa Prof Assad ofisini kabla miaka yake miwili ya kustaafu haijafika.
Jmn kuiba trilun 1.5 CYO mchezo aibe wapeleke wapi labd ndio kajengea madaraja jmn duh na kufince Kaz zingine
 

Uwazitu

JF-Expert Member
Aug 19, 2019
1,420
2,000
Analazimisha kuonekana ni mtu msomi anaejielewa ana misimamo.

Bahati mbaya alikutana na Chuma.

Nilichokuwa nampendea yule baba JPM ukijifanya wewe ni wa muhimu sana kwenye hii nchi yeye anakuonesha namna ulivyo takataka tu na nchi inaweza kwenda mbele bila wewe hahahah.

Profesa uliondolewa na kidume sasa unalialia nini!!?
Kidume chako kiko wapi kwa sasa?

Chuma hakina ujanja mbele ya kutu.
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
12,214
2,000
Mwenzio kaacha legacy chuo kikuu UDSM na pia as one of the best CAG... vp wewe una legacy yeyote zaidi ya UCHAWA?
Best CAG alikuwa Utuoh; alimaliza kipindi chake akiwa anaheshimika sana. Assad hakuwa na legacy yoyote ya kuacha pale UDSM, aliondoka akiwa associate professor mwenye journal papers 14 tu, nusu yake zikiwa ni local kwenye journals za NBAA na IFM.

Yeye hakusomea kuwa CAG, hiyo ni position ya uteule tu. Baada ya kuondolewa nafasi ya CAG alitakiwa arudi UDSM. Condoleeza Rice alipomaliza kuwa Secretary of State marekani alirudi Stanford kuendelea kuwa profesa wa public policy. Steven Chu (Nobel laureate) alipoacha nafasi ya Secretary of energy, alirudi Stanford kuendelea kama profesa wa Physics.

Kwa nini jamaa huyu analalamikia nafasi za kuteuliwa kila siku na kusahau ukweli huo kwake yeye kama "msomi"? Nadhani alijua ameula miaka kumi tena, akatupilia mbali lecture zake zote. Baada ya kutimuliwa akawa hawezi kufundisha tena kwa vile alishatupa lil desa la kufundishia.

Miaka ya 2006-2007 kulikuwa na member mmoja hapa anaitwa Nungwi alikuwa akimshambulia sana huyu bwana kuwa hana lolote kichwani; inawezekana kweli Nungwi alikuwa akimfahamu jamaa huyu vizuri sana kuliko sisi wengine wakati huo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom